Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Mei 2020, 14:56:46

Bisoprolol
Bisoprolol ni ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Zebeta au Monocor.
Rangi ya Bisoprolol
Rangi yake huwa inatofautiana mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza
Bisoprolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
5mg
10mg
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Bisoprolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu
Hufanya kazi kwa kuzuia matendo yanayosababisha mapigo ya moyo kwenda kasi kwa kupinga utendji kazi wa seli za beta adrenorisepta.
Matendo ya bisoprolol kwenye seli za alfa 1 adrenejik risepta hufanya misuli ya damu kulainika, hivyo hupelekea kupungua kwa upinzani wa mzunguko wa damu ndani ya mishipa ya damu. Matendo haya hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu na hivyo kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri mwilini.
Bisoprolol pia huzaniwa kupunguza matokeo ya renin kwenye figo ambayo huongeza shinikizo la damu kwenye mwili.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Atenolol (Tenormin)
Betaxolol (Kerlone)
Acebutolol (Sectral )
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor, Toprol-XL)
Nadolol (Corgard)
Nebivolol (Bystolic)
Penbutolol (Levatol)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Kazi za dawa ni kama ifuatavyo:
Hutumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acebutolol
Betaxolol
Bisoprolol
Carvedilol
Celiprolol
Clonidine
Digoxin
Diltiazem
Esmolol
Labetalol
Lofexidine
Metoprolol
Nadolol
Nebivolol
Penbutolol
Pindolol
Propranolol
Rivastigmine
Saquinavir
Sotalol
Timolol
Verapamil
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa zingine za Beta bloka
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye kisukari
Wagonjwa wenye haipathairodizim
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye shida ya Ini
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Wagonjwa wenye umri mkubwa
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (ARBs):
Dawa hii haruhusiwi kutumika kwa mtu ambaye hajafikisha umri wa miaka 18
Dawa hii baada ya kutumiwa huanza kazi yake baada ya masaa 2 na kufikia kilele kati ya masaa 4 na haiingiliani na chakula wakati wa ufyonzaji.
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii itumike kwa tahadhari kwa mama mjamzito.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonesha kuwa dawa hii inaweza kuathiri maziwa ya mama anayenyonyesha, hata hivyo itumike kwa uangalifu.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Kutapika
Kichefuchefu
Kuharisha
Kukosa usingizi usiku
Miguu kuwa ya baridi
Mwili kuchoka
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-