Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
21 Aprili 2020, 20:32:49
Bumetanide
Bumetadine ni dawa mojawapo ya kutibu kuvimba kwa mwili kutokana na magonjwa ya moyo na figo. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Loop Diuretics. Dawa hii huwa maarafu kwa majina ya Bumex na Burinex.
Rangi ya Bumetanide
Rangi ya Bumetanide huweza kuwa nyeupe,lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza
Dawa hii haina madhara inapotumika pamoja na chakula
Bumetadine hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa Milligram zifuatazo;
0.5mg
1mg
2mg
Pia hupatikana katika mfumo wa maji kwa ajili ya sindano katika uzito wa 0.25mg/Ml
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Loop Diuretics) na dawa hii ni;
Ethacrynic Acid
Furosemide
Torsemide
Namna dawa inavyofanya kazi:
Hufanya kazi kwa kuzuia ufyozwaji wa Sodiamu Chloraidi na maji kwenye mirija ya figo na hii humpelekea mtu kukojoa mara kwa mara
Sodiamu inapopungua mwilini , mishipa ya damu huongezeka kipenyo na hivyo kushusha shinikizo la damu.
Ufyozwaji wa maji unapozuiwa, maji mengi hupotea kwa njia ya mkojo na hivyo uvimbe wa mwili hupunguza kwa wagonjwa wa moyo na figo.
Kazi ya dawa;
Hutumika kutibu hali ya kuvimba kwa sehemu za mwili kama miguu na uso ambayo hali hii huweza kuwatokea wagonjwa wa moyo ulioferi Ini na figo
Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Amikacin
Gentamicin
Lofexidine
Neomycin
Paromomycin
Squill
Streptomycin
Tobramycin
Matumizi ya Bumetanide
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye mzio na dawa hii na mgonjwa mwenye shida ya kukojoa pamoja na watoto chini ya siku 28
Tahadhari kwa dawa hii:
Huweza kupelekea hatari ya kupoteza elekrolaiti kwenye mwili na yapo madhara mengi ya kupoteza elekrolaiti kama Haipaglaisemia , haipotensheni, haipokalemia, haiponatremia na kuishiwa maji.
Endapo itatumika kwa mgonjwa mwenye shida ya kukojoa anapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na ;
Upungufu wa madini ya Potasiamu
Upungufu wa madini ya Sodiamu
Sukari kuwa nyingi mwilini
Kuongeza kwa wingi wa creatinine kwenye damu
Kizunguzungu
Misuli kukaza
Sumu kwenye sikio
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dawa anapaswa kutumia pindi anapokumbuka.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:48:09
Rejea za mada hii:-