Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Mei 2020, 15:30:31

Carteolol
Carteolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Ocupress.
Dawa hii huwa mfumo ya maji ambayo hutumika kupunguza presha kwenye macho
Carteolol hupatikana katika mfumo wa maji
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu;
Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Carteolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza presha kwenye macho.
Hufanya kazi ya msingi ya kupunguza shinikizo kwenye macho kwa kupunguza utengenezaji wa maji maji yanayojulikana kama aquasi huma. Kwa kufanya hivi hupunguza presha kwenye macho.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo,
Atenolol (Tenormin)
Betaxolol (Monocor,Zebeta)
Acebutolol (Sectral )
Betaxolol (Kerlone)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor, Toprol-XL)
Nadolol (Corgard)
Nebivolol (Bystolic)
Penbutolol (Levatol)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo;
Hutumika kutibu wagonjwa wenye presha ya jicho
Hutumika kutibu ya glaukoma
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acidophilus
Aricept
Artificial Tears
Aspirin
Benadryl
Diltiazem
Fentanyl Transdermal System
Fiber Lax
Lasix
Milk of Magnesia
Promethazine
Omeprazole
Mirtazapine
Brimonidine
Synthroid
Acetaminophen
Vitamini C
Xalatan
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye asthma
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine za Beta bloka
Tahadhari kwa mama mjamzito.
Hakuna takwimu zinazoonesha kuwa dawa hii inaweza kuathiri maziwa ya mama anayenyonyesha, hata hivyo itumike kwa uangalifu.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni ;
Kuhusi macho kuungua
Kutokwa na mchozi kupita kiasi
Kuhisi mchanga machoni
Kuogopa mwanga
Kutoona usiku vzuri
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-