Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
30 Januari 2024 15:43:16
Clavam
Ni jina la kibiashara la dawa inayojulikana kama amoxiclav, ambayo ni muunganiko wa dawa mbili yaani Amoxicilin na clavulanate potassium. Dawa hii hutumika kutibu maambukizi mbali mbali yanayosababishwa na bacteria.
Uzito wa clavam
Dawa hii hupatikana katika fomu ya vidonge na dawa ya unga ambayo huchanganywa na maji kupata dawa ya maji katika uzito ufuatao
Vidonge
250 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 250 na clavulanate potassium miligramu 125)
500 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 500 na clavulanate potassium miligramu 125)
875 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 875 na clavulanate potassium miligramu 125)
1000 mg/62.5 mg (amoxcilin miligramu 1000 na clavulanate potassium miligramu 125)
200 mg/28.5 mg (amoxcilin miligramu 200 na clavulanate potassium miligramu 28.5)
400 mg/57 mg (amoxcilin miligramu 400 na clavulanate potassium miligramu 57)
Â
Dawa ya maji
(125 mg/31.25 mg)/5 ml- amoxcilin miligramu 125 na clavulanate potassium miligramu 31.25, katika ujazo wa mililita 5
(200 mg/28.5 mg/)5 ml - amoxcilin miligramu 200 na clavulanate potassium miligramu 28.5, katika ujazo wa mililita 5
(250 mg/62.5 mg/)5ml- amoxcilin miligramu 250 na clavulanate potassium miligramu 62.5, katika ujazo wa mililita 5
(400 mg/57 mg/)/5ml- amoxcilin miligramu 400 na clavulanate potassium miligramu 57, katika ujazo wa mililita 5
(600 mg/42.9 mg)/5ml- amoxcilin miligramu 600 na clavulanate potassium miligramu 42.9, katika ujazo wa mililita 5
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Kupata maelezo zaidi kuhusu clavam/amoxiclav soma mada inayohusiana na Amoxiclav
Majina mengine ya kibiashara ya clavam
Yafuatayo ni majina mengine ya kibiashara ambayo humaanisha amoxcilin/clavulanate potassium
Cledomox
Augmentin
Augmentin XR
Augmentin ES-600
Gamok
Â
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Februari 2024 17:47:43
Rejea za mada hii:-