Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Aprili 2020 14:14:09
Darunavir
Darunavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na Hepataitizi C, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaazi inhibita.
Dawa hii haitumiki yenyewe bali huunganishwa pamoja Ritonavir na dawa zingine za kuthibiti makali ya kirusi cha UKIMWI-ART ili kufanya kazi kwa ufanisi kuzuia kuzaliana kwa virusi na kuongeza kwa kinga za mwili.
Dawa inapoingia mwilini, huenda kuzuia kimeng’enya muhimu cha kirusi kinachoitwa proteazi ili kisifanye kazi yake. Kimeng’enya hiki hufanya kazi muhimu ya kukifanya kirusi kikomae, dawa hii inapozuia utendai kazi wa kirusi basi virusi huwa havikomai na kukosa uwezo wa kuambukiza seli zingine za CD4.
Rangi na fomu ya Darunavir
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge na maji, kidonge huwa na uzito wa
75-mg
150-mg
600-mg
800-mg
Au maji yenye uzito wa 100-mg/mL oral
Rangi ya dawa hutegemea kiwanda kilichozalisha
Dawa huweza kutumika pamoja au bila chakula
Dawa zilizo kundi moja na Lopinavir
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Lopinavir/Ritonavir ni zifuatazo :
Amprenavir
Atazanavir
Darunavir
Fosamprenavir
Indinavir
Lopinavir
Nelfinavir
Ritonavir
Saquinavir
Tipranavir
Baadhi ya dozi zenye muunganiko wa dawa ya Darunavir ni kama zifuatazo:
Dolutegravir (DTG)+Darunavir (DRV)+Lamivudine (3TC)
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na Daktari
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Lopinavir
Darunavir haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Alfozosin
Cabergoline
Carbemezapine
Cobimetinib
Ergotamine
Erythromycin
Rifampin
Eliglustat
Irinotecan
Midostaurin
Neratinib
Olaparid
Bosentan
Ceritinib
Cimetinide
Conjugated Estrogen
Copanlisib
Tahadhari ya Lopinavir
Inapaswa kukatishwa endapo vipele na mzio utatokea
Mgonjwa anayetumia dawa hii huweza kuvimba kongosho
Kuwa makini inapotumika kwa wazee
Huongeza kolestro mwilini
Huongeza glukozi mwilini
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Mgonjwa mwenye mzio na dawa hii
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Lopinavir Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii haina madhara kwa mama mjamzito na mtoto
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote japo dawa hii haina madhara kwake mtoto licha ya kuwa huwa inapita kwenye maziwa
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ya Lopinavir ni pamoja na:
Kuharisha
Kichwa kuuma
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Kungogezeka kwa kolestrol mwilini
Kuchoka
Kuvimba kongosho
Je endapo umesahau dozi ya Lopinavir ufanyeje?
Dawa hii hutumika kwa Pamoja na dawa zingine za kuthibiti Virusi vya UKIMWI, endapo utasahau kunywa dozi yako, unapaswa kunywa mara moja. Endapo muda umekaribia sana wa kunywa dozi ingine kunywa mara moja na usinywe dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:46:50
Rejea za mada hii:-