Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Septemba 2021 13:27:42
Dawa Albendazole
Ni dawa ya ya kutibu maambukizi ya minyoo iliyo katika kundi la anthelmintic. Dawa hii hutibu maambukizi ya minyoo kwa binadamu kutoka kwa mbwa na nguruwe na pia hufahamika kwa jina jingine la procaine, Albenza, Eskazole na Albendazolum.
Uzito na fomu ya Albendazole
Albendazole hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa
Milligramu 200
Dawa kundi moja na albendazole
Dawa zingine zilizo kundi la anthelmintic kama Albendazole ni;
Mebendazole
Thiabendazole
Ivermectin
Praziquantel
Diethylcarbamazine
Triclabendazole
Moxidectin
Pyrantel pamoate
Albendazole hutibu nini?
Hutibu maambukizi ya minyoo jamii ya Taenia Solium wanaosababisha
Hutibu maambukizi yanayosababishwa na minyoo jamii ya Echinococcus
Hutibu maambukizi ya minyoo yanayoitwa kapillariasis
Namna Albendazole inavyofanya kazi
Albendazole hufanya kazi ya kuharibu chembe za minyoo katika matumbo yao hivyo kuzifanya zisiweze kuzalisha nishati. Kushindwa zalisha nishati hufanya minyoo isindwe jongea na kutumia glukosi kwa ajili ya kuishi na hivyo hufa.
Vimelea wanaodhuriwa na Albendazole:
Taenia Solium
Echinococcus
Ancylostoma
Trichostrongylus
Enteroblus
Clonorchis Sinensis
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Albendazole
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Albendazole au benzimidazoles
Mambo ya kufahamu kabla ya kutumia albendazole
Mwambie daktari wako kwama una hali au magonjwa yafuatayo kabla ya kutumia dawa hii;
Magonjwa ya macho haswa yale yanayohuaisna na retina
Magonjwa ya ini
Magonjwa ya uboho wa mifupa
Kama unatarajia kubeba ujauzito ndani ya wiki moja ( tumia kondomu au njia za uzazi wa mpango kama upo kwenye siku za hatari maana dawa hii inaweza kuw ana madhara kwa uumbaji wa kijusi)
Utoaji taka za Albendazole mwilini
Chini ya asilimia 1 Albendazole hutolewa kwa njia ya mkojo na kiasi kingine humeng’enywa na ini kuwa albendazole sulfoxide kisha kuingia kwenye mfumo wa nyongo na huaminika kutolewa njia hii kupitia kinyesi.
Matumizi ya Albendazole kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti za kutosha kwa binadamu kuonyesha madhara yake hata hivyo taarifa za wanyama zinaonyesha kuwa na hatari ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa kijusi tumboni.
Matumizi ya Albendazole kwa mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonyesha dawa hii kuwa na madhara kwa mtoto endapo mama atatumia wakati wa kunyonyesha.
Mwingiliano wa Albendazole na dawa zingine
Albendazole ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu na mtaalamu wa afya :
Acalabrutinib
Fosphenytoin
Phenytoin
Dawa zenye mwingiliano mwingiliano mdogo na Albendazole
Dexamethasone
Praziquantel
Maudhi ya Albendazole
Kichwa kuuma
Tumbo kuuma
Kichefuchefu
Kizunguzungu
Homa
Kutokwa na vipele
Maumivu ya kichwa
Shingo kuwa ngumu
Kuongezeka hisia za macho kwenye mwanga
Kuchanganyikiwa
Homa
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Kubadilika kwa vipimo vya kazi za ini
Kizunguzungu
Hisia za vitu kuzunguka
Kupoteza nywele kwa muda
Hiasia cha kuchoka
Degedege
Hisia za maumivu nyuma ya macho
Dalili zinazotakiwa kukufanya uwasiliane na daktari haraka;
Homa
Kutetemeka
Vidonda kooni
Vidonda kinywani
Hisia za kichwa kuwa chepesi
Degedege
Maumivu makali ya kichwa
Masikio kutoa makelele
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Matatizo ya uono na hisia za maumivu nyuma ya macho
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka ,isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea inayofuata kama muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-