Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Septemba 2021 18:56:58
Dawa Alendronate
Alendronate ni moja kati ya dawa jamii ya bisphosphonate inayotumika kukinga na kutibu magonjwa ya mifuta dhaifu (yenye hatari ya kuvunjika haraka).
Majina mengine ya Alendronate
Majina mengine ya Alendronate ni;
Adrovance
Binosto
Fosamax
Fosamax Plus D
Fosavance
Dawa zilizo kundi moja na Alendronate
Dawa zilizo kundi moja na Alendronate ni;
Risedronate
Ibandronate
Etidronate
Pamidronate
Zoledronate
Fomu na uzito wa Alendronate
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Vidonge vyenye uzito wa;
5mg
10mg
35mg
40mg
70mg
Kimiminika cha kunywa chenye uzito wa;
70mg/75mls
Namna Alendronate inavyoweza kufanya kazi
Mara baada ya kuingia kwenye damu Alendronic acid hujishikiza kwenye hydroxyapatite ya mifupa. Ufyonzwaji kalisiamu kwenye mifupa hutengeneza mazingira ya utindikali katika mifupa na kupelekea kuachiwa kwa alendronic acid kutoka kwenye mifupa. Alendronic acid hufyonzwa na chembe osteoclasts kisha kuachiwa kwenye saitosol ya osteoclasts inayofanya kazi ya kufyonza mifupa. Kuzuiwa ufanyaji kazi wa osteoclasts husababisha kupungua kwa ufyonzwaji wa kalisiiamu ndani ya mifupa na hivyo kufanya mifupa iwe imara kutokana na kutopoteza madini hayo.
Alendronate hutibu nini?
Hutumika kutibu na kukinga mifupa dhaifu
Hutumika kutibu mifupa dhaifu iliyoamshwa na dawa jamii ya glucocorticoid
Hutumika kutibu ugonjwa wa Paget
Ufozwaji wa dawa
Mara baada ya kunywa dawa, wastani wa kiini cha dawa kinachoingia kwenye damu kwa mwanamke ni asilimia 0.64 tu na kwa wanaume ni asilimia 0.59. Kiini cha dawa kinachoingia kwenye damu hupungua mpaka asilima 40 kama ikitumika ndani ya saa moja baada ya kula.
Mwingiliano wa Alendronate na chakula
Ufyonzwaji wa dawa hupungua kama itatumika ndani ya saa moja kabla au baada ya kula. Unapaswa kunywa masaa mawili kabla ya kula au kusubiria masaa mawili baada ya kula.
Utoaji taka wa Alendronate mwilini
Asilimia hamsini (50%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo ndani ya msaa 72. Hakuna kiasi cha dawa kinachopatikana kwenye kinyesi. Wanaume hutoa kiwango kidogo cha dawa kwenye mkojo ukilinganisha na wanaume.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Alendronate
Wagonjwa wenye mzio wa Alendronate
Wagonjwa ambao calcium ipo chini (Haipokalsemia)
Dawa zenye muingiliano na Alendronate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Alendronate;
Tafiti zinaonesha hakuna dawa yenye muingiliano mkali na Alendronate.
Dawa zinazoweza kutumika na Alendronate chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Deferasirox
Magnesium
Nizatidine
Selenium
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Sucroferric oxyhydroxide
Trimagnesium citrate anhydrous
Voclosporin
Zinc
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Alendronate;
Aceclofenac
Acemetacin
Aspirin
Aspirin rectal
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Celecoxib
Choline magnesium trisalicylate
Diclofenac
Diflunisal
Entecavir
Etodolac
Famotidine
Fenoprofen
Flurbiprofen
Foscarnet
Ibuprofen
Ibuprofen iv
Ibuprofen/famotidine
Indomethacin
Ketoprofen
Ketorolac
Ketorolac a kuweka puani
Levothyroxine
Lornoxicam
Meclofenamate
Mefenamic acid
Meloxicam
Nabumetone
Naproxen
Oxaprozin
Parecoxib
Piroxicam
Salicylates (non-asa)
Salsalate
Sulfasalazine
Sulindac
Teriparatide
Tolfenamic acid
Tolmetin
Matumizi ya Alendronate kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii ina madhara kwa mama na mtoto aliyeko tumboni hivyo haitakiwi kutumika wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Alendronate mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo tahadhari inatakiwa ichukuliwe wakati wa kutumia dawa hii.
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi kwa wakati sahihi tumia pale utapokumbuka asubuhi inayofuata kisha endelea na dozi yako ya wiki kama ulivyopangiwa kwa siku za wiki. Usitumie dozi mbili kufidia ile uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:56:16
Rejea za mada hii:-