Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
14 Septemba 2021, 11:45:47

Dawa Artesunate
Artesunate ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu malaria kali, inayofahamika kwa jina jingine la Camequin
Uzito na fomu ya Artesunate
Hupatikana katika fomu ya unga wenye uzito wa milligramu 110 kwa chupa moja. Unga huu huchanganywa na maji na kutumika kwa kuchoma na sindano.
Artesunate hutibu nini?
Dawa hii imehifadhiwa kutumika kwa matibabu ya awali ya malaria kali na baada ya hapo hufuatia na dawa jamii nyingine za kumeza.
Vimelea wanaodhuriwa na artesunate
Plasmodium vivax
Plasmodium ovale
Namna Artesunate inavyofanya kazi
Dawa jamii ya Artemisinin ikiwa pamoja na artesunate humeng’enywa haraka na ini kutengeneza dihydroartemisinin (DHA)
Artesunate na DHA, kama ilivyo artemisinin zingine, huwa na kimeng’enya cha endoperoxide kinachoamshwa na madini chuma ili kuwa sumu ya oksijeni inayofanya kazi ya kuzuia uzalishaji wa protini na nucleic acid, kubadilisha umbile na kupunguza kasi ya ukuaji wa kimela na kuua
Artesunate na DHA hufanya kazi kwenye kimelea Plasmodium species kikiwa kwenye damu na fomu ya gametocytes, hufanya kazi pia kwenye kimelea hiki hata kama ni sugu kwenye chloroquine
Tahadhari kwa watumiaji wa artesunate
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii. Artesunate itapswa kusimamishwa mara moja endapo kuna dalili ya;
Kushuka kwa shinikizo la damu
Kiungulia
Kuvimba kwa mwili
Harara kwenye ngozi
Matumizi ya Artesunate na chakula
Dawa hii haijaripotiwa kuwa na mwingiliano na chakula
Nusu maisha ya dawa na utolewaji taka mwilini
Nusu maisha ya dawa ni masaa 0.3 hr kwa artesunate na masaa 1.3 kwa DHA 1.3. Haifahamiki mpaka sasa namna gani artesunate inavyotolewa mwilini.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Artesunate
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Artesunate
Wagonjwa waliofahamika kuwa na mzio wa anafailaksia kwenye dawa zingine
Dawa zenye mwingiliano na Artesunate
Dawa zenye mwingiliano mkali za kuzuia dawa hii kutumika pamoja na dawa zingine
Dapsone ya kupaka
Sotorasib
Tepotinib
Artesunate ikitumika na dawa hizi mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu;
Axitinib
Berotralstat
Carbamazepine
Deferasirox
Diclofenac
Diflunisal
Eltrombopag
Imatinib
Methylene blue
Nevirapine
Phenobarbital
Phenytoin
Regorafenib
Rifampin
Ritonavir
Sorafenib
Tucatinib
Vandetanib
Matumizi ya Artesunate kwa mama mjamzito
Taarifa za matokeo ya matumizi ya artesunate wakati wa ujauzito ni machache kuweza kusemea madhara yake wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Artesunate kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii hupatikana kwenye maziwa ya mama licha ya kutokuwepo na tafiti zinazoonyesha madhara yake kwa kichanga anayenyonya maziwa.
Maudhi ya Artesunate
Kuishiwa chembe nyekundu za damu
Kupunguza chembe sahani za damu
Kuwa na wingi wa bilirubin
Upungufu wa damu
Ongezeko la vimeng’enye vya ini (transaminase)
Upungufu wa che,be sahani za damu
Ongezeko la bilirubini kwenye damu
Leukosatosis
Kuferi ghafla kwa figo kiasi cha kuhitaji dayalisis
Dalili kali ua kupumua kwa shida
Limfopenia
Hemoglobinuria
Neutropenia
Kuganda wa damu kwenye mishipa ya vena ya ndani
Ongezeko la creatinine
Nimonia
Mapafu kuvia maji
Kuharisha
Manjano
Madhaifu ya mfumo wa fahamu
Je endapo umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka. Isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea inayofuata kama muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-