Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Septemba 2021 16:48:57
Dawa Aztreonam
Aztreonam ni moja kati ya antibiotic jamii ya Monobactam inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria gram hasi kama vile pseudomonas aeruginosa.
Aztreonam hufahamika kwa jina jingine la Azactam
Majina mengine ya Aztreonam
Aztreonam hufahamika pia kama azactam
Fomu na uzito wa dawa ya Aztreonam
Dawa hii ipo katika fomu ya unga (powder) kwa ajiri ya sindano na maji kwa ajiri ya kuvuta kwa pumzi
Uzito wa dawa ya Aztreonam
Aztreonam ina uzito ufuatao;
Unga (powder) kwa ajiri ya sindano
1gram
2gram
Maji ya kuvuta kwa pumzi
75mg
Aztreonam hutibu nini?
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Hutumika kutibu maambukizi kwenye vidonda
Hutumika kutibu uvimbe kwenye via vya uzazi
Maambukizi ya Pseudomonas aeruginosa kwenye mapafu
Namna Aztreonam inavyoweza kufanya kazi
Hufanya kazi ya kuzuia utengenezaji wa ukuta wa chembe hai ya bakteria kwa kujishikiza kwenye protini ya penicillin na pia kuamsha uvunjwaji wa ukuta wa bakteria kwa kimeng'enya cha autolysin
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mishipa na pia inapoingia kwenye mirija ya hewa. CHini ya asilimia 1 ya dawa hufyonzwa kama ikitumika kwa kunywa.
Vimelea wanaodhuriwa na Aztreonam
Escherichia coli
Enterobacter spp
Citrobacter spp
Proteus mirabilis
Serratia marcescens
Haemophilus influenza
Klebsiella pneumonia
Pseudomonas aeroginosa
Mwingiliano wa Aztreonam na chakula
Hakuna taarifa za matumizi ya dawa na na chakula. Wasiliana na daktari wako kwa maelezo zaidi
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Aztreonam
Wagonjwa wenye mzio wa Aztreonam
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya monobactams
Utoaji taka za Aztreonam mwilini
Asilimia 60 hadi 70 ya dawa hutolewa kama ilivyo kwa njia ya mkojo na asilimi 13 hadi 15 kwa njia ya kinyesi. Kiasi kilichobaki hutolewa katika fomu nyingine baada ya kufanyiwa umetaboli na ini
Matumizi ya Aztreonam kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Aztreonam kwa mama mjamzito
Tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa kwa mama mjamzito kwani dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto.
Matumizi ya Aztreonam kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inatolewa mwilini kwa njia ya maziwa hivyo haishauriwi kwa mama anayenyonyesha.
Dawa zenye muingiliano na Aztreonam
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Aztreonam;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya Kipindupindu
Chanjo hai ya Typhoid
Dawa zinazoweza kutumika na Aztreonam chini ya uangalizi;
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Conjugated estrogens
Digoxin
Estradiol
Estrogens conjugated synthetic
Estropipate
Mestranol
Metoclopramide ya kuweka puani
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Aztreonam;
Amikacin
Amoxicillin
Balsalazide
Biotin
Cefadroxil
Cefamandole
Cefpirome
Chloramphenicol
Dicloxacillin
Flucloxacillin
Gentamicin
Neomycin po
Pantothenic acid
Paromomycin
Pivmecillinam
Probenecid
Pyridoxine
Pyridoxine (kizimua sumu)
Streptomycin
Temocillin
Thiamine
Ticarcillin
Tobramycin
Maudhi ya Aztreonam
Kizunguzungu
Kikohozi
Maumivu ya koo
Kuharisha
Homa
Kichefuchefu
Kutapika
Uso kuvimba
Maumivu ya tumbo
Kichwa kuuma
Kuchanganyikiwa
Kifua kubana
Kupata vipele
Kuvimba kwa maungio ya mwili
Manjano
Kupungukiwa damu
Ufanye nini kama umeshau dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumiamara pale utakapokumbuka, isipokuwa kama muda umeenda sana, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-