Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
17 Septemba 2021, 10:31:54
Dawa Bedaquiline
Bedaquiline ni moja kati ya antibiotic jamii ya Antitubakula inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria mycobacteria tuberculae anayesababisha kifua kikuu (TB). Bedaquiline imehifadhiwa kutumika kwa wagonjwa wa kifua kikuu kinachosababishwa na bakteria wenye usugu kwenye dawa zingine za TB.
Majina mengine ya Bedaquiline
Majina mengine ya Bedaquiline ni;
Sirturo
Fomu na uzito wa Bedaquiline
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;
20mg
100mg
Dawa zilizo kundi moja na Bedaquiline
Dawa zilizo kundi moja na Bedaquiline ni;
Isoniazid
Rifampicin
Pyrazinamide
Ethambutol
Namna Bedaquiline inavyoweza kufanya kazi
Bedaquiline ni dawa jamii ya diarylquinoline, antitubakula inayofanya kazi kwa kuzuia ufanyaji kazi wa imeng’enya adenosine 5'-triphosphate synthase, kinachofanya kazi muhimu ya kutengeneza nishati kwa ajili ya bakteria Mycobacterium tuberculosis. Kitendo hiki hupelekea kufa kwa bakteria kutokana na kukosa nishati.
Vimelea wanaodhuriwa na Bedaquiline
Mycobacteria tuberculae
Bedaquiline hutibu nini?
Hutumika kutibu kifua kikuu (TB) kutokana na maambukizi ya Mycobacteria tuberculae.
Ufozwaji wa dawa na mwingiliano wake na chakula
Bedaquiline hufozwaji vema mara baada ya ikiingia kwenye mfumo wa chakula. Chakula husaidia ufozwaji wa dawa. Dawa hufikia kileleni kwenye damu masaa 5 baada ya kunywa dawa na hakuna mwingiliano ulioripotiwa kutokea endapo kitatumika na dawa hii.
Utoaji taka za Bedaquiline mwilini
Bedaquiline hutolewa kwa zaidi ya asilimia 99.9 kwa njia ya kinyesi, chini ya asilimia 0.001 hutolewa kwenye mkojo.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Bedaquiline
Wagonjwa wenye mzuio wa Bedaquiline.
Wagonjwa wenye mzuio wa dawa jamii ya antitubakula
Dawa zenye muingiliano na Bedaquiline
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Bedaquiline;
Abametapir
Amobarbital
Apalutamide
Aripiprazole
Artemether
Atazanavir
Chanjo hai ya bcg
Bosentan
Carbamazepine
Chloramphenicol
Chloroquine
Clarithromycin
Dexamethasone
Efavirenz
Fosamprenavir
Fosphenytoin
Glasdegib
Idelalisib
Imatinib
Indinavir
Inotuzumab
Isoniazid
Itraconazole
Ivosidenib
Ketoconazole
Lonafarnib
Lopinavir
Lorlatinib
Macimorelin
Nafcillin
Nefazodone
Nelfinavir
Nevirapine
Nicardipine
Oxcarbazepine
Panobinostat
Pentobarbital
Phenobarbital
Phenytoin
Ponesimod
Posaconazole
Primidone
Quinidine
Ribociclib
Rifampin
Voriconazole
Voxelotor
Dawa zinazoweza kutumika na Bedaquiline chini ya uangalizi;
Artemether/lumefantrine
Azithromycin
Chlorpromazine
Ciprofloxacin
Clarithromycin
Erythromycin
Fluconazole
Haloperidol
Levofloxacin
Lumefantrine
Methadone
Mifepristone
Moxifloxacin
Ofloxacin
Paliperidone
Pasireotide
Pazopanib
Pentamidine
Perphenazine
Pimozide
Posaconazole
Procainamide
Propafenone
Protriptyline
Quetiapine
Quinidine
Quinine
Ranolazine
Risperidone
Romidepsin
Rucaparib
Saquinavir
Selpercatinib
Sertraline
Solifenacin
Trimipramine
Triptorelin
Vandetanib
Vardenafil
Vemurafenib
Voclosporin
Voriconazole
Vorinostat
Ziprasidon
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Bedaquiline;
Tafiti zinaonesha kuwa hakuna dawa yenye mwingiliano mdogo na Bedaquiline.
Matumizi ya Bedaquiline kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Bedaquiline kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto. Hivyo haishauriwi kutumia dawa hii wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Bedaquiline mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa.Hivyo hairuhusiwi kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Bedaquiline;
Kukosa hamu ya kula
Kukanganyikiwa
Maumivu ya kichwa
Harara kwenye ngozi
Maumivu ya maungio ya mwili
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Kutapika
Kuchoka
Muwasho mkali wa mwili
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako kwa wiki mbili za mwanzo za matibabu usitumie dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda sahihi. Kama umesahau dozi kuanzia wiki tatu za matibabu na kuendelea tumia mara pale utakapokumbuka kisha endelea na dozi inayofata kama ulivyopangiwa na daktari.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:56:16
Rejea za mada hii:-