Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Septemba 2021, 15:01:54
Dawa Cefepime
Cefepime ni antibiotiki ya kizazi cha nne cha cephalosporin inayotumika katika matibabu ya magonjwa yanayosababiswha na maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaodhuriwa na dawa hii kwenye mapafu, mfumo wa mkojo, via vya uzazi, nogzi n.k.
Cefepime hudhuru bakteria wa gramu hasi na chanya na huwa na uwezo zaidi kuliko dawa za kizazi cha tatu na zilizo kwenye kundi moja nayo, hii ndio maana imehifadhiwa kwa ajili ya maambukizi makali nay ale yenye usugu kwenye dawa zingine.
Majina mengine ya Cefepime
Majina mengine ya Cefepime ni;
Maxipime
Dawa zilizo kundi moja na Cefepime
Dawa zilizo kundi moja na Cefepime ni ;
Cefazola
Cefaclor
Cefdinir
Cefuroxime
Cefadroxil
Cephalexin
Ceftriaxone
Fomu na uzito wa Cefepime
Dawa hii ipo katika fomu ya unga kwa ajiri ya sindano wenye uzito wa 1g na 2g
Cefepime pia hupatikana katika fomu ya infusheni yeney uzito wa;
1g/50mL
2g/100mL
Namna Cefepime inavyofanya kazi
Dawa jamii ya cephalosporins hufanya kazi kwa kuua bakteria na pia hufanya kazi zake kama dawa zingine za beta-lactam ( mfano penicillin). Cephalosporins huharibu utengenezaji wa peptidoglycan ukuta maalumu wa seli ya bakteria. Ukuta wa peptidoglycan huwa moja ya muhumiri kwenye ukuta wa seli ya bakteria haswa kwa bakteria gramu chanya. Hatua ya mwisho ya kutengeneza muhimiri huu huwezeshwa na kimeng’enya cha transpeptidases kinachofanya kazi kwa kuzijishika kwenye mlango penicillin.
Vimelea wanaodhuriwa na Cefepime
Bacteroides spp
Enterobacter spp
Escherichia coli
Haemophilus influenzae
Klebsiella spp
Proteus mirabilis
Pseudomonas spp
Staphylococcus aureus
Streptococcus pyogenes
Cefepime hutibu nini?
Cefepime hutibu magonjwa yanayotokana na maambukizi ya vimelea vinavyodhuriwa na dawa hii na hivyo;
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Hutumika kutibu maambukizi kwenye ngozi
Hutumika kutibu Nimonia
Hutumika kutibu maambukizi ndani ya tumbo
Hutibu neutropenia ya homa
Ufyonzwaji na utoaji taka Cefepime nje ya mwilini
Asilimia 82 ya dawa hufyonzwa na kufanya kazi kama itachomwa kwenye misuli na nusu maisha ya dawa ni masaa 2 na mara dawa inapoingia kwenye damu na kufanya kazi, asilimia themanini na tano (85%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiasi kilichobaki hufanyiwa umetaboli kwenye ini na kutolewa katika fomu nyingine. Dawa hii pia huweza kuingia kwenye maziwa ya mama.
Mwingiliano wa Cefepime na chakula
Dawa hii inaweza kutumika na chakula au pasipo chakula
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefepime
Wagonjwa wenye mzio wa Cefepime na dawa jamii ya cephalosporins.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Penicillin.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya beta lactam.
Dawa zenye muingiliano na Cefepime
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na cefepime;
Chanjo hai ya BCG
Chano ya kipindupindu
Chanjo hai ya typhoid
Dawa zinazoweza kutumika na Cefepime chini ya uangalizi;
Amifampridine
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Dienogest/estradiol valerate
Estradiol
Ethinylestradiol
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Probenecid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Cefepime;
Aminohippurate sodium
Aspirin
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Choline magnesium trisalicylate
Furosemide
Rose hips
Sulfasalazine
Tolmetin
Willow bark
Matumizi ya Cefepime kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha
Matumizi ya Cefepime kwa mama mjamzito
Tafiti zilizofanyika hazijaonesha madhara kwa mtoto aliyepo tumboni kwa mama.
Matumizi ya Cefepime mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha kuwa Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama kwa kiwango kidogo lakini hakuna tafiti zinazoonesha madhara kwa mtoto na katika uzalishaji wa maziwa.
Maudhi ya cefepime
Kipimo chanya cha Coombs bila kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu
Harara
Ongezeko la vimeng’enya vya ini
Kushuka kwa kiwango cha phosphate kwenye damu
Kuharisha
Eosinofiilia
Kuvia damu sindano ilipochomwa
Maumivu sehemu sindano ilipochomwa
Kichefuchefu na kutapila
Homa
Maumivu ya kichwa
Muwasho
Agranulosaitosis
Mzio wa anafailaktiki
Anafailaksia
Koma
Anaphylaxis
Encephalopath
Kusikia sauti zisizokuwepo
Leukopenia
Kukakamaa kwa maungio ya mwili
Kuharibika kwa umeme wa misuli
Neutropenia
Degedege
Upugufu wa chembe sahani za damu
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu kutumia dozi kwa wakati sahihi.Kama umesahau kutumia dozi yako muulize daktari au mfamasia wako muda sahihi wa kupata dozi nyingine.Usitumia dozi mbili kwa wakati mmoja ili kufidia dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-