Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
3 Novemba 2021, 10:33:54
Dawa cefexime
Cefixime ni antibayotiki kizazi cha tatu cha cephalosporin. Hutumika kutibu maradhi mbalimbali kutokana na bakteria jamii ya gramu chanya na hasi.
Majina ya kibiashara
Cefixime hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kama;
Suprax
Fomu na uzito cefixime
Namna cefixime inavyofanya kazi
Cefixime hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa vijenzi muhimu vya bakteria na hivyo kufanya wasijizalie na kufa. Vijenzi hivyo huwa na jina la mucopeptid, huwa muhimu katika ukuta wa nje ya bakteria. Cefixime huwezesha kazi hiyo kwa kuzuia utengenezaji wa vijenzi hivyo katika hatua ya kwanza na mwisho.
Vimelea wanaodhuriwa na cefixime
Vimelea wanaodhuriwa na dawa cefixime ni;
Staphylococcus aureus
Streptococcus pneumonia
Streptococcus pyogenes
Hemophilus influenza
Moraxella catarrhalis
E. coli, Klebsiella
Proteus mirabilis
Salmonella
Shigella
Neisseria gonorrhoeae
Cefixime inatibu nini?
Cefixime hutibu magonjwa yanayosababiswha na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.
Baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na Cefixime ambapo inapaswa kutumika yenyewe au ikiwa imechanganyika na dawa zingine ni;
Bronkaitiz
Gono
Otitis
Pharyngitis
Tonses
U.T.I
Ufyonzwaji wa cefixime
Asilimia 40-5o ya dawa hufyonzwa kwenye utumbo na kuingia kwneye damu
Cefixime na chakula
Ufyonzwaji wa cefixime hauzuiliwi na chakula, hufyonzwa vema ikitumika na au pasipo chakula. Hata hivyo huchukua masaa 0.8 zaidi kufyonzwa kwa kiwango hiko kama ikitumika na chakula.
Umetaboli wa cefixime
Asilimia 50ya dawa iliyofyonzwa tumboni na kuingia kwenye damu hutolewa bila kufnayiwa umetaboli kupitia mkojo ndani ya masaa 24.
Nusu maisha ya cefixime
Nusu maisha ya cefixime kwenye damu ni masaa 3 hadi 4 ( ingawa yanaweza kwenda hadi 9). Kama utendaji kazi wa figo ni mdogo kiasi cha 5 hadi 20 mililita kwa dakika, nusu maisha yake huongezeka kwa wastani wa masaa 11.5.
Matumizi ya cefixime na dawa zingine
Dawa zenye mwingiliano mkali kiasi cha kutopaswa kutumika pamoja;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya kipindupindu
Chanjo hai ya taifodi
Cefixime ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anabidi kuwa kwenye uangalizi wa karibu wa mtaalamu wa afya;
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Dienogest/estradiol valerate
Estradiol
Ethinylestradiol
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Probenecid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Voclosporin
Warfarin
Dawa zenye muingiliano mdogo sana na cefixime
Aminohippurate sodium
Aspirin
Aspirin rectal
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Bendroflumethiazide
Chloramphenicol
Choline magnesium trisalicylate
Cyclopenthiazide
Furosemide
Meloxicam
Rose hips
Willow bark
Dalili za kuzidisha dozi ya cefixime
Madhara ya kuzidisha dozi ya cefixime huonekana na dalili za;
Damu kwenye mkojo
Kuharisha
Kichefuchefu
Maumivu juu ya kitovu
Kutapika
Cefixime kwa mjamzito
Taarifa zilizopo na zamani sana kuhusu matumizi ya cefixime kwenye ujauzito hazijaweza kugundua madhara ya cefixime kwa kijusi tumboni, kujifungua mtoto kwenye ulemavu, mimba kutoka au madhara makubwa katika ujauzito.
Cefixime kipindi cha kunyonyesha
Hakuna taarifa kuhusu uwepo wa dawa hii kwenye maziwa ya mama, madhara yake kwa kichanga anayenyonya na kama ina madhara katika uzalishaji wa maziwa.
Maudhi ya cefixime
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Tumbo kujaa gesi
Kiungulia
Kichefuchefu
Kutapika
Madhara ya cefixime
Unapaswa kuwasiliana na daktari mara moja kama una dalili zifuatazo baada ya kutumia cefixime;
Kupata kinyesi laini chenye damu
Maumivu makali ya kunyonga kwa tumbo
Homa
Harara kwenye ngozi
Kuwashwa
Kuvimba ngozi
Kushindwa pumua vema au kumeza kutokana na kuvimba ndani ya kinywa
Miruzi wakati wa kupumua
Kuvimba uso, koo, ulimi, midomo na macho
Hisia za kurejea kwa maumivu ya koo, homa na dalili zingine za mabambukizi
Yaliyooroshedhwa hapo juu ni madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa watumiaji wa cefixime.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:07:17
Rejea za mada hii:-