Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
14 Septemba 2021, 09:14:14

Dawa Cefpodoxime
Cefpodoxime ni antibiotiki ya kizazi cha tatu cha cephalosporin inayotumika kutibu magonjwa yatokanayo na bakteria wa gram hasi na gram chanya.
Majina mengine ya Cefpodoxime
Majina mengine ya Cefpodoxime ni vantin
Dawa zilizo kundi moja na Cefpodoxime
Dawa zilizo kundi moja na cefpodoxime ni ;
Ceftriaxone
Cefixime
Ceftibuten
Ceftazidime
Cefotaxime
Fomu na uzito wa cefpodoxime
Cefpodoxime hupatikana katika fomu ya;
Suspesheni
Vidonge
Suspesheni huwa na uzito wa;
50mg/5mls
100mg/5mls
Vidonge huwa na uzito wa;
100mg
200mg
Cefpodoxime hutibu nini?
Cefpodoxime hutibu magonjwa yanayotokana na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii mfano;
Hutibu maambukizi katika mfumo wa mkojo
Hutibu Nimonia
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye ngozi
Hutibu maambukizi kwenye koo
Hutibu maambukizi kwenye mfumo wa hewa
Hutumika kutibu kaswende
Hutumika kutibu sepsisi na septikemia
Vimelea wanaodhuriwa na Cefpodoxime
Bacteroides fragilis
Staphylococcus spp
Streptococcus spp
Clostridium perfringens
Morexella catarrtialis
Escherichia coli
Haemophilus spp
Klebsiella spp.
Neisseria spp
Proteus spp
Namna Cefpodoxime inavyofanya kazi
Cefpodoxime hufanya kazi ya kuzuia utengenezaji wa kuta za seli ya bakteria kwa kufunga milango inayotumiwa na penicillin. Hii hupelekea kutokamilika utengenezaji wa bakteria na kuyeyuka kwa bakteria kuyeyuka kwa kumeng’enywa.
Mwingiliano wa Cefpodoxime na chakula
Dawa hii inatakiwa kutumika pamoja na chakula kwani chakula husaidia kuongeza ufozwaji wa dawa.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefpodoxime
Wagonjwa wenye mzio wa hii na dawa nyingine jamii ya Cephalosporin
Wagonjwa wenye mzio wa Penicillin
Utoaji taka wa Cefpodoxime mwilini
Asilimia 80 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo ndani ya masaa 24.
Dawa zenye muingiliano na Cefpodoxime
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Cefpodoxime;
Argatroban
Bivalirudin
Chanjo hai ya BCG
Chanjo ya kipindupindu
Dalteparin
Enoxaparin
Fondaparinux
Heparin
Warfarin
Dawa zinazoweza kutumika na Cefpodoxime chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Azithromycin
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Calcium carbonate
Cimetidine
Clarithromycin
Demeclocycline
Didanosine
Dienogest/estradiol valerate
Digoxin
Doxycycline
Erythromycin base
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Esomeprazole
Famotidine
Ibuprofen/famotidine
Minocycline
Nizatidine
Omeprazole
Probenecid
Rabeprazole
Sodium bicarbonate
Tetracycline
Warfarin
Dawa zenye muingiliano mdogo na cefpodoxime;
Ceftibuten
Choline magnesium trisalicylate
Furosemide
Rose hips
Willow bark
Matumizi ya Cefpodoxime kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Cefpodoxime kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha dawa hii inaweza kutumiwa na mama mjamzito na isilete madhara kwa mtoto.
Matumizi ya Cefpodoxime kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inatolewa njee kupitia maziwa ya mama hivyo haishauriwi kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Cefpodoxime;
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kupata maambukizi ya vimelea ukeni
Homa
Kutapika
Kuwasha mwilini na kupata vipele
Kichefuchefu
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-