Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
1 Juni 2022, 17:29:09

Dawa cefuroxime
Ni antibayotiki ya kizazi cha pili cha cephalosporine inayotumika katika matibabu ya maradhi mbalimbali yanayosababishwa na bakteria. Dawa hii huwa na uwezo wa kutibu mafua, homa ya baridi na maambukizi mengine ya virusi.
Majina mengine ya Cefuroxime
Cefuroxime huwa na majina mengine ambayo ni:
Zinacef
Ceftin
Cefzil
Uzito na fomu ya Cefuroxime
Cefuroxime hupatikana katika fomu ya kidonge, unga na kimiminika.
Kimiminika kwa ajili ya kunywa huwa na uzito ufuatao:
125mg/5mL
250mg/5mL
Unga kwa ajili ya kuchoma sindano huwa na uzito ufuatao:
750mg
1.5g
7.5g
75g
225g
Kidonge huwa na uzito ufuaao:
250mg
500mg
Dawa kundi moja na Cefuroxime
Dawa zingine zilizo kundi moja na cefuroxime yaani kizazi cha pili cha cephalosporin ni:
cefaclor
cefotetan
cefoxitin
cefprozil
Vimelea wanaodhuriwa na Cefuroxime
Vimelea wanaouliwa na cefuroxime ni pamoja na:
Borrelia burgdorferi
Escherichia coli
Haemophilus influenza
Spishi za Klebsiella
Moraxella catarrhalis
Neisseria gonorrhoeae
Proteus mirabilis
Streptococcus pneumonia
Streptococcus pyogenes
Cefuroxime hutibu nini?:
Cefuroxime hutibu magonjwa yafuatayo yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii:
Maambukizi kwenye tonses na koo
Maambukizi kwenye sainazi za mfupa maxilla
Bronkaitizi sugu iliyokali hivi sasa
Nimonia isiyo kali
Maambukizi yasiyo makali kwenye ngozi
UTI isiyo sugu
Kisonono (gono)
Ugonjwa wa lyme kwenye hatua za awali
Maambukizi makali
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Maambukizi ya bakteria kwenye sikio
Namna Cefuroxime inavyoweza kufanya kazi
Cefuroxime hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa kuta ya nje ya bakteria na hivyo kusababisha kuta hiyo kufa na hatimaye bakteria hufa pia.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefuroxime
Cefuroxime haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa pia kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye majibu mabaya ya INR
Wanaougua ugonjwa wa kolaitiz
Wenye mzio wa penicillin
Wenye historia ya degedege
Ufyonzwaji wa Cefuroxime
Asilimia 37 tu ya dawa hufyonzwa endapo itatumika pasipo chakula, asilimia 52 hufyonzwa endapo itatumika baada ya kula chakula. Mara baada ya kunywa, dawa hufikia kileleni kwenye damu baada ya masaa 2 hadi 3.
Umetaboli
Dawa hii hufanyiwa umetaboli kwenye ini na asilimia 66 hadi 100 ya dawa hutolewa kwenye mkojo ikiwa haijafanyiwa umetaboli.
Matumizi ya Cefuroxime kwa mama mjamzito
Taarifa za tafitizilizopo hazijaweza kuonyesha madhara kwa vichanga waliozaliwa na wamama wajawazito waliotumia dawa hii wakati wa ujauzitotafiti. Soma zaidi kuhusu usalama wa dawa hii katika makala ya Cefuroxime na ujauzito
Matumizi ya Cefuroxime kwa mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti za kutosha kuonyesha madhara ya dawa hii kwa mtoto wa mama anayetumia dawa hii. Matumizi ya dawa yanapaswa kuzingatia faida na madhara yanayoweza kujitokeza.
Dawa zenye mwingiliano mkali na Cefuroxime
Dawa zifuatazo huw ana mwingiliano mkali na cefuroxime kiasi cha kutopaswa tumika pamoja:
Argatroban
Bivalirudin
Chanjo hai ya BCG
Chanjo ya kipindupindu
Dalteparin
Enoxaparin
Fondaparinux
Heparin
Dawa zinazohitaji uchunguzi wa karibu kama zikitumika na cefuroxime
Cefuroxime ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anapaswa kuwa chini ya uchunguzi wa karibu wa mtaaalamu wa afya
Aluminum hydroxide
Azithromycin
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Calcium carbonate
Cimetidine
Clarithromycin
Demeclocycline
Didanosine
Dienogest/estradiol valerate
Doxycycline
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Esomeprazole
Ethinylestradiol
Famotidine
Ibuprofen/famotidine
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Minocycline
Nizatidine
Omeprazole
Probenecid
Rabeprazole
Sodium bicarbonate
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Sodium zirconium cyclosilicate
Tetracycline
Voclosporin
Warfarin
Dawa zenye mwingiliano mdogo na cefuroxime
Chloramphenicol
Choline magnesium trisalicylate
Furosemide
Vitu vingine vyenye mwingiliano na Cefuroxime
Cefuroxime pia inaweza kuingiliana na pombe, sigara na baadhi ya vyakula. Ongea na daktari wako kuhusu matumizi ya dawa hii na vitu vingine kama yanafaa.
Maudhi madogo ya Cefuroxime
Maudhi ya mara kwa mara
Homa
Kuhara
Kutetemeka
Hisia za kuumwa
Maumivu ya kichwa
Kuwashwa maeneo ya uke
Maumivu wakati wa kushiriki ngono
Kukakamaa kwa misuli
Kutokwa jasho
Kutokwa na uchafu mzito usio au ulio na harufu ukeni
Maudhi yanayotokea mara chache
Kinyesi cheusi kinachonata
Maumivu ya kifua
Kikohozi
Kinyesi laini
Kuishiwa pumzi
Vidonda kooni
Maumivu wakati w akukojoa
Vidonda kwenye midomo au kinywani
Kuvimba kwa tezi
Kutokwa na damu pasipo sababu
Uchovu mkali usio wa kawaida
Kuvia damu chini ya ngozi pasipo sababu
Maudhi yanayotokea kwa nadra sana
Maumivu ya tumbo, mgongo na miguu
Maumivu ya kibofu
Fizi kutoa damu
Maumivu ya mwili
Hisia za kuungua wakati wa kukojoa
Mkojo uliopauka
Mkojo wenye damu au wenye mawingu
Kushindwa kupumua
Kukosa hamu ya kula
Mapigo ya moyo kwenda kasi na vibaya
Kukojoa mara kwa mara
Kupoteza sauti
Kuja mafua
Kuvimba mwili
Maumivu chini ya mgongo
Kupauka kwa ngozi
Kutokwa damu puani
Kichefuchefu na kutapika
Mkojo kuw ana rangi ya pinki
Kupiga chafya
Kutokwa na mafua
Kuvimba kwa tezi
Kifua kubana
Kuvimba kwa maungio ya mwili
Kutokwa na uchafu mweupe ukeni
Kutoka uchafu wa kahawia ukeni
Kupata mabaka kwenye kinywa na ulimi
Macho kuwa ya njano
Je endapo utasahau dozi ya cefuroxime ufanyaje ?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa kunyw adozi nyingine umefika ambapo utapaswa kusubilia muda ufike ndipo utumie dozi hiyo na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.
Uhifadhi ya Cefuroxime
Hifadhi dawa yako kwenye kikopo cha kutunzia dawa kilichokuja na dawa na katika joto la mazingira. Usiweke kwenye friji au sehemu yenye mwanga wa jua au joto ili kuepuka kuiharibu dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Juni 2022, 18:20:36
Rejea za mada hii:-