top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Sospeter M, MD

Dkt. Lugonda B, MD

6 Februari 2026, 08:01:03

Dawa Chloramphenicol

Dawa Chloramphenicol

Chloramphenicol ni moja kati ya antibiotikiya kutengenezwa aina ya amphenicol inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria kwa baadhi ya bakteria waliokuwa sugu kwenye antibiotiki zingine.


Hata hivyo, matumizi yake yanahitaji uangalizi wa karibu wa kitabibu kutokana na hatari ya madhara makubwa na usugu wa vimelea.


Majina mengine ya chloramphenicol ni;

  • Chloromycetin

  • Econochlor

  • Ocu-chlor


Dawa zilizo kundi moja na Chloramphenicol

Dawa zilizo kundi moja na chloramphenicol ni ;
  • Benzathine penicillin

  • Procaine penicillin

  • Penicillin G

  • Penicillin V


Fomu ya dawa yana uzito wa chloramphenicol


Dawa hii ipo katika fomu ya;
  • Suspension

  • Kidonge

  • Unga kutumika kwa kuchoma

  • Maji kutumika kama matone


Vimelea wanaodhuriwa na chloramphenicol

  • Staphylococcus aureus

  • Streptococcus pneumoniae .

  • Escherichia coli

  • Haemophilus influenza

  • Neisseria meningitis

  • Salmonella typhi (kwa sasa anausugu kwenye dawa hivyo dawa hii si chaguo la kwanza)


Namna Chloramphenicol inavyoweza kufanya kazi

Chloramphenicol hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria ndani ya seli yake kwa kuzuia uzalishwaji wa protini muhimu ambazo ni vijenzi vya bakteria. Kwa kufanya hivyo huzuia ukuaji na kuenea kwa bakteria mwilini.


Chloramphenicol hutibu nini?

Chloramphenicol hutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria, baadhi ya kazi zake ni
  • Hutibu maambukizi katika mfumo wa mkojo

  • Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye masikio na macho

  • Hutibu maambukizi kwenye uti wa mgongo

  • Hutibu kipindupindu

  • Hutibu homa ya matumbo

  • Hutumika kutibu vimeta

  • Hutumika kutibu Nimonia


Ufozwaji wa dawa

Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula.


Mwingiliano wa Chloramphenicol na chakula

Chloramphenicol inaweza kutumika na chakula ama bila chakula.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Chloramphenicol

  • Wagonjwa wenye mzio wa chloramphenicol

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa nyingine jamii ya za antibayotiki


Utoaji taka wa Chloramphenicol mwilini

Kiwango kikubwa cha dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo kwa njia ya haja kubwa.


Dawa zenye muingiliano na Chloramphenicol


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Chloramphenicol;
  • Amlodipine

  • Chanjo hai ya BCG

  • Benzhydrocodone/acetaminophen

  • Fexinidazole

  • Haloperidol

  • Mifepristone

  • Ombitasvir/paritaprevir/ritonavir

  • Trazodone

  • Chanjo hai ya Typhoid

  • Vincristine liposomal

  • Vorapaxar

  • Voxelotor

  • Warfarin


Dawa zinazoweza kutumika na Chloramphenicol chini ya uangalizi;

  • Artemether/lumefantrine

  • Ceftriaxone

  • Cocaine

  • Conjugated estrogens, a kuweka ukeni

  • Diazepam intranasal

  • Estrogens conjugated

  • Levamlodipine

  • Levonorgestrel a kunywa ethinylestradiol/ferrous bisglycinate

  • Lomitapide

  • Lumefantrine

  • Oxacillin

  • Oxycodone

  • Pentobarbital

  • Phenobarbital

  • Phenytoin

  • Progesterone asili

  • Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid

  • Terbinafine

  • Tinidazole


Dawa zenye muingiliano mdogo na chloramphenicol;

  • Amoxicillin

  • Ampicillin

  • Cefixime

  • Cefotaxime

  • Cephalexin

  • Chlorpropamide

  • Cocaine

  • Dicloxacillin

  • Folic acid

  • Ospemifene

  • Penicillin g aqueous

  • Penicillin vk

  • Pentobarbital

  • Phenobarbital

  • Rifampin

  • Tolazamide

  • Tolbutamide


Matumizi ya Chloramphenicol kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Matumizi ya Chloramphenicol kwa mama mjamzito

Mpaka sasa hakuna tafiti inayoonyesha madhara ya chloramphenicol kwa mama mjamzito hivyo haipaswi kutumiwa.


Matumizi ya Chloramphenicol mama anayenyonyesha

Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha hivyo haitakiwi kutumika ama kimoja kati ya dawa na kunyonyesha mama anaweza akaacha kulingana na uhitaji.


Maudhi madogo ya Chloramphenicol;

  • Ndoto mbaya

  • Kichwa kuuma

  • Upele

  • Kuharisha

  • Maumivu ya tumbo

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Hupunguza ufanyaji kazi wa uboho wa mifupa

  • Kupungukiwa damu

  • Nganzi ya mikono na miguu

  • Michomo kwenye mshipa wa fahamu wa Optic

  • Sindromu ya Gray


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?

Kama umesahau kutumia dozi yako muone daktari au mfamasia wako kwa ushauri zaidi.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara na majibu yake

1. Je, Chloramphenicol inatibu taifodi (homa ya matumbo)?

Ndiyo, Chloramphenicol inaweza kutibu taifodi (homa ya matumbo) inayosababishwa na bakteria Salmonella typhi. Hata hivyo, kwa sasa haitumiki kama chaguo la kwanza katika nchi nyingi kwa sababu ya hatari ya madhara makubwa kama kupungua kwa seli za damu. Hutumika zaidi pale ambapo bakteria wameonyesha usugu dhidi ya antibayotiki nyingine salama zaidi kama ceftriaxone au azithromycin.

2. Chloramphenicol hutumika kwa magonjwa gani hasa?

Chloramphenical hutumika kutibu maambukizi makali ya bakteria kama:

  • Homa ya matumbo (taifodi) (hata hivyo si dawa ya chaguo la kwanza)

  • Maambukizi kwenye uti wa mgongo (meninjitis)

  • Maambukizi makali ya macho na masikio

  • Nimonia

  • Kipindupindu

  • Kimeta (anthrax)

Hutumika pale ambapo dawa nyingine hazifanyi kazi au hazipatikani.

3. Kwa nini Chloramphenicol haitumiki sana siku hizi?

Ingawa ni antibayotiki yenye nguvu, Chloramphenical ina hatari ya madhara makubwa, hususan:

  • Kupunguza uzalishaji wa damu kwenye uboho wa mifupa

  • Kusababisha upungufu mkali wa damu (aplastic anemia)

Kwa sababu hiyo, matumizi yake yamewekewa masharti makali ya kitabibu.

4. Je, Chloramphenicol ni salama kwa watoto?

Kwa tahadhari kubwa. Chloramphenical inaweza kusababisha “Sindromu ya Mtoto wa kijivu” kwa watoto wachanga, hali hatari inayosababisha:

  • Ngozi kuwa ya kijivu

  • Kushuka kwa joto la mwili

  • Kupumua kwa shida

Ndiyo maana matumizi kwa watoto wachanga hayapendekezwi isipokuwa kwa dharura chini ya uangalizi wa daktari bingwa.

5. Dalili za hatari za Chloramphenicol ni zipi ninazopaswa kuangalia?

Dalili hatarishi ni pamoja na:

  • Uchovu usio wa kawaida

  • Kupauka kwa ngozi

  • Maambukizi ya mara kwa mara

  • Kutokwa damu kirahisi

  • Maumivu ya macho au kupungua kwa uwezo wa kuona

Ukiona dalili hizi, acha dawa na wahi hospitali haraka.

6. Je, Chloramphenicol inaweza kutibu maambukizi ya virusi?

Hapana. Chloramphenical haitibu virusi kama mafua, homa ya kawaida, au UVIKO-19. Ni antibayotiki inayofanya kazi dhidi ya bakteria pekee, na kuitumia vibaya huongeza usugu wa vimelea.

7. Je, Chloramphenicol inaruhusiwa kutumika bila vipimo?


Hapana. Haitakiwi kutumika bila ushauri wa daktari. Kwa kawaida, daktari hupendekeza:

  • Vipimo vya damu

  • Ufuatiliaji wa seli za damuHii ni kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa bila dalili za mapema.

8. Chloramphenicol huanza kufanya kazi baada ya muda gani?

Kwa kawaida, huanza kuonyesha athari ndani ya saa 24–48 baada ya kuanza matumizi. Hata hivyo, mgonjwa anatakiwa amalize dozi yote hata kama anahisi nafuu mapema ili kuzuia usugu wa bakteria.

9. Je, ninaweza kunywa Chloramphenicol pamoja na dawa nyingine?

Baadhi ya dawa haziwezi kutumika pamoja na Chloramphenical kwa sababu huongeza hatari ya madhara au kupunguza ufanisi. Mfano:

  • Warfarin

  • Phenytoin

  • PhenobarbitalNi muhimu kumwambia daktari au mfamasia dawa zote unazotumia.

10. Nifanye nini nikisahau dozi ya Chloramphenicol?

Ukisahau dozi:

  • Usinywe dozi mbili kwa wakati mmoja

  • Chukua dozi mara tu unapoikumbuka kama muda haujapita sana

  • Kama una shaka, muone daktari au mfamasia kwa ushauriKufuata ratiba sahihi ni muhimu ili kuzuia kushindwa kwa matibabu.


ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

9 Septemba 2021, 09:55:16

Rejea za mada hii:-

MEDSCAPE.Chloramphenicol. https://reference.medscape.com/drug/chloramphenicol-iv-chloromycetin-342554#90. Imechukuliwa 08/09/2021

DRUG.COM. Chloramphenicol. https://www.drugs.com/dosage/chloramphenicol.html. Imechukuliwa 08/09/2021

NCBI. Chloramphenicol. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK555966/. Imechukuliwa 08/09/2021

Rxlist consumer. Chloramphenicol. https://www.rxlist.com/consumer_chloramphenicol_chloramphenicol/drugs-condition.htm. Imechukuliwa 08/09/2021

World Health Organization. WHO Model List of Essential Medicines. 23rd list. Geneva: World Health Organization; 2023.

World Health Organization. Background document: The diagnosis, treatment and prevention of typhoid fever. Geneva: WHO; 2003.

Mandell GL, Bennett JE, Dolin R. Mandell, Douglas, and Bennett’s Principles and Practice of Infectious Diseases. 9th ed. Philadelphia: Elsevier; 2020.

Katzung BG, Trevor AJ. Basic & Clinical Pharmacology. 15th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2021.

Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2023.

Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Typhoid fever: Treatment and antimicrobial resistance. Atlanta: CDC; 2024.

Brooks GF, Carroll KC, Butel JS, Morse SA, Mietzner TA. Jawetz, Melnick & Adelberg’s Medical Microbiology. 28th ed. New York: McGraw-Hill; 2019.

Murray PR, Rosenthal KS, Pfaller MA. Medical Microbiology. 9th ed. Philadelphia: Elsevier; 2020.

Sweetman SC, ed. Martindale: The Complete Drug Reference. 41st ed. London: Pharmaceutical Press; 2023.

UpToDate. Chloramphenicol: Drug information and clinical use. Waltham, MA: UpToDate Inc.; 2024.

Bhalerao S, Talsania N. Chloramphenicol-induced aplastic anemia: a review. J Pharmacol Pharmacother. 2019;10(2):65–70.

Parry CM, Hien TT, Dougan G, White NJ, Farrar JJ. Typhoid fever. N Engl J Med. 2002;347(22):1770–82.
bottom of page