Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Septemba 2021 15:57:29
Dawa Ciprofloxacin
Ciprofloxacin ni moja kati ya antibiotiki kwenye kundi la Fluoroquinolones. Dawa hii ina uwezo wa kukabiliana sana na bakteria jamii ya gramu hasi.
Fomu na uzito wa dawa
Dawa hii hupatikana katika fomu ya
Kidonge chenye uzito wa
Miligramu 250
Miligramu500
Suspension yenye uzito wa
Miligramu 250 kwa kila mililita 5
Miligramu 125 kwa kilamililita 5
Dawa zilizo kundi moja na Ciprofloxacin
Dawa zilizo kundi moja na ciprofloxacin ni ;
Norfloxacin
Gemifloxacin
Levofloxacin
Moxifloxacin
Ofloxacin
Delafloxacin
Sparfloxacin
Ciprofloxacin hutibu nini?
Hutibu maambukizi katika mfumo wa mkojo
Hutibu maambukizi katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye mfumo wa upumuaji
Hutibu kaswende na maambukizi ya bakteria kwenye via vya uzazi
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye ngozi
Huttibu maambukizi ya bakteria kwenye misuli na mifupa
Hutumika kuzuia maambukizi ya kimeta (Anthrax)
Namna Ciprofloxacin inavyoweza kufanya kazi na ufyonzaji wake
Ciprofloxacin hufanya kazi ya kuua na kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuharibu urudiaji wa DNA na kupunguza usanisi wa protini katika miundo ya seli ya bakteria.
Ufozwaji wa ciprofloxacin
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula
Vimelea wanaodhuriwa na Ciprofloxacin
Campylobacter jejuni
Escherichia coli
Haemophilus spp
Klebsiella pneumonia
Pseudomonas aeruginosa
Shiggella spp
Streptococcus pneumonia
Staphylococcus spp
Vibrio cholera
Salmonella typhi
Neisseria gonorrhoea
Yersinia enterocolitica
Mwingiliano wa Ciprofloxacin na chakula
Dawa hii ni nzuri endapo itatumika na chakula kwani chakula hufanywa dawa hii ifyozwe vizuri.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ciprofloxacin
Wagonjwa wenye mzuio wa hii na dawa nyyingine jamii ya Fluoroquinoles
Utoaji taka za Ciprofloxacin mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii tulolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo kwa njia ya haja kubwa
Dawa zenye muingiliano na Ciprofloxacin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ciprofloxacin;
Agomelatine
Bepridil
Ziprasidone
Tizanidine
Thioridazine
Piperaquine
Mesoridazine
Dronedarone
Dawa zenye muingiliano mdogo na ciprofloxacin
Dawa zenye muingiliano mdogo na ciprofloxacin ambazo unaweza ukatumia walau masaa mawili kabla na masaa sita baada ya kutumia ciprofloxacin;
Antiacid
Carafate(sucralfate)
Videx (didanosine)
Multivitamins or supplements with magnesium, calcium,aluminium,iron, zinc
Phosphate binder
Matumizi ya ciprofloxacin kwa mama mjamzito
Wakati wa ujauzito dawa hii inaweza kutumika pale tu panakuwa na uhitaji mkubwa wa mhimu zaidi hiyo; unashauriwa kumuona daktari wako kwa maushauri na maelekezo zaidi.
Matumizi ya Ciprofloxacin kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama na inaweza kuleta madhara kwa mtoto hivyo mshirishe daktari wako kabla kutumia dawa hii.
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako unaweza kutumia mara pale utakapo kumbuka, kama ni chini ya masaa sita kabla ya dozi inyofuata usitumie dozi hiyo,tumia dozi inayofuata kwa muda sahihi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-