Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Septemba 2021 18:28:24
Dawa Clofazimine
Clofazimine ni moja ya antibiotiki jamii ya riminophenazine iliyo kwenye kundi la antitubakula, hutumika pamoja na dawa zingine kutibu ukoma. Hufanya kazi kwa kuua bakteria aina ya mycobacterium leprae (Hensen’s bacillus).
Majina mengine ya Clofazimine
Majina mengine ya Clofazimine ni;
Clofaz
Clofozine
Fazim
Hansepran
Lamprene
Dawa zilizo kundi moja na Clofazimine
Dawa zilizo kundi moja na Clofazimine ni ;
Isoniazid
Rifampicin
Pyrazinamide
Ethambutol
Bedaquiline
Dapsone
Fomu ya dawa ya Clofazimine
Dawa hii ipo katika fomu ya tembe yenye uzito wa 50mg.
Clofazimine hutibu nini?
Hutumika kutibu ukoma
Hutibu ukoma sugu kwenye dapson
Hutibu madhara ya ukoma kama erythema nodosum leprosum
Ili vimelea vya ukoma visitengeneze usugu kwenye dawa hii, inashauriwa clofazimine itumike pamoja nadawa zingine kutibu ukoma.
Namna Clofazimine inavyoweza kufanya kazi
Ingawa namna halisi clofazimine inavyofanya kazi haifahamiki, uwezo wake wa kitiba unaonekana kutokana na uwezo wake wa kuharibu ukuta wa bakteria. Dawa hii huingiliana na phospholipid kijenzi maalumu kwenye ukuta wa bakteria wa ukoma na kutengeneza lysophospholipids na kufanya ukuta usijikimu na kiasi cha kuharibu uwezo wake wa kuingiza K+ ndani ya bakteria na kisha kushindwa kuzalisha nishati na kufa.
Uwezo wa clofazimine kupunguza michomo kinga hutokana na matokeo ya kuzuia uamshwaji wa chembe T za ulinzi mwilini.
Vimelea wanaodhuriwa na Clofazimine
Mycobacterium leprae
Ufozwaji wa dawa na mwingiliano na chakula
Mara baada ya kunywa dawa, asilimia 45 hadi 62 ya dawa hufyonzwa kwenye utumbo na kuingia kwenye damu. Matumizi ya Clofazimine pamoja na chakula huongeza ufyonzwaji wake kwa asilimia 30 ukilinganisha na matumizi bila chakula. Hakuna chakula kilichofahamika kuwa na mwingiliano na chakula.
Utoaji taka wa Clofazimine mwilini
Kiasi Fulani cha dawa hupatikana kwenye kinyesi na hivyo kuweza kusema dawa hii hutolewa kwa njia ya kinyesi wakati kiasi kingine kidogo hupatikana kwenye jasho, mafuta ya ngozi na mate. Utoaji wa mazao ya umetaoli wa dawa kwenye mkojo uliokusanywa masaa 24 umetoa majibu ya kiasi kidogo sana kisicho na mashiko.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Clofazimine
Wagonjwa wenye mzio wa Clofazimine.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya antitubekula
Dawa zenye mwingiliano na Clofazimine
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Clofazimine;
Entrectinib
Fexinidazole
Glasdegib
Hydroxychloroquine sulfate
Ivosidenib
Lefamulin
Macimorelin
Pitolisant
Ribociclib
Dawa zinazoweza kutumika na Clofazimine chini ya uangalizi;
Azithromycin
Chloroquine
Deutetrabenazine
Dofetilide
Escitalopram
Fostemsavir
Gemtuzumab
Lofexidine
Osilodrostat
Oxaliplatin
Ozanimod
Selpercatinib
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Triclabendazole
Voclosporin
Matumizi ya Clofazimine kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Clofazimine kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii hupitia kwenye kondo la nyuma na kuingia kwa mtoto. Inapoingia kwa mtoto hubadilisha rangi ya ngozi ya mtoto na hivyo haishauriwi kutumika kwa mjamzito.
Matumizi ya Clofazimine mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inasambaa kwenye maziwa ya mama hivyo isitumike kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Clofazimine
Kubadirika kwa rangi ya ngozi
Kuwashwa mwili
Vipele
Maumivu ya tumbo
Kuharisha
Kutapika
Kichefuchefu
Kukosa hamu ya kula
Kupata choo kigumu
Manjano
Kizunguzungu
Mwili kuchoka
Kichwa kuuma
Maumivu ya mifupa
Kupungukiwa damu
Homa
Kushindwa kutambua radha
Ini kuongezeka
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi kwa wakati sahihi muone daktari au mfamasia wako ili akupe maelekezo ya kutumia dozi nyingine inayofuatia.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:56:16
Rejea za mada hii:-