Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Septemba 2021 09:24:46
Dawa Cloxacillin
Cloxacillin ni moja kati ya antibiotiki katika kundi la ‘Penicillin pinzani kwa Penicillinase’ inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria jamii ya gram chanya na wale wanaozalisha kimeng’enya cha beta lactamase. Majina mengine ya dawa hii ni Orbenin, Cloxaca, Tegopen, Cloxapen
Dawa zilizo kundi moja na Cloxacillin
Dawa zilizo kundi moja na cloxacillin ni;
Oxacillin
Dicloxacillin
Methacillin
Nafcillin
Fomu na uzito wa dawa
Fomu ya dawa ya cloxacillin
Dawa hii inapatikana katika fomu ya;
Suspension
Kidonge
Uzito wa dawa ya cloxacillin
Suspension ni miligramu 125 kwa kila mililita 5
Kidonge cha miligramu 250 na miligramu 500
Cloxacillin hutibu nini?
Dawa cloxacillin hutumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii kwenye sehemu mbalimbali mfano;
Mfumo wa mkojo
Masikio na koo
Uti wa mgongo
Mfumo wa hewa
Hutibu nimonia
Mifupa
Hutibu sepsisi na septisemia
Ngozi
Homa ya matumbo
Namna Cloxacillin inavyoweza kufanya kazi
Cloxacillin hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria ndani ya seli yake kwa kuzuia utengenezaji wa hatua ya mwisho ya ukuta wa seli yake.
Ufozwaji wa cloxacillin
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ukiwa hujala.Inashauriwa kutumia saa moja mpaka mawili kabla hujala.
Vimelea wanaodhuriwa na cloxacillin
Staphylococcus spp
Streptococcus spp
Escherichia coli
Haemophilus spp
Neisseria spp
Mwingiliano wa Cloxacillin na chakula
Cloxacillin ni nzuri endapo itatumika bila chakula kwani tumbo likiwa halina chakula ufozwaji wake hufanyika vizuri.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cloxacillin
Wagonjwa wenye mzuio wa hii na dawa nyingine jamii ya Penicillin
Wagonjwa wenye mzuio wa Cepharosporins
Utoaji taka za Cloxacillin mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo kwa njia ya haja kubwa.
Dawa zenye muingiliano na Cloxacillin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Cloxacillin;
Chanjo hai ya BCG
Doxycycline
Omadacycline
Sarecycline
Eravacycline
Demeclocycline
Oxytetracycline
Dawa zinazoweza kutumika na Cloxacillin chini ya uangalizi;
Warfarin
Ibuprofen
Esomeprazole
Omeprazole
Pantoprazole
Lansoprazole
Asprin
Chloroquine
Choline magnesium trisalicylate
Deflazacort
Dexlansoprazole
Esomeprazole
Sodium becarbonate
Methotrexate
Dawa zenye muingiliano mdogo na cloxacillin;
Clarithromycin
Allopurinol
Chloramphenicol
Rifampicin
Erythromycin
Didanose
Atenolol
Azithromycin
Chlorothiazide
Clarithromycin
Metolazone
Colestipol
Hydrochlorothiazide
Maudhi madogo ya Cloxacillin
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kuchoka
Kutetemeka
Koo kuuma
Homa
Misuli kukaza na kuuma
Kutapika
Kuwasha mwilini na kupata vipele
Kubadirika kiasi cha mkojo na rangi
Manjano kwenye ngozi na macho
Viungio vya mwili kuuma na kuvimba
Matumizi ya Cloxacillin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Cloxacillin kwa mama mjamzito
Mpaka sasa hakuna makala inayoonyesha madhara ya cloxacillin kwa mama mjamzito.Itumike pale penye uhitaji zaidi.
Matumizi ya Cloxacillin kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama kwa kiasi kidogo kama itatumika tahadhari inapaswa kuchukuliwa.
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako unaweza kutumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea na dozi inayofuata kama muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-