top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

19 Septemba 2021 13:27:52

Dawa Cycloserine

Dawa Cycloserine

Cycloserine ni moja kati ya antibiotiki katika kundi la antitubakula inayotumika na dawa zingine katika matibabu ya magonjwa yaliyosugu kwenye dawa zingine kutokana na maambukizi ya bakteria mycobacteria tuberculae kama kifua kikuu kutokana (TB).


Majina mengine ya Cycloserine


Majina mengine ya Cycloserine ni;

Seromycin


Fomu na uzito wa Cycloserine


Dawa hii ipo katika fomu yanye uzito wa 250mg


Dawa zilizo kundi moja na Cycloserine


Dawa zilizo kundi moja na Cycloserine ni;

  • Isoniazid

  • Ethambutol

  • Rifampicin

  • Pyrazinamide


Namna Cycloserine inavyoweza kufanya kazi


Cycloserine ni dawa analogia ya D alanine. Hufanya kazi kwa kuingilia uzalishaji wa vijenzi vya ukuta wa seli katika saitoplazim ya bakteria kwa kushindana na vimeng’enya viwili L-alanine racemase kinachotengeneza D-alanine kutoka kwenye L-alanine, na D-alanylalanine synthetase, inayounga D-alanine kwenye pentapeptide ili kutengeneza peptidoglycan, kijenzi muhimu kwenye ukuta wa bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.


Vimelea wanaodhuriwa na Cycloserine


Mycobacteria tuberculae

Escherichia coli


Ufozwaji wa cycloserin


Mara baada ya kunywa dawa, asilimia 70 hadi 90 ya cycloserine hufyonzwa haraka na hupatikana kwenye damu kuleta madhara ya kitiba.


Mwingiliano wa cycloserin na chakula


Usinywe dawa hii muda mfupi kabla au baada ya kula chakula chenye mafuta mengi. Chakula chenye mafuta mengi hupunguza ufyonzwaji wake hata hivyo bado haifahamiki huzuia kwa kiasi gani.


Nusu maisha na utoaji taka wa Cycloserine mwilini


Nusumaisha ya cycloserine ni masaa 10, mara baada ya kufanya kazi asilimia 50 hutolewa kwenye mkojo ikiwa haijafanyiwa umetaboli ndani ya masaa12 na kiasi hicho huongezeka hadi asilimia 70 ndani ya masaa 24.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cycloserine


Wagonjwa wenye mzio wa Cycloserine

Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya antitubakula


Dawa zenye muingiliano na Cycloserine


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Cycloserine;

Hakuna orodha ya dawa zenye mwingiliano mkali na cycloserine


Dawa zinazoweza kutumika na Cycloserine chini ya uangalizi;


Ethionamide

Isoniazid

Sodium picosulfate/Magnesium oxide


Dawa zenye muingiliano mdogo na Cycloserine;

Hakuna orodha ya dawa zenye mwingiliano mwingiliano mdogo na cycloserine


Matumizi ya Cycloserine kwa mama mjamzito na anayenyoneysha


Matumizi ya Cycloserine kwa mama mjamzito

Tafiti zinaonesha dawa hii inatakiwa kutumiwa kwa tahadhari kwani inaweza kuleta madhara kwa mtoto.


Matumizi ya Cycloserine mama anayenyonyesha

Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha na haijaonesha kuleta madhara kwa mtoto.


Maudhi ya Cycloserine


  • Kudhoofika mwili

  • Kuchanganyikiwa

  • Kusinzia mara kwa mara

  • Kutokuwa na utulivu

  • Mapigo ya moyo kubadirika

  • Upungufu wa folate

  • Kukosa uwiano wakati wa mwendo

  • Kuongezeka kwa vimeng’enya vya ini

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kupoteza fahamu

  • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:56:16

Rejea za mada hii:-

bottom of page