Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Septemba 2021, 17:30:44
Dawa Dapsone
Dapsone ni dawa iliyotengenezwa kutoka kwenye kemikali diamino-sulfone yenye uwezo wa kuzuia michomo kutokana na kinga za mwili pamoja na uwezo w akufanya kazi kama antibayotiki. Hutumika awali kwenye matibabu ya ukoma na leprosy ugonjwa wa ngozi wa dermatitis herpetiformis.
Majina mengine ya Dapsone
Majina mengine ya Dapsone ni;
Avlosulfon
Aczone
Namna Dapsone inavyoweza kufanya kazi
Hufanya kazi kwa kupunguza uvimbe kutokana mwitikio wa kinga za mwili na kuzuia ukuaji wa bakteria.
Kwenye tiba ya ukoma, dapson hufanya kazi kwa kuzuia uzalianaji wa bakteria Mycobacterium leprae. Hufanya hivi kwa kuzuia bakteria kutumia para-aminobenzoic acid (PABA) ili kuzalisha folic acid
Licha ya kutofahamika vema namna inavyofanya kazi kutibu magonjwa ya ngozi, dapson hufahamika kuweza kufanya kazi hiyo kwa kudhuru utendaji kazi wa chembe za ulinzi za neutrophil, eosinophils na monosait.
Dawa zilizo kundi moja na Dapsone
Dawa zilizo kundi moja na Dapsone ni ;
Clofazimine
Rifampicin
Fomu ya dawa ya Dapsone
Dawa hii ipo katika fomu ya vidonge vyenye uzito wa miligramu;
25mg
100mg
Dapsone hutibu nini?
Matumizi ambayo yameidhinishwa na FDA
Hutumika kutibu ukoma
Hutumika kutibu ugonjwa wa ngozi wa dermatitis herpetiformis
Hutumika kutibu ugonjwa wa Hansen's
Hutumika kutibu kifua kikuu ikiunganishwa na dawa nyingine kama Rifampicin na Ethambutol
Hutumika kama kinga na tiba ya nimonia ya jiroveci au Pneumocystis (carinii) jiroveci
Matumizi ambayo hayajahidhinishwa na FDA
Kutibu malenge ya makubwa ya dermatosis
Malenge makubwa ya lupus erythematosus,
Kutibu malenge makubwa ya erythema elevatum diutinum
Kutibu magonjwa ya malenge makubwa kutokana na shambulio binafsi la kinga za mwili mfano IgA pemphigus, pustular dermatosis ya kope za macho, pemphigus vulgaris, pemphigus foliaceous, na epidermolysis bullosa acquisita
Kutibu michomo kinga kwenye mishipa ya damu kama ugonjwa wa leukocytoclastic na urticarial
Kutibu magonjwa ya ngozi kutokana na ongezeko la neutrophil mfano sindromu ya Sweet, pyoderma gangrenosum na sindromu ya Behcet
Kutibu lupus erythematosus ya wastani, polychondritis ya kujirudia, granuloma annulare, loxoscelism, granuloma faciale, rosacea, panniculitis, pustular psoriasis, chunusi kubwa na rhinosporidiosis
Vimelea wanaodhuriwa na Dapsone
Mycobacterium Leprae
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikiingia kwenye mfumo wa chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dapson
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Dapsone ni wale
Wagonjwa wenye mzio na Dapsone.
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Antileprosy.
Mwingiliano wa Dapsone na chakula
Dawa hii huweza kutumika kukiwa na chakula ama bila chakula.
Utoaji taka wa Dapsone mwilini
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo.
Matumizi ya Dapsone kwa mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Dapsone kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto. Hivyo haishauriwi kutumia dawa hii wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Dapsone mama anayenyonyesha
Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha na kusababisha madhara kwa mtoto hivyo haitakiwi kutumiwa na mama anayenyonyesha.
Dawa zenye muingiliano na Dapsone
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Dapsone;
Abametapir
Aluminum hydroxide
Apalutamide
Calcium carbonate
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya Typhoid
Dapsone topical
Famotidine
Fexinidazole
Ibuprofen/famotidine
Idelalisib
Ivosidenib
Lansoprazole
Lonafarnib
Mefloquine
Nefazodone
Saquinavir
Selinexor
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Tucatinib
Voxelotor
Dawa zinazoweza kutumika na Dapsone chini ya uangalizi;
Carbamazepine
Cenobamate
Clarithromycin
Cobicistat
Digoxin
Efavirenz
Erythromycin base
Isoniazid
Ketoconazole
Methotrexate
Mifepristone
Rifabutin
Rifampin
Stiripentol
Tazemetostat
Tecovirimat
Teriflunomide
Tetracaine
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Dapsone;
Artemether/lumefantrine
Atazanavir
Cortisone
Dexamethasone
Etravirine
Fluconazole
Griseofulvin
Hydrocortisone
Methylprednisolone
Metronidazole
Miconazole vaginal
Nifedipine
Phenobarbital
Phenytoin
Prednisone
Rifapentine
Ritonavir
Rufinamide
Secobarbital
Sulfamethoxazole
Verapamil
Voriconazole
Zafirlukast
Zidovudine
Maudhi ya dapsone
Kwenye damu
Upungufu wa damu kutokana na kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu
Methemoglobinemia
Leukopenia
Agranulocytosis
Ngozi
Mzio wa ngozi
Kubanduka kwa ngozi
Mebilliform eruption
Exfoliative erythroderma
Lupus erythematosus ya dawa
Epidermal necrolisis
Mfumo wa beva
Nyuropathi ya pembeni na kupoteza uwezo wa kimota
Kiakili
Kukosa usingizi na saikosis
Macho
Uono hafifu
Sikio, kinywa na pua
Kusikia masauti,
Hisia za vitu kuzunguka
Moyo
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Mapafu
Eosinophilia ya mapafu
Ini
Hepatitis ya dawa
Sindromu ya dapsone
Manjano ya kutulia na kupungua kiwango cha albumin kwenye damu bila kuwa na kiwango kikubwa cha protini
Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya kula
Kupungua uzito
Michomo kwenye kongosho
Figo
Sindromu ya Nephrotic,
Albuminuria,
Nekrosisi ya papilla za figo
Sindromu ya dapson
Hutokea wiki 2 hadi 6 toka mgonjwa ameanza kutumia dawa. Huwa na dalili za homa, harara kwenye ngozi, na hepataitis. Vipimo huonyesha ongezeko la vimeng’enya vya ini kwenye damu na eosinophilia. Huweza sababisha mgonjwa kupoteza maisha kama asipopata matibabu
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-