top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

10 Septemba 2021 12:38:21

Dawa Dicloxacillin

Dawa Dicloxacillin

Ni moja ya antibayotiki kwenye kundi la pili la Penicillin, antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wasiozalisha beta lactam na hufahamika kwa majina mengine kama dycill, dynapen.


Uzito na fomu ya Dicloxacillin


Dawa hupatikana katika fomu ya tembe yenye uzito wa miligramu 250 na 500


Dawa zilizo kundi moja na Dicloxacillin


Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na dicloxacillin ni zifuatazo;


 • Amoxicillin

 • Bacampicillin

 • Penicillin G

 • Penicillin V

 • Methicillin

 • Ampicillin

 • Procaine Penicillin

 • Piperacillin


Dicloxacillin hutibu nini?


Dicloxacillin hutibu maambukizi yanayosababishwa na bacteria aina ya Staphylococcus aures kama;


 • Nimonia kwa watu wazima

 • Maambukizi ya ngozi na tishu zingine laini za mwili

 • Maambukizi mfumo wa juu wa hewa(falinjaitiz na bronkaitiz) kwa watoto na watu wazima

 • Osteomyelitis


Namna Dicloxacillin inavyoweza kufanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa ukuta wa bakteria na hivyo kufanya wasizaliane na kufa.


Ufyozwaji


Dawa hii hufyonzwa vizuri inapoingia kwenye mfumo wa chakula


Utoaji taka wa Dicloxacillin mwilini


Asilimia 50 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia zinazobaki hutolewa kwa njia ya haja kubwa


Vimelea wanaodhuriwa na Dicloxacillin


 • Staphylococcus Aureus


Mambo ya kufahami kabla ya kutumia dicloxacillin


Mwambie daktari wako kuwa una hali au magonjwa yafuatayo kabla ya kutumia dicloxacillin

 • Pumu ya kifua

 • Ugojnwa wa kolaitiz

 • eczema

 • Ugonjwa wa figo

 • Mzio dhidi ya dawa dicloxacillin, au zingine jamii ya penicillins

 • Ujauzito

 • Unanyonyesha


Mwingiliano wa Dicloxacillin na chakula


Dicloxacillin ni nzuri endapo itatumika pasipo chakula


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Dicloxacillin


 • Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Penicillin

 • Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya cephalosporins


Mwingiliano wa Dicloxacillin na dawa zingine


Dawa zenye mwingiliano mkali kiasi cha kutopaswa kutumia pamoja na Dicloxacillin;

 • Chanjo hai ya BCG

 • Chanjo hai ya kipindupindu

 • Demeclocycline

 • Doxycycline

 • Minocycline

 • Omadacycline

 • Sarecycline

 • Tetracycline

 • Chanjo hai ya Typhoid


Dawa hizi zina mwingiliano mdogo na Dicloxacillin lakini huhitaji mgonjwa kufanyiwa ufuatiliaji wa karibu sana kama zikitumika pamoja;

 • Aspirin

 • Axitinib

 • Bendroflumethiazide

 • Chlorothiazide

 • Choline magnesium trisalicylate

 • Dienogest/estradiol valerate

 • Ethinylestradiol

 • Hydrochlorothiazide

 • Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous Bisglycinate

 • Mestranol

 • Methotrexate

 • Methyclothiazide

 • Metolazone

 • Mycophenolate

 • Parecoxib

 • Phenindione

 • Piroxicam

 • Probenecid

 • Salicylates

 • Salsalate

 • Sulfasalazine

 • Tazemetostat

 • Tinidazole

 • Ubrogepant

 • Warfarin

 • Willow bark


Dawa zenye mwingiliano mdogo;


 • Azithromycin

 • Aztreonam

 • Chloramphenicol

 • Clarithromycin

 • Colestipol

 • Erythromycin base

 • Erythromycin ethylsuccinate

 • Erythromycin lactobionate

 • Erythromycin stearate

 • Nitazoxanide

 • Pyridoxine (antidote)


Matumizi ya Dicloxacillin kwa mama mjamzito


Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito ambapo huweza kutumika sababu hakuna tafiti zinazoenyesha madhara kwa mnyama na kwa binadamu.


Matumizi ya Dicloxacillin kwa mama anayenyonyesha


Dawa hii inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha ,hakuna tafiti zinazoenyesha madhara yatakayompata mtoto.


Maudhi ya Dicloxacillin


 • Mzio wa ngozi unaosababisha kuvimba kwa uso, midomo na ulimu

 • Choo cheusi kinachonata

 • Kushindwa pumua vema

 • Kifua kutoa miruzi

 • Ulimi kubadilika rangi

 • Homa

 • Kutetemeka

 • Kushindwa kojoa cema

 • Wekundu, malenge na kulegea kwa ngozi pamoja ya mwili au midomo

 • Degedege

 • Kuvimba kwa maungio ya mwili ( miguu na mikono)

 • Kutoka na damu na kupata majeraha kirahisi

 • Kuhisi mchovu au kuchoka

 • Kuhara

 • Maumivu ya kichwa

 • Kichefuchefu na kutapika

 • Koo chungu

 • Mvurugiko wa tumbo


Je endapo utasahau dozi yako ya dicloxacillin ufanyaje?


Kama ukisahau tumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kama muda uliopangiwa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:25

Rejea za mada hii:-

1. Medscape. Dicloxacillin. https://reference.medscape.com/drug/dicloxacillin-342477. Imechukuliwa 20/8/2021

2. NCBI. Dicloxacillin. https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Dicloxacillin. Imechukuliwa 20/8/2021

3. PubMed. Dicloxacillin. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/7036850/. Imechukuliwa 20/8/2021

4. PubChem. Dicloxacillin. https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Dicloxacillin . Imechukuliwa 20/8/2021

5. WebMd. Dicloxacillin. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-10328/dicloxacillin-oral/details. Imechukuliwa 20/8/2021

6. Dicloxacillin. https://www.drugs.com/mtm/dicloxacillin.html. Imechukuliwa 20/8/2021
bottom of page