Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Septemba 2021, 15:50:02
Dawa Ethambutol
Ethambutol ni moja kati ya antibiotic katika kundi la antitubercular inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria aina ya mycobacteria tuberculae moja wa bakteria anayesabisha kifua kikuu (TB). Ethambutol hufahamika kwa jina jingine kama myambutol
Dawa zilizo kundi moja na Ethambutol
Dawa zilizo kundi moja na ethambutol ni ;
Isoniazid
Rifampicin
Pyrazinamide
Fomu na uzito wa Ethambutol
Dawa hii ipo katika fomu vidonge vyenye uzito wa miligramu
100
400
Ethambutol hutibu nini?
Hutumika kutibu kifua kikuu (TB)
Namna Ethambutol inavyoweza kufanya kazi katika tiba
Ufanyaji kazi wake kutibu maambukizi ya TB bado haufahamiki, hata hivyo kuna ushahidi kwamba dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia kimeng’enya cha arabinosyl transferase kinachohusika katika, utengenezaji wa kuta ya nje ya bakteria na hivyo kuzuia uzalianaji wa bakteria wa TB.
Ufozwaji wa ethambutol
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikiingia kwenye mfumo wa chakula
Vimelea wanaodhuriwa na Ethambutol
Mycobacteria tuberculae
Mwingiliano wa Ethambutol na chakula
Dawa hii huweza kutumika pamoja na au bila chakula kwa kuwa ufyonzaji wake hauathiriwi na chakula. Hata hivyo kama ukitumia bila chakula unapata uchokozi wa tumbo, tumia pamoja na chakula
Tahadhari ya matumizi na watu wasiopaswa kutumia dawa ya ethambutol
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya macho kwa sababu dawa hii inaweza kusababisha kupungua kwa uono
Wagonjwa wengine wanaopaswa kuchukua tahadhari ni wale wenye;
Magonjwa ya macho kama michomo kinga kwenye uveitis na iritis
Wenye matatizo ya macho kutokana na kisukari
Wenye mtoto wa jicho
Wenye magonjwa ya ini
Wenye magonjwa ya figo
Wenye gauti
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ethambutol
Wagonjwa wenye mzio wa Ethambutol.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya antitubercular.
Utoaji taka za Ethambutol mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo hutolewa kupitia kinyesi
Dawa zenye muingiliano na Ethambutol
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ethambutol;
Chanjo hai ya BCG
Dawa zinazoweza kutumika na Ethambutol chini ya uangalizi;
Allupurinol
Aluminum hydroxide
Magnesium carbonate
Magnesium trisilicate
Febuxostat
Probenecid sodium picosulfate
Matumizi ya Ethambutol kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto. Hivyo haishauriwi kutumia dawa hii wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Ethambutol mama anayenyonyesha
Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha hivyo haitakiwi kutumika ama kimoja kati ya dawa na kunyonyesha mama anaweza akaacha kulingana na uhitaji.
Maudhi madogo ya Ethambutol
Kukosa hamu ya kula
Kuchanganyikiwa
Kichwa kuuma
Upele
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Kutapika
Kuchoka
Mwili kuwasha sana
Uono hafifu au uliofifia
Kupoteza uono kwenye jicho moja kunakodumu saa moja au zaidi
Kuongezeka kwa hisia za macho
Kupoteza uono kwenye rangi
Maumivu jicho linapocheza au nyuma ya jicho
Mkojo uliopuka, kunyesi cha kilichopauka na manjano
Mzio mkali wa ngozi
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:33
Rejea za mada hii:-