top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

3 Juni 2022 18:25:55

Dawa Flucamox

Dawa Flucamox

Flucamox ni dawa jamii ya antibayotiki yenye muunganko wa Flucloxacillin na amoxycillin. Muunganiko huu huipa flucamox uwanja mpana zaidi wa kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria wanaozuliwa na dawa hizo.


Uzito na fomu ya Flucamox


Flucamox hupatikana kama tembe yenye uzito wa miligramu 500. Kila miligramu 500 za flucamox huwa na miligramu 250 za flucloxacillin na miligramu za amoxicillin.


Dawa kundi moja na Flucamox


Dawa zingine zilizo kundi moja na Flucamox ni zile ambazo huwa kundi la amoxicillin na flucloxacillin ni kama vile:


 • Amoxicillin (Amoxil)

 • Amoxicillin/clavulonate (Augmentin)

 • Ampicillin

 • Apalcillin

 • Carbapenems

 • Carbenicillin

 • Cephalosporins

 • Cephamycins (cephems)

 • Cloxacillin

 • Mezlocillin

 • Monobactams

 • Nafcillin

 • Oxacillin

 • Penicillin G

 • Penicillin V.

 • Piperacillin

 • Ticarcillin


Vimelea wanaodhuriwa na Flucamox


Vimelea wanaodhuliwa na Flucamox ni pamoja na:


 • Staphylococcus aureus

 • Staphylococcus epidermidis

 • Streptococcus pneumonia

 • Streptococcus pyogenes

 • Streptococcus agalactiae

 • Clostridia tetani

 • Clostridia botulinum

 • Clostridia perfringens

 • Clostridia difficile

 • Bacillus anthracis

 • Corynebacterium diphtheria

 • Listeria monocytogenes

 • Helicobacter pyroli

 • Enterococcus

 • Haemophilus

 • Moraxella


Flucamox hutibu nini?:


Flucamox hutibu magonjwa yafuatayo yanayosababishw ana bakteria wanaodhuriwa na dawa hii:


 • Maambukizi kwenye koo

 • Maambukizi kwenye ngozi kama selulaitiz, usaha, jipu

 • Maambukizi ya upili kwenye ngozi kama kwa wogonjwa wenye pumu ya ngozi, chunusi na vidonda

 • Maambukizi kwenye mfumo wa hewa kama jipu, usaha kwenye mpafu

 • Maambukizi kwenye masikio

 • Maambukizi kwenye tonses

 • Kusambaa kwa sumu ya bakteri kwenye damu

 • Maambukizi kwenye sainaz

 • Maambukizi kwenye moyo kama endokadaitiz

 • Maambukizi ya njia ya mkojo kama UTI

 • Maambukizi kwenye mifupa kama osteoathraitiz

 • Homa ya uti wa mgongo

 • Homa ya matumbo


Namna Flucamox inavyoweza kufanya kazi


Flucamox hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa kuta ya nje ya bakteria na hivyo kusababisha kuta hiyo kufa na hatimaye bakteria hufa pia.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Flucamox


Flucamox haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na flucloxacillin, amoxicillin na dawa zingine jamii ya penicillin.


Dawa hii haipaswi kutumika pia kwa wagonjwa waliowahi kupata mzio kwa kutumia dawa hii au dawa zingine jamii yake.


Utoaji taka mwilini


Flucamox kwa kiasi kikubwa hutolewa njia ya mkojo


Matumizi ya Flucamox kwa mama mjamzito


Taarifa za tafiti zilizopo hazijaweza kuonyesha madhara kwa vichanga waliozaliwa na wamama wajawazito waliotumia dawa hii wakati wa ujauzitotafiti. Hata hivyo matumizi ya dawa hii yanapaswa kuangalia faida dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza


Matumizi ya Flucamox kwa mama anayenyonyesha


Kiasi kidogo cha dawa huingia kwenye maziwa ya mama, na hivyo hofu ya kusabaisha mzio kwa mtoto inapaswa kufikiriwa, baadhi ya madhara yaliyoonekana kwenye tafiti ni pamoja na kusababisha kuhara kwa mtoto. Hivyo matumizi ya flucamox wakati wa kunyonyesha yanapaswa kuzingatia faida dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto.


Dawa zenye mwingiliano mkali na Flucamox


Dawa zifuatazo hazipaswi kutumika pamoja na flucamox kutokana na kuwa na mwingiliano mkali:


 • Dawa zenye mwingiliano mkali

 • Chanjo hai ya BCG

 • Chanjo hai ya kipindupindu

 • Chanjo hai ya taifodi

 • Demeclocycline

 • Doxycycline

 • Eravacycline

 • Minocycline

 • Mycophenolate

 • Omadacycline

 • Pexidartinib

 • Pretomanid

 • Sarecycline

 • Tetracycline


Dawa zenye mwingiliano wa wastani na flucamox


Dawa zifuatazo endapo zitatumika pamoja na flucamox mgonjwa anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa mtaalamu wa afya:

 • Acyclovir

 • Allopurinol

 • Aspirin

 • Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate

 • Bazedoxifene/conjugated estrogens

 • Bendroflumethiazide

 • Chlorothiazide

 • Choline magnesium trisalicylate

 • Cyclopenthiazide

 • Dienogest/estradiol valerate

 • Estradiol

 • Ethinylestradiol

 • Hydrochlorothiazide

 • Levonorgestrel/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate

 • Mestranol

 • Methotrexate

 • Methyclothiazide

 • Metolazone

 • Salicylates

 • Salsalate

 • Sodium phenylacetate

 • Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid

 • Sulfasalazine


Dawa zenye mwingiliano mdogo sana na flucamox


 • Amiloride

 • Azithromycin

 • Aztreonam

 • Chloramphenicol

 • Clarithromycin

 • Erythromycin base

 • Erythromycin ethylsuccinate

 • Erythromycin lactobionate

 • Erythromycin stearate

 • Pyridoxine (antidote)


Maudhi madogo ya Flucamox


Maudhi ya mara kwa mara


 • Hisia za kuugua

 • Kichefucehfu na kutapika

 • Kuhara

 • Hisia za kuvimbiwa

 • Tumbo kujaa gesi


Maudhi ya nadra sana


 • Upungufu wa chembe nyeupe za damu

 • Upungufu wa chembe sahani za damu

 • Eosinophilia

 • Upungufu wa damu kutokana na uhalibifu wa chembe nyekundu za damu

 • Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili

 • Mzio wa anafailaksia

 • Kuungua kwenye koo la chakula

 • Oesophagitis

 • Kukereketa kwa koo

 • Maumivu ya mdomo

 • Manjano

 • Magonjwa ya ngozi kama yutikaria na papula

 • Syndromu ya Stevens-Johnson

 • Kuoza kwa ngozi

 • Erythema multiforme

 • Maumivu ya maungo ya mwili

 • Maumivu ya misuli

 • Nephratiz


Je endapo utasahau dozi ya Flucamox ufanyaje ?


Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa kunyw adozi nyingine umefika ambapo utapaswa kusubilia muda ufike ndipo utumie dozi hiyo na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.


Uhifadhi ya Flucamox


Hifadhi dawa yako kwenye kikopo cha kutunzia dawa kilichokuja na dawa na katika joto la mazingira. Usiweke kwenye friji au sehemu yenye mwanga wa jua au joto ili kuepuka kuiharibu dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

4 Juni 2022 08:39:17

Rejea za mada hii:-

1. Science Direct. Beta Lactam Antibiotic. https://www.sciencedirect.com/topics/pharmacology-toxicology-and-pharmaceutical-science/beta-lactam-antibiotic#. Imechukuliwa 03.06.2022

2. Flucloxacillin. https://www.medicines.org.uk/emc/product/545/smpc#gref. Imechukuliwa 03.06.2022

3. Sharon S. Castle. Amoxicillin. https://www.sciencedirect.com/topics/chemistry/amoxicillin. Imechukuliwa 03.06.2022
bottom of page