top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Juni 2022 09:53:30

Dawa flucloxacillin

Dawa flucloxacillin

Flucloxacillin ni dawa ya antibayotiki kutoka kwenye kundi la penicillin inayotumika sana kutibu magonjwa ya ngozi na tishu laini kutokana na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.


Flucloxacillin huwa na uwanja mdongo wa kuua vimelea jamii ya gramu hasi isipokua kimelea staphylococcus aureus aliye sugu kwenye methicillin.


Majina mengine ya flucloxacillin


Flucloxacillin hufahamika kwa majina ya kibiashara kama:

 • Fluclox

 • Staphlex


Uzito na fomu ya Flucloxacillin


Flucloxacillin hupatikana kama unga kwa ajili ya kuchoma sindano ya misuli au mishipa wa damu baada ya kuchanganywa na maji. Hupatikana pia kama tembe yenye uzito wa miligramu 500 au kimiminika kwa ajili ya kunywa.


Dawa kundi moja na Flucloxacillin


Dawa zingine zilizo kundi moja na Flucloxacillin ni kama vile:

 • Amoxicillin (amoxil)

 • Amoxicillin/clavulonate (augmentin)

 • Ampicillin (unasyn)

 • Dicloxacillin (dycill)

 • Nafcillin (nallpen)

 • Oxacillin (bactocill)

 • Penicillin g (pfizerpen, permapen)

 • Penicillin v.

 • Piperacillin (pipracil)

 • Piperacillin/tazobactam


Vimelea wanaodhuriwa na Flucloxacillin


Vimelea wanaodhuliwa/kuuliwa na flucloxacillin ni pamoja na:


 • Staphylococcus aureus

 • Staphylococcus epidermidis

 • Streptococcus pneumonia

 • Streptococcus pyogenes

 • Streptococcus agalactiae

 • Clostridia tetani

 • Clostridia botulinum

 • Clostridia perfringens

 • Clostridia difficile

 • Bacillus anthracis

 • Corynebacterium diphtheria

 • Listeria monocytogenes

 • Helicobacter pyroli

 • Enterococcus

 • Haemophilus

 • Moraxella


Flucloxacillin hutibu nini?:


Flucloxacillin hutibu magonjwa yafuatayo yanayosababishw ana bakteria wanaodhuriwa na dawa hii:


 • Homa ya matumbo

 • Homa ya uti wa mgongo

 • Jipu kwenye mapafu

 • Kinga ya maambukizi kabla ya upasuaji

 • Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu

 • Kutibu kidonda chenye maambukizi

 • Kutibu malenge yaliyopata maambukizi

 • Maaambukizi ya bakteria kwenye kidonda cha kuungua

 • Maambukizi kwenye koo

 • Maambukizi kwenye kuta za moyo kama endokadaitizi

 • Maambukizi kwenye mfumo wa kati na wa nnje wa sikio

 • Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo kama UTI

 • Maambukizi kwenye mifupa

 • Maambukizi kwenye ngozi kama jipu, Selulaitiz, Sinusaitiz, pumu ya ngozi na chunusi

 • Maambukizi kwenye tonses

 • Nimonia


Namna Flucloxacillin inavyoweza kufanya kazi


Flucloxacillin hufanya kazi kwa kujishikiza kwenye mlango wa penicillin ulio kwenye ukuta wa nje wa bakteria. Mlango wa penicillin hufanya kazi ya kuzalisha ukuta wan je wa bakteria, na hivyo kujishikiza kwa dawa kwenye ukuta huu, huzuia uzalishaji wa vijenzi muhimu vya ukuta wa bakteria katika na hivyo hufa.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Flucloxacillin


Flucloxacillin haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na flucloxacillin, amoxicillin na dawa zingine jamii ya penicillin.


Dawa hii haipaswi kutumika pia kwa wagonjwa waliowahi kupata mzio kwa kutumia dawa hii au dawa zingine jamii yake.


Matumizi ya flucloxacillin na pombe


Unaweza kutumia flucloxacillin na pombe, hata hivyo usitumie pombe nyingi pamoja na dawa hii kuepuka maudhi ya kichefuchefu na kutapika.


Ufyonzwaji wa flucloxacillin


Mara baada ya kunywa dawa, ni asilimia 50 hadi 70 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu kwa ajili ya kufanyakazi yake.


Utoaji taka mwilini


Flucloxacillin kwa kiasi kikubwa hutolewa njia ya mkojo


Nusu maisha ya flcloxacillin


Flucloxacillin mara baada ya kuingia kwenye damu, hudumu kwa muda wa saa 0.75 hadi 1 kabla ya kutolewa nje ya mwili.


Matumizi ya Flucloxacillin kwa mama mjamzito


Taarifa za tafiti zilizopo hazijaweza kuonyesha madhara kwa vichanga waliozaliwa na wamama wajawazito waliotumia dawa hii wakati wa ujauzitotafiti. Hata hivyo matumizi ya dawa hii yanapaswa kuangalia faida dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza


Matumizi ya Flucloxacillin kwa mama anayenyonyesha


Kiasi kidogo cha dawa huingia kwenye maziwa ya mama, na hivyo hofu ya kusabaisha mzio kwa mtoto inapaswa kufikiriwa. Hivyo matumizi ya flucloxacillin wakati wa kunyonyesha yanapaswa kuzingatia faida dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto.


Dawa zenye mwingiliano na flucloxacillin


Dawa zifuatazo huwa na mwingiliano endapo zitatumika pamoja na flucloxacillin. Ongea na daktari wako kuona kama zinaruhusiwa kutumika pamoja au la ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.


 • Abemaciclib

 • Acalabrutinib

 • Acemetacin

 • Acenocoumarol

 • Albendazole

 • Alectinib

 • Alpelisib

 • Amikacin

 • Aminophylline

 • Amiodarone

 • Amlodipine

 • Aripiprazole

 • Aripiprazole lauroxil

 • Astemizole

 • Atazanavir

 • Atenolol

 • Atorvastatin

 • Atracurium

 • Atracurium besylate

 • Atropine

 • Axitinib

 • Azithromycin

 • Chanjo hai ya BCG

 • Belantamab mafodotin

 • Bicalutamide

 • Bortezomib

 • Bosentan

 • Bosutinib

 • Brentuximab vedotin

 • Brigatinib

 • Budesonide

 • Busulfan

 • Cabazitaxel

 • Cabergoline

 • Capmatinib

 • Capreomycin

 • Carbamazepine

 • Cefaclor

 • Celecoxib

 • Cephalexin

 • Ceritinib

 • Cerivastatin

 • Chlorpromazine

 • Cholic Acid

 • Cimetidine

 • Cinoxacin

 • Ciprofloxacin

 • Cisapride

 • Cisatracurium

 • Clarithromycin

 • Clindamycin

 • Clomipramine

 • Clonazepam

 • Clonidine

 • Cobimetinib

 • Colistin

 • Conivaptan

 • Copanlisib

 • Crizotinib

 • Cyclophosphamide

 • Cyclosporine

 • Cyproterone acetate

 • Dabrafenib

 • Dacomitinib

 • Dasatinib

 • Daunorubicin

 • Delafloxacin

 • Demeclocycline

 • Deoxycholic acid

 • Desogestrel

 • Dexamethasone

 • Dexamethasone acetate

 • Diclofenac

 • Dicoumarol

 • Dienogest

 • Diethylstilbestrol

 • Digitoxin

 • Digoxin

 • Dihydroergocornine

 • Dihydroergocristine

 • Dihydroergotamine

 • Dihydrostreptomycin

 • Dipyridamole

 • Disulfiram

 • Docetaxel

 • Dofetilide

 • Doxacurium

 • Doxazosin

 • Doxorubicin

 • Doxycycline

 • Dronedarone

 • Drospirenone

 • Duvelisib

 • Ebastine

 • Efavirenz

 • Elexacaftor

 • Enasidenib

 • Enoxacin

 • Entrectinib

 • Eravacycline


Maudhi madogo ya Flucloxacillin


Maudhi ya mara kwa mara


 • Hisia za kuugua

 • Kichefucehfu na kutapika

 • Kuhara

 • Hisia za kuvimbiwa

 • Tumbo kujaa gesi


Maudhi ya nadra sana


 • Eosinophilia

 • Erythema multiforme

 • Kukereketa kwa koo

 • Kuoza kwa ngozi

 • Kushindwa kupumua

 • Kuungua kwenye koo la chakula

 • Kuvimba midomo

 • Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili

 • Magonjwa ya ngozi kama yutikaria na papula

 • Manjano

 • Maumivu ya maungo ya mwili

 • Maumivu ya mdomo

 • Maumivu ya misuli

 • Muwasho ukeni na kutokwa na uchafu mweupe

 • Muwasho wa ngozi

 • Mzio wa anafailaksia

 • Oesophagitis

 • Syndromu ya Stevens-Johnson

 • Upungufu wa chembe nyeupe za damu

 • Upungufu wa chembe sahani za damu

 • Upungufu wa damu kutokana na uhalibifu wa chembe nyekundu za damu

 • Nephratiz


Je endapo utasahau dozi ya Flucloxacillin ufanyaje ?


Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa kunyw adozi nyingine umefika ambapo utapaswa kusubilia muda ufike ndipo utumie dozi hiyo na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.


Uhifadhi ya Flucloxacillin


Hifadhi dawa yako na kuiepusha na joto la mazingira. Usiweke kwenye friji au sehemu yenye mwanga wa jua au joto ili kuepuka kuharibu dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

4 Juni 2022 20:33:08

Rejea za mada hii:-

1. Science Direct. Beta Lactam Antibiotic. https://www.sciencedirect.com/topics/pharmacology-toxicology-and-pharmaceutical-science/beta-lactam-antibiotic#. Imechukuliwa 03.06.2022

2. Flucloxacillin. https://www.medicines.org.uk/emc/product/545/smpc#gref. Imechukuliwa 03.06.2022

3. Barza M: Antimicrobial spectrum, pharmacology and therapeutic use of antibiotics. Part 2: penicillins. Am J Hosp Pharm. 1977 Jan;34(1):57-67.

4. Dekker SJ, Dohmen F, Vermeulen NPE, Commandeur JNM: Characterization of kinetics of human cytochrome P450s involved in bioactivation of flucloxacillin: inhibition of CYP3A-catalysed hydroxylation by sulfaphenazole. Br J Pharmacol. 2019 Feb;176(3):466-477. doi: 10.1111/bph.14548. Epub 2018 Dec 26.

5. Huwyler J, Wright MB, Gutmann H, Drewe J: Induction of cytochrome P450 3A4 and P-glycoprotein by the isoxazolyl-penicillin antibiotic flucloxacillin. Curr Drug Metab. 2006 Feb;7(2):119-26.

6. Imming P, Sinning C, Meyer A: Drugs, their targets and the nature and number of drug targets. Nat Rev Drug Discov. 2006 Oct;5(10):821-34.

7. Lacey RW: Mechanisms of resistance to beta-lactam antibiotics in Staphylococcus aureus. Scand J Infect Dis Suppl. 1984;42:64-71.

8. Mainardi JL, Villet R, Bugg TD, Mayer C, Arthur M: Evolution of peptidoglycan biosynthesis under the selective pressure of antibiotics in Gram-positive bacteria. FEMS Microbiol Rev. 2008 Mar;32(2):386-408. doi: 10.1111/j.1574-6976.2007.00097.x. Epub 2008 Feb 11.

9. Overington JP, Al-Lazikani B, Hopkins AL: How many drug targets are there? Nat Rev Drug Discov. 2006 Dec;5(12):993-6.

10. Pedersen JM, Matsson P, Bergstrom CA, Hoogstraate J, Noren A, LeCluyse EL, Artursson P: Early identification of clinically relevant drug interactions with the human bile salt export pump (BSEP/ABCB11). Toxicol Sci. 2013 Dec;136(2):328-43. doi: 10.1093/toxsci/kft197. Epub 2013 Sep 6.
bottom of page