top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Septemba 2021 20:09:57

Dawa Fluticasone

Dawa Fluticasone

Ni dawa aina jamii ya corticosteroid maarufu kwa jina jingine la Clarispray au Flonase. Dawa hii ni moja ya dawa zinazotumika kunyunyiza ndani ya pua.


Uzito na fomu ya Fluticasone


Hupatikana katika fomu ya maji yanayotumika kwa kunyunyiza puani

Dawa huwa na uzito wa mikrogramu


 • 27.5mcg/ kwa mnyunyizo mmoja

 • 50mcg/kwa mnyunyizo mmoja

 • 93 mcg/ kwa mnyunyizo mmoja


Namna Fluticasone inavyoweza kufanya kazi


Dawa hii hufanya kazi katika mfumo wa kinga ya mwili kwa kupunguza uvimbe, wekundu na kuwashwa kutokana na mwitikio wa kinga za mwili kwenye kiamsha mzio, kazi hii hufanikiwa kwa kusinyaza mishipa ya damu kwenye eneo lililonyunyiziwa dawa.


Matumizi ya Fluticasone


 • Hutumika kutibu mafua yanayochuruzika kutokana na mzio

 • Hutumika kwa kutibu wagonjwa wa nyama za pua

 • Hutibu eczema

 • Soriasis

 • Harara kwenye ngozi kutokana na mzio


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Fluticasone


Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Fluticasone au dawa zingine jamii ya corticosteroid


Utoaji taka wa Fluticasone


Chini ya asilimia 2 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia zinazobaki hutolewa kwa njia ya kinyesi.


Namna ya kutumia dawa


 • Tikisa taratibu chupa ya dawa

 • Jaribu kunyunyiza kwanza kama ni chupa mpya au kama hunyanyunyiza kwa muda wa wiki au zadi

 • Unapotumia, elekeza mbali na macho

 • Peng'a pua kwanza kabla ya kunyunyiza dawa puani


Endapo utatumia dozi kubwa kuliko kawaida


Kutumia dozi kubw akuliko kawaida mara nyingi hakutokei kwa sababu dawa ni ya kunyunyiza puani. Hata hivyo ikitokea umekunywa kwa bahati mbaya, wasiliana na huduma za dharura kwa msaada zaidi


Tahadhari kwa matumizi ya fluticasone


Huweza kuficha maambukizi makali puani ikiwa pamoja na maambukizi ya fangasi Huweza kuongeza ukali wa maambukizi ya virusi kwenye pua Huchelewesha kupona kwa vidonda vya puani kutokana na maambukizi, upasuaji n.k


Mwingiliano wa Fluticasone na dawa zingine


 • Dawa zenye mwingiliano mkali za kuzuia dawa hii kutumika pamoja na dawa zingine; Atazanavir

 • Clarithromycin

 • Conivaptan

 • Darunavir

 • Fosamprenavir

 • Imatinib

 • Indinavir

 • Isoniazid

 • Itraconazole

 • Ketoconazole

 • Kopinavir

 • Nefazodone

 • Nelfinavir

 • Nicardipine

 • Posaconazole

 • Quinidine

 • Ritonavir

 • Saquinavir

 • Tipranavir

 • Voriconazole

Fluticasone ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu na mtaalamu wa afya:


 • Fedratinib

 • Letermovir

 • Ribociclib

 • Ribociclib

 • Rucaparib

 • Stiripentol

 • Tazemetostat


Matumizi ya Fluticasone kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti yeyote inayoonyesha kuwa kuna madhara endapo itatumika kwa mama mjamzito. Tafiti zinaonyesha dawa hii hupita kwenye kondo kwenda kwa mtoto kwa wanyama kama panya na paka.


Matumizi ya Fluticasone kwa mama anayenyonyesha


Hakuna tafiti zinazoonyesha kuwa dawa hii inapita kwenye maziwa ya mama, madhara yake kwa mtoto anayenyonya maziwa ya mama.


Maudhi madogo ya Fluticasone


 • Kuongezeka hali ya kutokwa damu puani

 • Kutokwa na damu puani

 • Kuchuruzika kw mafua

 • Hisia za

 • Wekundu na mabaka kwenye koo au puani

 • Homa

 • Kutetemeka

 • Maumivu ya mwili

 • Maumivu ya macho

 • Uono hafifu

 • Kutopana kwa kidonda

 • Ongezeko la uchovu

 • Udhaifu wa misuli

 • Maumivu ya kichwa

 • Kichefuchefu

 • Kutapika

 • Kikohozi

 • Koo chungu

 • Hisia za kuungua au kuwashwa ndani ya pua


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?


Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:25

Rejea za mada hii:-

1. MedlinePlus.Fluticasone. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a695002. Imechukuliwa 1/9/2021

2. WebMd.Fluticasone. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-77986-1875/fluticasone-propionate-nasal/fluticasone-breath-activated-spray-nasal/details , Imechukuliwa 1/9/2021

3. Health Line.Fluticasone. https://www.healthline.com/health/fluticasone-side-effects , Imechukuliwa 1/9/2021

4. Mayoclinic.Fluticasone. https://www.mayoclinic.org/drugs-supplements/fluticasone-nasal-route/side-effects/drg-20070965?p=1, Imechukuliwa 1/9/2021

5. NCBI.Fluticasone. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK542161/ , Imechukuliwa 1/9/2021

6. Flucatison. https://www.rxlist.com/flonase-drug.htm#. Imechukuliwa 1/9/2021
bottom of page