Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
14 Septemba 2021 07:48:39
Dawa Fosfomycin
Fosfomycin ni moja kati ya antibiotic inayotumika kuzuia ukuaji na kuua bakteria wanaosababisha maambukizi kwenye kibofu cha mkojo.
Majina ya kibiashara
Majina mengine ya Fosfomycin ni;
Monurol
Fosfomycin ipo kundi gani la dawa?
Fosfomycin ni Antibiotiki iliyo katika kundi la antibiotiki zingine. Dawa hii haifanani na dawa zingine za antibayotiki ndo maana imewekwa kwenye kundi hili
Fomu na uzito wa fosfomycin
Dawa hii ipo katika fomu ya Unga na uzito ufuatao;
Unga kwa jaili ya sindano wenye gramu 3 kwa pakiti
Fosfomycin hutibu nini?
Fosfomycin hutibu magonjwa yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii haswa katika njia ya mkojo, mfano wake ni; Hutumika kutibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo ( maambukizi sugu, cystitis) Hutumika kutibu maambukizi kwenye tezi dume
Bakteria wanaodhuriwa na Fosfomycin
Escherichia coli
Staphylococcus aureus
Enterococcus species
Enterobacteriaceae
Klebsiella pneumoniae
Pseudomonas aeruginosa
Namna Fosfomycin inavyoweza kufanya kazi
Hufanya kazi ya kuzuia ukuaji na kuua bakteria wanaosababisha maambukizi kwenye kibofu cha mkojo kwa kuzuia utengenezwaji wa ukuta wa seli.
Ufozwaji na utolewaji taka mwilini wa fosfomycin
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri na haraka kwenye utumbo mdogo. Asilimia 38% hutolewa kwenye mkojo bila kufanyiwa umetaboli na asilimia 18 hutolewa kwa njia ya kinyesi. Kiasi kilichobaki hufanyiwa umetaboli na ini
Mwingiliano wa Fosfomycin na chakula
Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula ama akiwa bado hajapata chakula. Asilimia 37 ya daw ahufyonzwa kama isipotumiwa na chakula na asilimia 30 ya dawa hufyonzwa kama ikitumiwa na chakula. Hii inaonyesha kuwa kama ikitumiwa na chakula, ufyonzwaji wake hupungua kidogo.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Fosfomycin
Wagonjwa wenye mzio wa Fosfomycin.
Dawa zenye muingiliano na Fosfomycin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Fosfomycin;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya kipindupinfu
Chanjo hai ya typhoid
Dawa zinazoweza kutumika na Fosfomycin chini ya uangalizi;
Bazedoxifene/conjugated estrogens
conjugated estrogens
digoxin
estradiol
estrogens conjugated synthetic
estropipate
mestranol
metoclopramide ya kuweka puani
sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Fosfomycin;
Balsalazide
Biotin
Metoclopramide
Pantothenic acid
Pyridoxine
Pyridoxine (antidote)
Thiamine
Matumizi ya Fosfomycin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Fosfomycin kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha dawa hii inaweza kutumiwa na mama mjamzito.
Matumizi ya Fosfomycin kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inatolewa mwilini kwa njia ya maziwa hivyo haishauriwi kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Fosfomycin;
Kizunguzungu
Mwili kupata vipele
Kusinzia mara kwa mara
Kuharisha
Mapigo ya moyo kubadirika
Kichefuchefu
Kutapika
Anorexia
Maumivu ya tumbo
Kichwa kuuma
Kupata homa
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-