Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Septemba 2021 11:10:32
Dawa Imipenem
Imipenem ni moja kati ya antibiotiki jamii ya carbapenems yenye uwanja mpana wa kudhuru bakteria inayotumika sana ikiwa imeunganika na cilastatin ili kuongeza muda wa ufanyaji kazi wake na kuzuia madhara yake kwenye figo. Dawa hii ina uwezo wa kudhuru bakteria wa gramu hasi, chanya na anaerobi na hivyo kutibu maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo, via vya uzazi, mapafu, tumbo, damu na moyo.
Majina mengine ya Imipenem
Majina mengine ya Imipenem ni; Primaxin Recarbrio
Dawa zilizo kundi moja na Imipenem
Dawa zilizo kundi moja na Imipenem ni ;
Doripenem
Ertapenem
Meropenem
Fomu ya dawa ya Imipenem
Dawa imipenem hutumika pamoja na cilastine na hupatikana kwenye fomu ya unga kwa ajiri ya sindano wenye uzito wa;
250mg/250mg
500mg/500mg
Imipenem hutibu nini?
Imipenem hutumika ikiwa imeunganika na cilastatin kwa ajili ya matibabu ya;
Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Maambukizi kwenye ngozi
Maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke
Maambukizi ndani ya tumbo
Maambukizi ya pseudomonas
Namna imipenem inavyofanya kazi
Imipenem hufanya kazi yake ya kudhuru bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa ukuta wa seli ya bakteria. Huweza kuzuia ujenzi wa kuta za bakteria jamii ya gramu chanya na hasi. Uzuiaji huo kwa bakteria wa gramu hasi hufanyika kwa kujishikiza kwenye protini muhimu ya bakteria inayotumiwana penicillin. Kwa kujishikiza kwenye protini hii hupelekea kuzuia utengenezwaji wa protini zinazotengeneza vijenzi vya ukuta wa seli ya bakteria na hivyo bakteria hufa.
Vimelea wanaodhuriwa na Imipenem
Pseudomonas aeruginosa
Streptococcus agalactiae
Haemophilus influenzae
Escherichia coli
Staphylococcus aureus
Enterococcus faecalis
Staphylococcus epidermidis
Serratia marcescens
Proteus vulgaris
Providencia rettgeri
Morganella morganii
Enterobacter cloacae
Klebsiella pneumoniae
Haemophilus parainfluenzae
Citrobacter freundii
Bacteroides thetaiotaomicron
Klebsiella aerogenes
Bacteroides caccae
Bacteroides ovatus
Bacteroides stercoris
Bacteroides uniformis
Bacteroides vulgatus
Fusobacterium nucleatum
Parabacteroides distasonis
Acinetobacter spp.
Enterobacter spp.
Klebsiella spp.
Citrobacter spp.
Proteus spp.
Bifidobacterium spp.
Clostridium spp.
Eubacterium spp.
Peptococcus spp.
Peptostreptococcus spp.
Propionibacterium spp.
Bacteroides spp.
Fusobacterium spp.
Serratia spp.
Gardnerella vaginalis
Mwingiliano wa Imipenem na chakula
Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula ama akiwa bado hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Imipenem
Wagonjwa wenye mzio wa Imipenem Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Carbapenems
Ufyonzwaji na utoaji taka wa Imipenem mwilini
Asilimia 89 ya dawa hufyonzwa kwenye misuli na kuingia kwenye damu, dawa hii kama itatumika kwa kunywa, ufyozwaji wake huwa mdogo na hii ndio maana inapatikana kwa kuchoma sindano ya misuli au mishipa ya damu. Mara baada ya kuingia kwneye damu asilimia sabini (70%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiasi kilichobaki hufanyiwa umetobaoli na ini.
Dawa zenye muingiliano na Imipenem
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Imipenem;
Chanjo hai ya BCG
Cholera vaccine
Divalproex sodium
Ganciclovir
Probenecid
Valacyclovir
Valproic acid
Dawa zinazoweza kutumika na Imipenem chini ya uangalizi;
Chanjo hai ya BCG
Cyclosporine
Sodium picosulfate
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Chanjo hai ya Typhoid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Imipenem;
Tafiti zinaonesha hakuna dawa yenye mwingiliano mdogo na imipenem
Matumizi ya Imipenem kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Imipenem kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha dawa hii inaleta madhara kwa mtoto hivyo haishauriwi kwa mama mjamzito kutumia dawa hii.
Matumizi ya Imipenem mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha kuwa Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama anayenyosha na haijaonesha kuleta madhara kwa mtoto pia madhara katika uzalishwaji wa maziwa hivyo mama anaweza kufanya kitu kimoja kati ya kutumia dawa na kunyonyesha.
Maudhi ya Imipenem
Upungufu wa damu
Ongezeko la eosinophilia
Ongezeko la muda wa prothrombin
Leukopenia
Kupungua kwa ufanyajikazi wa uboho
Upungufu wa chembe sahani za damu
Mshituko wa moyo
Mapigo ya moyo kwenda mbio
Michomo kwenye mishipa ya damu
Dehedege
Huzuniko
Kizunguzungu
Hisia za mazingira kuzunguka
Kichefuchefu
Kutapika
Maambukizi ya fangasi mdomoni
Kolaitiz ya uongo
Kubadilika radha ya chakula
Kupungua kwa ufanyaji kazi wa
Kuongezeka kwa vmeng’enya vya ini
Kuvia damu kwenye mapafu
Kuferi kwa mapafu
Kupumua kwa kina
Kubana kwa pumzi
Muwasho
Kuvimba
Harara kwenye ngozi
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu kutumia dozi kwa wakati sahihi.Kama umesahau kutumia dozi yako muulize daktari au mfamasia wako muda sahihi wa kupata dozi nyingine.Usitumia dozi mbili kwa wakati mmoja ili kufidia dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-