Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Septemba 2021, 09:53:16

Dawa Imipenem/cilastatin
Imipenem/cilastatin ni moja ya antibiotic jamii ya Carbapenem inayotumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii ikiwa pamoja na bakteria gramu hasi, gramu chanya, anaerobi na walio sugu kwenye dawa zingine.
Majina mengine ya Imipenem
Majina mengine ya Imipenem/cilastatin ni; Cilastatin Primaxin
Dawa zilizo kundi moja na Imipenem/cilastatin
Dawa zilizo kundi moja na Imipenem/cilastatin; Doripenem Meropenem
Fomu ya dawa na uzito wa Imipenem/cilastatin
Imipenem/cilastine ipo katika fomu ya unga kwa ajiri ya sindano wenye uzito wa;
250mg/250mg 500mg/500mg
Imipenem/cilastatin hutibu nini?
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Hutumika kutibu maambukizi kwenye ngozi
Hutumika kutibu maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke (PID)
Hutumika kutibu maambukizi ndani ya tumbo
Hutumika kutibu maambukizi ya pseudomonas
Vimelea wanaodhuriwa na Imipenem
Pseudomonas aeruginosa
Streptococcus agalactiae
Haemophilus influenzae
Escherichia coli
Staphylococcus aureus
Enterococcus faecalis
Staphylococcus epidermidis
Serratia marcescens
Proteus vulgaris
Providencia rettgeri
Morganella morganii
Enterobacter cloacae
Klebsiella pneumoniae
Haemophilus parainfluenzae
Citrobacter freundii
Bacteroides thetaiotaomicron
Klebsiella aerogenes
Bacteroides caccae
Bacteroides ovatus
Bacteroides stercoris
Bacteroides uniformis
Bacteroides vulgatus
Fusobacterium nucleatum
Parabacteroides distasonis
Acinetobacter spp.
Enterobacter spp.
Klebsiella spp.
Citrobacter spp.
Proteus spp.
Bifidobacterium spp.
Clostridium spp.
Eubacterium spp.
Peptococcus spp.
Peptostreptococcus spp.
Propionibacterium spp.
Bacteroides spp.
Fusobacterium spp.
Serratia spp.
Gardnerella vaginalis
Namna Imipenem inavyofanya kazi
Imipenem/cilastatin hufanya kazi yake ya kudhuru bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa ukuta wa seli ya bakteria. Huweza kuzuia ujenzi wa kuta za bakteria jamii ya gramu chanya na hasi. Uzuiaji huo kwa bakteria wa gramu hasi hufanyika kwa kujishikiza kwenye protini muhimu ya bakteria inayotumiwana penicillin. Kwa kujishikiza kwenye protini hii hupelekea kuzuia utengenezwaji wa protini zinazotengeneza vijenzi vya ukuta wa seli ya bakteria na hivyo bakteria hufa.
Mwingiliano wa Imipenem/cilastatin na chakula
Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula ama akiwa bado hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Imipenem
Wagonjwa wenye mzio wa Imipenem Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Carbapenems
ufyonzwaji na Utoaji taka wa Imipenem mwilini
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye misuli (asilimi 89 huingia kwenye damu) na mishipa, hata hivyo dawa hii ikitumika kwa kunywa ufyonzwaji wake huwa mdogo na ndio maana hupatikana kwenye fomu ya unga kwa ajili ya kuchoma tu. Asilimia sabini (70%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiasi kilichobaki
Dawa zenye muingiliano na Imipenem/cilastatin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Imipenem/cilastatin;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo ya kipindupindu
Divalproex sodium
Ganciclovir
Probenecid
Valacyclovir
Valproic acid
Dawa zinazoweza kutumika na Imipenem/cilastatin chini ya uangalizi;
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya typhoid
Cyclosporine
Sodium picosulfate
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Imipenem/cilastatin
Tafiti zinaonesha hakuna dawa yenye mwingiliano mdogo na imipenem
Dawa zenye muingiliano mdogo na Imipenem/cilastatin
Mpaka sasa hakuna dawa zilizopatikana kuwa na mwingiliano mdogo na imipenem
Matumizi ya Imipenem/cilastatin kwa mjamzito na mama anayenyonyesha
Matumizi ya Imipenem kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha dawa hii inaleta madhara kwa mtoto hivyo haishauriwi kwa mama mjamzito kutumia dawa hii.
Matumizi ya Imipenem/cilastatin mama anayenyonyesha Tafiti zinaonesha kuwa Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama anayenyosha na haijaonesha kuleta madhara kwa mtoto pia madhara katika uzalishwaji wa maziwa hivyo mama anaweza kufanya kitu kimoja kati ya kutumia dawa na kunyonyesha.
Maudhi ya Imipenem/cilastatin
• Degedege
• Kuchanganyikiwa
• Kutapika
• hofu na mfadhaiko
• Mzio
• Kuharisha
• Maumivu ya tumbo
• Upungufu wa damu
• Kizunguzungu
• Maumivu ya kichwa
• Kuhisi mapigo ya moyo
• Homa
• Kichefuchefu
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako ya Imipenem/cilastatin?
Ni muhimu kutumia dozi kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pele utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia ambapo utakakiwa subiria muda ufike ndipo unywe dozi inayofuata. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-