Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
1 Juni 2022 16:32:06
Dawa levamisole
Ni dawa ya kutengenezwa kiwandani iliyo na asili ya imidazothiazole na jamii ya anthelmintics. Levamisole ilikuwa inatumika kutibu maambukizi ya minyoo, bakteria na virusi kwa binadamu na wanyama.
Kutokana na uwezo wake wa kuingilia mfumo wa kinga, dawa hii iliwahi kutumika pia katika matibabu ya magonjwa ya kujishambulia kwa mfumo wa kinga na kama tiba nyongeza katika matibabu ya saratani.
Kwa sababu ya madhara yake ya kusababisha upungufu mkali wa chembe nyeupe za damu, dawa hii iliondolewa sokoni na FDA mwaka 2000 na hivyo haitumiki kwa binadamu.
Majina mengine ya levamisole
Levamisole huwa na majina mengine kama Ergamisol (Janssen) / Ketrax (AstraZeneca)
Uzito na fomu ya levamisole
Levamisole hupatikana katika fomu ya kidonge
Milligrammu 50
Milligrammu 100
Dawa kundi moja na levamisole
Dawa zingine zilizo kundi moja na levammisole yaani anthelminthic ni;
Albendazole
Thiabendazole
Ivermectin
Praziquantel
Diethylcarbamazine
Triclabendazole
Moxidectin
Pyrantel pamoate
Levamisole hutibu nini?:
Hutibu maambukizi ya minyoo jamii ya Enteroblus Vermicularis
Hutibu maambukizi yanayosababishwa na minyoo jamii ya Ascaris Lumbricodes
Hutibu maambukizi ya minyoo yanayoitwa trichuris trichiura
Hutibu ukoma
Hutibu magonjwa ya madhaifu ya kolajeni katika mishipa ya damu
Hutibu magnjwa ya ngozi kutokana na shambulio la kinga ya mwili
Hutumika na dawa zingine kutibu saratani kama saratani ya utumbo
Hutibu vidonda vya kinywa
Hutibu ugonjwa wa nephrotic sindromu
Namna levamisole inavyoweza kufanya kazi
Levamisole hufanya kazi kwa kuzuia ufanyaji kazi wa misuli ya minyoo na hivyo kushindwa kujamiana na kufa.
Haifahamiki namna gani dawa hii hufanya kazi kama dawa ya saratani inapochanganywa na fluorouracil.
Vimelea wanaodhuriwa na levamisole
Echinococcus
Ancylostoma
Trichostrongylus
Enteroblus
Trichuris Trichiura
Wagonjwa wasiopaswa kutumia levamisole
Levamisole haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii. Tahadhari inapaswa kuchukuliwa pia kwa wagonjwa wenye Baridi yabisi, sindromu ya Sjogren, kifafa na magonjwa ya ini
Ufyonzwaji wa levamisole
Zaidi ya asilimia 80 ya Levamisole hufyonzwa haraka na kuingia kwenye damu ndani ya masaa 2 baada ya kunywa.
Umetaboli
Dawa hii hufanyiwa umetaboli kwenye ini
Matumizi ya levamisole kwa mama mjamzito
Hakuna tafiti za kutosha kwa binadamu kuonyesha madhara yake mbali na kusababisha upungufu wa chembe nyeupe za damu. Hata hivyo tafiti za wanyama zinaonyesha dawa inaweza kuwa sumu kwa kichanga. Matumizi ya dawa hii yanapswa kuzingatia faida inayopatikana dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Matumizi ya levamisole kwa mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti za kutosha kuonyesha madhara ya dawa hii kwa mtoto wa mama anayetumia dawa hii. Matumizi ya dawa yanapaswa kuzinatia faida na madhara yanayoweza kujitokeza.
Mwingiliano wa levamisole na dawa zingine
Dawa zenye mwingiliano na levamisole ni:
Capecitabine
Doxifluridine
Fluorouracil
Tegafur
Warfarin
Ivermectin
Albdendazole
Vitu vingine vyenye mwingiliano na levamisole
Levamisole pia inaweza kuingiliana na pombe, sigara na baadhi ya vyakula. Ongea na daktari wako kuhusu matumizi ya dawa hii na vitu vingine kama yanafaa.
Maudhi madogo ya levamisole
Maudhi ya mara kwa mara
Homa
Kutetemeka
Kuhisi bughudha mwilini
Kuharisha
Ladha ya umetali
Kichefuchefu
Maudhi ya mara chache
Wasiwasi
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Msongo wa mawazo
Harara kwenye ngozi
Kuwashwa
Kukosa usingizi
Uchovu mkali usio wa kawaida
Ndoto za kutisha
Kutapika
Maumivu ya misuli
Maumivu ya maungio ya mwili
Maudhi ya nadra sana
Kuchanganyikiwa
Uono hafifu( kuona ukungu)
Kupoteza fahamu
Kuvimba mwa midomo
Ganzi na hisia za kuchomachoma kwenye uso, mikono na miguu
Hisia za kutishiwa au kuhukumiwa
Kuvimba kwa mashavu
Kutetemeka mwili au mikono
Kushindwa tembea
Kushindwa dhibiti mjongeo wa mikono na miguu
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Kama umesahau kutumia dozi yako, acha dozi uliyosahau na subiri muda wa kunywa dozi nyingine kisha utumie kama ulivyoandikiwa na daktari wako. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.
Uhifadhi ya levamisole
Hifadhi dawa yako kwenye kikopo cha kutunzia dawa kilichokuja na dawa na katika joto la mazingira. Usiweke kwenye friji au sehemu yenye mwanga wa jua au joto ili kuepuka kuiharibu dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Juni 2022 16:41:04
Rejea za mada hii:-