Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Septemba 2021, 20:04:51

Dawa Levofloxacin
Levofloxacin ni moja ya antibayotiki jamii ya fluoroquinolone inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa kwenye njia ya hewa, ngozi, mfumo wa mkojo, tezi dume na waliojianika kwenye kimeta na plague.
Majina mengine ya Levofloxacin
Majina mengine ya Levofloxacin ni;
Levaquin
Quinsair
Dawa zilizo kundi moja na Levofloxacin
Dawa zilizo kundi moja na Levofloxacin ni ;
Ciprofloxacin
Gemifloxacin
Moxifloxacin
Ofloxacin
Fomu ya dawa ya Levofloxacin
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Solution kwa ajiri ya sindano
Solution kwa ajiri ya kunywa
Vidonge
Fomu ya dawa ya Levofloxacin
Dawa hii ipo katika fomu ya kimiminika kwa ajiri ya sindano, Solution kwa ajiri ya kunywa na Vidonge
Uzito wa dawa ya Levofloxacin
Levofloxacin ina uzito ufuatao;
Kimiminika kwa ajiri ya sindano
250mg/50ml
500mg/100ml
750mg/150ml
Solution kwa ajiri ya kunywa
25mg/ml
Vidonge
250mg
500mg
750mg
Levofloxacin hutibu nini?
Levofloxacin hutibu magonjwa yanyotokana na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii kwenye maeneo mbalimbali mfano;
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Hutumika kutibu sinusitis kali ya bakteria
Hutumika kutibu maambukizi kwenye ngozi
Hutumika kutibu Nimonia
Hutumika kutibu maambukizi ya bakteria kwenye damu
Hutumika kutibu Inhalation kimeta
Hutumika kutibu maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Hutumika kutibu vimeta
Hutumika kutibu maambukizi kwenye tezi dume
Hutumika kutibu maambukizi kwenye epididymis
Namna Levofloxacin inavyoweza kufanya kazi
Uwezo wa kitiba wa levofloxacin hutokana na uwezo wake wa kuzuia ufanyajikaziwa kimeng’enya topoisomerase II (DNA gyrase) na topoisomerase IV. DNA gyrase ni kimeng’enya muhimu katika utengenezaji nakala, unukuu na kurekebisha madhaifu ya DNA ya bakteria. Topoisomerase IV ni kimeng’enya kinachofahamika kufanya kazi ya kugawanya chromosome ya DNA wakati wa kutengenezwa nakala za bakteria.
Vimelea wanaodhuriwa na Levofloxacin
Chlamydia pneumonia
Enterococcus faecalis
Enterobacter cloacae
Escherichia coli
Haemophilus influenza
Haemophilus parainfluenzae
Klebsiella pneumonia
Legionella pneumophila
Morganella morganii
Moraxella catarrhalis
Proteus mirabilis
Providencia spp
Pseudomonas aeruginosa
Serratia spp
Staphylococcus aureus
Streptococcus spp
Ufozwaji wa levofloxacin
Asilimia 99 ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu, kutokana na kufyonzwa vema kwenye mfumo wa chakula, dawa hii hutumiwa kwa njia ya kunywa na kuchoma kama sindano.
Mwingiliano wa Levofloxacin na chakula
Dawa hii ni nzuri ikitumika na chakula kwani chakula husaidia ufozwaji wa dawa.
Utoaji taka wa Levofloxacin mwilini
Asilimia themanini na saba (87%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia nne (4%) kwa njia ya haja kubwa.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Levofloxacin
Wagonjwa wenye mzio wa levofloxacin
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Fluoroquinolone
Dawa zenye muingiliano na Levofloxacim
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Levofloxacim;
Artemether
Chanjo hai yaBCG
Chanjo hai ya typhoid
Chanjo hai ya kipindupindu
Disopyramide
Ferrous gluconate
Ferrous sulfate
Hydroxychloroquine sulfate
Methyl aminolevulinate
Procainamide
Quinidine
Ribociclib
Rose hips
Saquinavir
Sodium bicarbonate
Dawa zinazoweza kutumika na Levofloxacin chini ya uangalizi;
Artemether/lumefantrine
Bedaquiline
Betamethasone
Chloroquine
Clarithromycin
Dexamethasone
Diclofenac
Digoxin
Epinephrine
Erythromycin base
Fluconazole
Glipizid
Hydrocortisone
Haloperidol
Ibuprofen
Indomethacin
Insulin
Ketoconazole
Magnesium suppliments
Mefenamic acid
Meloxicam
Mifeprostol
Metformin
Moxifloxacin
Ofloxacin
Methadone
Piroxicam
Prednisolone
Quinine
Promethazine
Warfalin
Zinc
Dawa zenye muingiliano mdogo na Levofloxacin;
Aceclofenac
Acemetacin
Azithromycin
Balsalazide
Chlordiazepoxide
Clonazepam
Flurazepam
Foscarnet
Green tea
Isotretinoin
Itraconazole
Loprazolam
Lorazepam
Lormetazepam
Lornoxicam
Midazolam
Oxazepam
Pantothenic acid
Parecoxib
Pazopanib
Pyridoxine
Temazepam
Thiamine
Tolfenamic acid
Matumizi ya Levofloxacin kwa mama mjamzito
Tafiti zilizofanyika hazijaonesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyeko tumboni hivyo haishauriwi kutumiwa na mama mjamzito.
Matumizi ya Levofloxacin mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama lakini hazijaonesha madhara ya dawa kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo mama anashauriwa asinyonyeshe wakati anatumia dawa hii.
Maudhi ya Levofloxacin
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Kuharisha
Kukosa usingizi
Kupata choo kigumu
Kizunguzungu
Mvurugiko wa tumbo
Vipele
Kutapika
Kifua kuuma
Kushindwa kupumua
Mwili kuvimba
Mwili kuchoka
Maambukizi ya fangasi
Maumivu
Ngozi kuwasha
Maambukizi ukeni
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Endapo utasahau kutumia dozi yako muulize daktari au mfamasia wako muda sahihi wa kutumia dozi mpya. Usitumie dozi mbili ili kufidia dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-