top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

18 Septemba 2021 19:10:38

Dawa Linezolid

Dawa Linezolid

Linezolid ni moja kati ya antibiotik jamii ya oxazolidinone inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria jamii ya gramu chanya wanaodhuriwa na dawa hii.


Majina mengine ya Linezolid


Majina mengine ya Linezolid ni;

  • Zyvox

  • Zyvoxam

Dawa kundi moja na Linezolid

Dawa zilizo kundi moja na Linezolid ni; Tedizolid


Fomu na uzito wa Linezolid


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Kimiminika kwaajiri ya sindano

  • Kimiminika kwaajiri ya kunywa

  • Vidonge

Uzito wa dawa ya Linezolid


Linezolid ina uzito ufuatao;


  • Kimiminika kwaajiri ya sindano huwa na uzito wa 2mg/ml (100ml) na 300ml infusheni)


  • Kimiminika kwaajiri ya kunywa huw ana uzito wa 100mg/5ml


  • Kidonge huwa na uzito wa 600mg

Linezolid hutibu nini?


  • Inatumika kutibu maambukizi ya bakteria Enterococcal wenye usugu kwenye Vancomycin

  • Inatumika kutibu maambukizi kwenye ngozi

  • Inatumika kutibu Nimonia ya kuambukizwa kwenye jamii

  • Inatumika kutibu bakteria staphylococcal Aereus wenye usugu kwenye Methicilin

  • Inatumika kutibu bakteria staphylococcal Aereus wasio na usugu kwenye Methicilin

  • Hutibu nimoni ya kuambukizwa hospitali


Namna Linezolid inavyoweza kufanya kazi


Linezolid hufanya kazi kwa kuingilia utoaji nakala za protini ya bakteria. Hufanya kazi hiyo kwa kujishikiza kwenye RNA ya bakteria na kufanya ishindwe kujizalia. Kubadilika kwa rRNA ya bakteria inaweza kusababisha usugu wa bakteria kwenye linezolid na kufanya kushindwa akutibu vimelea vya Enterococcus faecium na Staphylococcus aureus.


Vimelea wanaodhuriwa na Linezolid


  • Enterococcus faecium

  • Staphylococcus aureus

  • Streptococcus spp


Ufozwaji na mwingiliano wa Linezolid na chakula


Mara baada ya kunywa, dawa hii hufyonzwa vema na asilimia 100 hupatikana kufanya kazi katika tiba. Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula ama akiwa bado hajapata chakula.


Utoaji taka wa Linezolid mwilini


Asilimia themanini ya (80%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia tisa (9%) kwa njia ya haja kubwa.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Linezolid


Wagonjwa wenye mzio wa Linezolid. Wagonjwa wenye mzio wa dawa nyingine jamii ya Oxazolidinones.


Dawa zenye mwingiliano na Linezolid


Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Linezolid;

  • Amitriptyline

  • Belladonna and opium

  • Benzhydrocodone/acetaminophen

  • Chanjo hai ya BCG

  • Chanjo hai ya typhoid

  • Cholera vaccine

  • Epinephrine racemic

  • Ergotamine

  • Hydrocodone

  • Isoniazid

  • Lithium

  • Lorcaserin

  • Maprotiline

  • Meperidine

  • Metaproterenol

  • Methadone

  • Methylene blue

  • Metoclopramide ya kuweka puani

  • Milnacipran

  • Mirtazapine

  • Morphine

  • Nalbuphine

  • Nefazodone

  • Nortriptyline

  • Opium tincture

  • Oxycodone

  • Oxymorphone

  • Papaveretum

  • Paroxetine

  • Pentazocine

  • Phenelzine

  • Pirbuterol

  • Procarbazine

  • Sufentanil

  • Sufentanil sl

  • Sumatriptan

  • Sumatriptan ya kuweka puani

  • Tapentadol

  • Terbutaline

  • Tramadol

  • Tranylcypromine

  • Trazodone

  • Trimipramine

  • Valbenazine

  • Venlafaxine

  • Vilazodone


Dawa zinazoweza kutumika na Linezolid chini ya uangalizi;

  • Amifampridine

  • Aripiprazole

  • Asenapine

  • Carbamazepine

  • Cariprazine

  • Chlorpropamide

  • Clozapine

  • Conjugated estrogens

  • Desflurane

  • Difenoxin hcl

  • Digoxin

  • Diphenoxylate hcl

  • Estradiol

  • Estrogens conjugated synthetic

  • Estropipate

  • Etomidate

  • Fluphenazine

  • Glimepiride

  • Glipizide

  • Glyburide

  • Green tea

  • Haloperidol

  • Hydralazine

  • Iloperidone

  • Insulin

  • Ketamine

  • Lasmiditan

  • Levodopa ya pumzi

  • Lithium

  • Loxapine

  • Loxapine ya pumzi

  • Lurasidone

  • Mestranol

  • Metformin

  • Metrizamide

  • Molindone

  • Olanzapine

  • Tapentadol

  • Thiothixene

  • Tolazamide

  • Tolbutamide

  • Trifluoperazine

  • Yohimbe

  • Ziprasidone

Dawa zenye muingiliano mdogo na Linezolid;

  • Amobarbital

  • Balsalazide

  • Biotin

  • Butabarbital

  • Butalbital

  • Celandine

  • Cordyceps

  • Disulfiram

  • Panax ginseng

  • Pantothenic acid

  • Pentobarbital

  • Phenobarbital

  • Pleurisy root

  • Primidone

  • Pyridoxine

  • Pyridoxine (Kizimua sumu)

  • Secobarbital

  • Sulfadiazine

  • Sulfamethoxazole

  • Sulfisoxazole

  • Thiamine


Matumizi ya Linezolid kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Matumizi ya Linezolid kwa mama mjamzito Hakuna tafiti zinazoonyesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na mtoto aliyepo tumboni hivyo haishauriwi kutumiwa na mama mjamzito. Matumizi ya Linezolid kwa mama anayenyonyesha Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama na husababisha mtoto kuharisha na kutapika hivyo mama anapoitumia tahadhari inapaswa kuchukuliwa juu ya mtoto.


Maudhi ya Linezolid


  • Maumivu ya kichwa

  • Kuharisha

  • Kichefuchefu

  • Kutapik

  • Kizunguzungu

  • Harara kwenye ngozi

  • Moniliasis ya uke

  • Kubadilishwa radha ya chakula

  • Oral moniliasis ya kinywa

  • Kubadilika kwa viashiria vya ufanyaji kazi wa ini

  • Maambukizi ya fangasi

  • Maumivu ya tumbo sehemu moja ya mdomo

  • Kubadilika rangi ya ulimi

  • Maumivu ya tumbo yaliyosambaa

  • Eosinophilia

  • Muwasho

  • Kuhisi vitu vinazunguka

  • Lactic acidosis

  • Kupungua utendaji kazi wa uboho

  • Nyuropathi ya pembeni

  • Madhaifu ya mshipa wa fahamu optic

  • Sindromu ya Serotonin


Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:56:16

Rejea za mada hii:-

Medscape. Linezolid. https://reference.medscape.com/drug/zyvox-linezolid-342574#0. Imechukuliwa 16/09/2021.

WebMD Linezolid. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-18168-6154/linezolid-oral/linezolid-oral/details. Imechukuliwa 16/09/2021.

DRUG COM. Linezolid.https://www.drugs.com/drug-class/oxazolidinone-antibiotics.html. Imechukuliwa 16/09/2021.

Drugbank. Linezolid https://go.drugbank.com/drugs/DB00601. Imechukuliwa 16/09/2021.
bottom of page