Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
Imeboreshwa:
28 Mei 2025, 10:15:48

Dawa Mifepristone
Mifepristone ni dawa ya kuzuia homoni ya projesteroni ambayo hutumika kwa ajili ya kutoa mimba salama (medical abortion), kusababisha uchungu wa uzazi na kutibu hali nyingine zinazohusiana na homoni.
Rangi na Fomu ya Mifepristone
Mifepristone hupatikana katika fomu ya kidonge (tablet).Kidonge mara nyingi huwa na miligramu 200 za mifepristone.Rangi ya kidonge hutofautiana na kampuni lakini huwa nyeupe au kijivu hafifu.
Dawa kundi moja na Mifepristone
Mifepristone haipo kwenye kundi la dawa nyingi, lakini mara nyingi hutumika pamoja na:
Misoprostol – kwa ajili ya kutoa mimba au kusababisha uchungu
Methotrexate – katika baadhi ya taratibu mbadala kwa uavyaji mimba wa mapema
Mifepristone hutibu nini?
Utoaji wa mimba salama (medical abortion) hadi wiki 10 za ujauzito
Kutibu mimba iliyofia tumboni (missed abortion)
Kusababisha uchungu wa uzazi kabla ya upasuaji au kujifungua
Kutibu fibroids au hali ya homoni inayojulikana kama Cushing’s syndrome (katika baadhi ya nchi)
Dozi ya Mifepristone
Kwa kutoa mimba salama: 200 mg kwa mdomo, ikifuatiwa na misoprostol 800 mcg baada ya saa 24–48.
Dozi maalum hutolewa na mtoa huduma wa afya kulingana na hali ya ujauzito na afya ya mgonjwa.
Dawa zisizopaswa kutumika na Mifepristone
Corticosteroids (kama dexamethasone) – hupingana na mifepristone
Anticoagulants (kama warfarin) – huongeza hatari ya kutokwa damu
Erythromycin
Ketoconazole
Rifampin
Phenytoin
St. John’s Wort (dawa ya mitishamba)
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Mifepristone
Mama mjamzito asiye na nia ya kutoa mimba
Wenye historia ya mzigo wa mimba nje ya mji wa mimba (ectopic pregnancy)
Wagonjwa wa pumu kali
Wagonjwa wenye matatizo ya tezi, ini au figo
Wenye matatizo ya damu kuganda (bleeding disorders)
Tahadhari kwa mtumiaji
Dawa itumiwe chini ya uangalizi wa mtoa huduma wa afya mwenye mafunzo maalum.
Tumia kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye historia ya upasuaji mkubwa wa uterasi.
Hakikisha huna mimba nje ya uterasi kabla ya matumizi.
Matumizi kwa mama mjamzito
Hairuhusiwi, isipokuwa kwa madhumuni mahsusi ya kutoa mimba au kusababisha uchungu kwa sababu ya mimba iliyofia tumboni.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Taarifa kuhusu usalama wake wakati wa kunyonyesha bado ni chache. Ushauri wa kitaalamu unahitajika kabla ya kutumia.
Maudhi ya Mifepristone
Baadhi ya maudhi ya kawaida ni:
Maumivu ya tumbo
Kutokwa na damu ukeni
Kichefuchefu
Kuharisha
Kizunguzungu
Homa ndogo
Uchovu
Maumivu ya kichwa
Kutapika
Je, ukisahau dozi ya Mifepristone ufanyaje?
Kwa kuwa dawa hutumika kwa tukio maalum (single use), ni muhimu kufuata ratiba ya dozi kama ilivyoelekezwa. Ikiwa dozi imecheleweshwa, wasiliana na mtoa huduma wa afya kabla ya kuendelea na misoprostol.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa:
28 Mei 2025, 10:11:37
Rejea za mada hii:-
