Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Septemba 2021, 20:16:32

Dawa Moxifloxacin
Moxifloxacin ni anitbayotiki ya jamii ya fluoroquinolone inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuruwa na dawa hii kama maambukizi kwenye sainazi, njia za hewa na mapafu. Majina mengine ya Moxifloxacin ni;
Avelox
Moxifloxacin systemic
Dawa zilizo kundi moja na Moxifloxacin
Dawa zilizo kundi moja na Moxifloxacin ni ;
Ciprofloxacin
Gemifloxacin
Levofloxacin
Ofloxacin
Fomu na uzito wa Moxifloxacin
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Kimiminika kwa ajiri ya sindano
Vidonge
Kimiminika kwa ajiri ya sindano huwa na zuito wa;
400mg/250ml
Vidonge huwa na uzito wa;
400mg
Ufozwaji wa dawa
Hufyonzwa vema kwenye mfumo wa chakula na asilimia 90 ya dawa huingia kwenye damu. Chakula huathiri kwa kiasi kidogo sana ufyonzwaji wake.
Namna Moxifloxacin inavyoweza kufanya kazi
Uwezo wa kitiba wa moxifloxacin hutokana na uwezo wake wa kuzuia ufanyajikaziwa kimeng’enya topoisomerase II (DNA gyrase) na topoisomerase IV. DNA gyrase ni kimeng’enya muhimu katika utengenezaji nakala, unukuu na kurekebisha madhaifu ya DNA ya bakteria. Topoisomerase IV ni kimeng’enya kinachofahamika kufanya kazi ya kugawanya chromosome ya DNA wakati wa kutengenezwa nakala za bakteria.
Moxifloxacin hutibu nini?
Moxifloxacin hutibu magonjwa yafuatayo kutokana na bakteria;
Nimonia
Sinusitiz kali
Konjaktivaitiz ya bakteria
Bakteria kwenye damu
Maambukizi baada ya upasuaji
Plague
Maambukizi ya bakteria kwenye macho
Nimonia ya jamii
Bronkaitiz sugu iliyo kali
Michomo kinga baada ya upasuaji
Magonjwa ya macho
Vimelea wanaodhuriwa na Moxifloxacin
Bacillus anthracis
Bacteroides spp
Citrobacter spp
Clostridium perfringens
Escherichia coli
Enterobacter spp
Haemophilus influenza
Klebsiella pneumoniae
Morganella morganii
Moraxella catarrhalis
Mycobacterium spp
Neisseria gonorrhoeae
Proteus spp
Pseudomonas aeruginosa
Salmonella typhi
Shigella spp
Staphylococcus spp
Streptococcus spp
Vibrio cholerae
Yersinia pestis
Mwingiliano wa Moxifloxacin na chakula
Chakula kina athari ndogo sana kwenye ufyonzwaji wake, hivyo inaweza kutumika bila au pamoja na chakula
Utoaji taka wa Moxifloxacin mwilini
Asilimia ishirini na tano (25%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya haja kubwa na asilimia ishirini (20%) kwa njia ya mkojo.Kiasi kilichobaki hufanyiwa umetaboli na ini na kutolewa katika fomu nyingine.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Moxifloxacin
Wagonjwa wenye mzio wa moxifloxacin. Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Fluoroquinolones.
Dawa zenye muingiliano na Moxifloxacim
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Moxifloxacim;
Amoxapine
Artemether/lumefantrine
Chanjo hai ya BCG
Chanjo ya kipindupindu
Chanjo ya typhoid
Chlorpromazine
Clarithromycin
Doxepin
Epinephrine
Erythromycin
Ferrous sulphate
Haloperidol
Hydroxychloroquine sulphate
Ivosidenib
Ketoconazole
Promethazine
Rose hips
Saquinavir
Trimipramine
Vemurafenib
Ziprasidone
Dawa zinazoweza kutumika na Moxifloxacin chini ya uangalizi;
Amifampridine
Azithromycin
Betamethasone
Chloroquine
Ciprofloxan
Corticotropin
Cortisone
Diclofenac
Dexamethasone
Digoxin
Gilipizide
Hydrocortisone
Ibuprofen
Indomethacin
Insulin
Ketoprofen
Levofloxacin
Magnesium supplement
Mefenamic acid
Warfarin
Mifepristone
Meloxicam
Orfloxacin
Prednisolone
Zinc
Dawa zenye muingiliano mdogo na Moxifloxacin;
Alprazolam
Balsalazide
Biotin
Chlordiazepoxide
Clonazepam
Clorazepate
Estazolam
Flurazepam
Foscarnet
Isotretinoin
Itraconazole
Loprazolam
Lorazepam
Lormetazepam
Midazolam
Oxazepam
Pantothenic acid
Pyridoxine
Pyridoxine (antidote)
Quazepam
Quercetin
Temazepam
Thiamine
Triazolam
Matumizi ya Moxifloxacin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Moxifloxacin kwa mama mjamzito
Tafiti zilizofanyika zinaonesha dawa hii ina madhara kwa mtoto hivyo haipaswi kutumiwa na mama mjamzito.
Matumizi ya Moxifloxacin mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa kwa mtoto na katika uzalishaji wa maziwa.
Maudhi ya Moxifloxacin;
Degedege
Kizunguzungu
Kutapika
Kuferi kwa figo
Mzio
kuchefuchefu
Agranulosaitosis
Kupungukiwa damu
Mwitikio wa anafailaksia
Ini kushindwa kufanya kazi vizuri
Sindromu ya Steven Johnson
Mwitikio wa kinga za mwili
Homa ya ini
Thrombocytopenia
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Endapo utasahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka kama ni masaa nane au zaidi kufikia dozi nyingine ila kama ni chini ya masaa nane usitumie dozi hiyo ila tumia dozi inayofata katika muda sahihi uliopangia. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja ili kufidia dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-