Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
17 Septemba 2021, 09:47:32
Dawa Ofloxacin
Ofloxacin ni moja ya antibiotic jamii ya Fluoroquinolone inayotumika kutibu magonjwa yanayotokana na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii kama nimonia, selulaitiz, homa ya njia ya mkojo, prostaitiz, plague, kaswende, klamidia, uambukizo kwenye ngozi, na aina kadhaa za maradhi ya kuhara.
Majina mengine ya Ofloxacin
Ofloxacin hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kamai;
Anoflox
Canoxcin
Canoxcin
Cebran
Entof
Florobid
Floxin
J P Flox
Ofden
Oflacin
Oflomac
Oflomil
Oflox
Oley
Olfi
Otox
Oxwal
Quinobid
Tarivid
Tarivid
Wyflox
Yflox
Zanocin
Zatroflox
Zenflox
Zo
Dawa zilizo kundi moja na Ofloxacin
Dawa zilizo kundi moja na Ofloxacin ni ;
Ciprofloxacin
Gemifloxacin
Moxifloxacin
Levofloxacin
Fomu na uzito wa Ofloxacin
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;
200mg
300mg
400mg
Namna Ofloxacin inavyoweza kufanya kazi
Uwezo wa kitiba wa ofloxacin hutokana na uwezo wake wa kuzuia ufanyajikaziwa kimeng’enya topoisomerase II (DNA gyrase) na topoisomerase IV. DNA gyrase ni kimeng’enya muhimu katika utengenezaji nakala, unukuu na kurekebisha madhaifu ya DNA ya bakteria. Topoisomerase IV ni kimeng’enya kinachofahamika kufanya kazi ya kugawanya chromosome ya DNA wakati wa kutengenezwa nakala za bakteria.
Vimelea wanaodhuriwa na ofloxacin
Vimelea wanaodhuriwa na Ofloxacin ni;
Chlamydia trachomatis
Citrobacter spp
Enterobacter spp
Escherichia coli
Klebsiella pneumonia
Neisseria gonorrhoeae
Proteus mirabilis
Pseudomonas aeruginosa
Staphylococcus aureus
Streptococcus pneumoniae
Ofloxacin hutibu nini?
Ofloxacin hutibu magonjwa yanayosabaishwa na bakteria wanaodhurika na dawa mfano;
Hutibu maradhi ya bakteria kwenye mfumo wa upumuaji.
Hutibu sinusitis kali
Hutibu maambukizi kwenye ngozi
Hutibu Nimonia
Hutibu Kaswende
Hutibu maambukizi kwenye via vya uzazi
Hutibu maradhi ya bakteria kwenye mfumo wa mkojo
Hutibu Kimeta
Hutibu maambukizi kwenye tezi dume
Hutibu epididymis
Hutumika kutibu mchafuko wa tumbo
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula.
Mwingiliano wa Ofloxacin na chakula
Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.
Utoaji taka wa Ofloxacin mwilini
Asilimia themanini (80%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia nne hadi nane (4%-8%) kwa njia ya haja kubwa.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ofloxacin
Wagonjwa wenye mzio wa Ofloxacine
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Fluoroquinolones.
Dawa zenye muingiliano na Ofloxacim
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ofloxacim; Arsenic trioxide
Artemether
Chanjo hai ya bcg
Carbonyl iron
Chanjo hai ya kipindupindu
Didanosine
Disopyramide
Entrectinib
Ferric maltol
Ferrous fumarate
Ferrous gluconate
Ferrous sulfate
Fexinidazole
Glasdegib
Hydroxychloroquine sulfate
Indapamide
Ivosidenib
Lefamulin
Quinidine
Ribociclib
Rose hips
Selinexor
Chanjo hai ya typhoid
Dawa zinazoweza kutumika na Ofloxacin chini ya uangalizi; Artemether/lumefantrine
Bedaquiline
Betamethasone
Chloroquine
Clarithromycin
Dexamethasone
Diclofenac
Digoxin
Epinephrine
Erythromycin base
Fluconazole
Glipizid
Hydrocortisone
Haloperidol
Ibuprofen
Indomethacin
Insulin
Ketoconazole
Magnesium suppliments
Mefenamic acid
Meloxicam
Mifeprostol
Metformin
Moxifloxacin
Levofloxacin
Methadone
Piroxicam
Prednisolone
Quinine
Promethazine
Warfalin
Zinc
Dawa zenye muingiliano mdogo na Ofloxacin;
Aceclofenac
Acemetacin
Aspirin
Azithromycin
Chlordiazepoxide
Chloroquine
Diclofenac
Glimepiride
Glipizide
Glyburide
Hydrochlorothiazide
Ibuprofen
Indomethacin
Insulin
Ketoprofen
Mefenamic acid
Meloxicam
Metformin
Methyclothiazide
Piroxicam
Quinine
Sulfamethoxazole
Thiamine
Verapamil
Maudhi madogo ya Ofloxacin;
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Kuharisha
Kukosa usingizi
Kupata choo kigumu
Kizunguzungu
Mvurugiko wa tumbo
Vipele
Kutapika
Kifua kuuma
Kushindwa kupumua
Mwili kuvimba
Mwili kuchoka
Maambukizi ya fangasi
Maumivu
Ngozi kuwasha
Maambukizi ukeni
Kukosa hamu ya kula
Mvurugiko katika mfumo wa chakula
Kukosa usingizi
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kifua
Matumizi ya Ofloxacin kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa tahadhari inatakiwa wakati mama mjamzito anatumia dawa hii kwani inaweza kuleta madhara kwa mtoto.
Matumizi ya Ofloxacin mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonesha dawa hii inatolewa kwenye maziwa ya mama hivyo mama anatakiwa kuchagua kimoja kati ya kunyonyesha au kutumia dawa.
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa kumeza dozi inayofata umekaribia sana usimeze dozi Uliyosahau subiria muda ufike wa dozi nyingine kisha endelea na dozi hiyo kwa muda sahihi uliopangiwa na Daktari. Usitumie dozi mbili kufidia dozi iliyosahaulika.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-