Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Septemba 2021, 09:41:38

Dawa Pamidronate
Pamidronic acid ni dawa ya kizazi cha pili cha bisphosphonate inayotumika katika matibabu ya ugonjwa wa Paget, kushusha kiwango cha juu cha kalisiamu kwenye damu kinachotokana na saratani na mifupa dhaifu.
Majina mengine ya Pamidronate
Majina mengine ya Pamidronate ni;
Aredia Pamisol
Dawa zilizo kundi moja na Pamidronate
Dawa zilizo kundi moja na Pamidronate ni;
Risedronate
Etidronate
Alendronate
Ibadronate
Zoledronate
Fomu ya dawa ya Pamidronate
Dawa hii ipo katika fomu ya Unga kwa ajili ya kutumika kama sindano wenye uzito wa 30mg Kimiminika kwa ajili ya sindano chenye uzito wa;
3mg/ml
6mg/ml
9mg/ml
Pamidronate hutibu nini?
Hutumika kutibu ugonjwa wa paget
Hutumika kutibu hyperkalsemia ya saratani
Hutumika kutibu saratani ya matiti iliyosambaa kwenye
Hutumika kutibu saratani ya multiple myeloma iliosambaa kwenye mifupa
Hutumika kukinga udhaifu wa mifupa kutonana na upungufu wa Androgen
Namna Pamidronate inavyoweza kufanya kazi
Dawa jamii ya Bisphosphonates kama ikiwa pamoja na Etidronate hufyonzwa na chembe na mifupa kisha kujishikiza kwenye hydroxyapatite. Kujishikiza huku husababisha kutengeneza mazingira ya utindikali na kuzalishwa kwa bisphosphonate inayosaidia chembe za osteoclast kuzuia kufyonzwa kwa kwa madini kalisiamu yaliyo kwenye mifupa.
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikiingia kwenye mishipa.
Mwingiliano wa Pamidronate na chakula
Hakuna mwingiliano uliolipotiwa kama ikitumika na chakula
Utoaji taka wa Pamidronate mwilini
Dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo bila kufnayiwa umetaboli. Nusu maisha yake ni masaa 28±7.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Pamidronate
Wagonjwa wenye mzio wa Pamidronate
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya kalisiamu
Dawa zenye muingiliano na Pamidronate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Pamidronate; Tafiti zinaonesha hakuna dawa yenye muingiliano mkali na Pamidronate. Dawa zinazoweza kutumika na Pamidronate chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Dichlorphenamide
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Tenofovir df
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Pamidronate;
Entecavir
Foscarnet
Teriparatide
Matumizi ya Pamidronate kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Pamidronate kwa mama mjamzito Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliye tumboni hivyo hairuhusiwi kwa mama mjamzito. Matumizi ya Pamidronate mama anayenyonyesha Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo hairuhusiwi kutumiwa na mama anayenyonysha.
Maudhi ya Pamidronate
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya mifupa, misuli na viungio vya mwili
Degedege
Homa
Kupungukiwa damu
Kizunguzungu
Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Kutapika
Kichefuchefu
Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa hewa
Kikohozi
Kupoteza hamu ya kula
Kupungu kwa kiwango cha kalisiam kwenye damu
Madini ya magnesium kupungua
Dalili za kuzidisha dozi;
Kupungua kwa kiwango cha kalisiamu kwenye damu
Homa
Kushuka kwa shinikizo la damu
Kubadilika kwa ladha
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi kwa wakati sahihi muone daktari wako ili aweze kukupangia muda sahihi wa kutumia dozi inayofata.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:56:16
Rejea za mada hii:-