Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Septemba 2021 19:21:09
Dawa Piperacillin
Piperacillin ni dawa ya antibayotiki katika kundi la ureidopenicillin. Dawa hii hutibu maambukizi ya wastani hadi makali ya bakteria wanaodhurika nayo haswa wale wa gramu chanya na hufahamika kwa majina mengine ya pipracil, hubercilina, piperacillin, pipril
Fomu na Uzito wa Piperacillin
Piperacillin hupatikana katika fomu ya unga wenye uzito wa
2 gm
3 gm
4 gm
40gm
Unga huu huchanganywa na maji ili kutumika kwa kuchoma sindano
Dawa zilizo kundi moja na Piperacillin
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Piperacillin ni zifuatazo :
Amoxicillin
Bacampicillin
Penicillin G
Penicillin V
Methicillin
Ampicillin
Procaine Penicillin
Dicloxacillin
Piperacillin hutibu magonjwa gani?
Matumizi ya Piperacillin ni kama zifuatazo :
Maambukizi ya UTI yasiyo makali
Cholangitis kali
Kaswende isiyo sugu
Maambukizi ya Pseudomonas
Ugonjwa wa Cystic Fibrosis
Vimelea wanaodhuriwa na Piperacillin
Vimelea wanaodhuriwa na dawa hii
Streptococcus spp
Enterococcus
Listeria monocytogenes
Pseudomonas aeruginosa
Klebsiella, Serratia
Enterobacter
Enterococcus
H. influenza
E. coli
Proteus mirabilis
Salmonella spp
Shigella spp
Vimelea wengine wanaoweza kudhuriwa na dawa hii
Acinetobacter spp.,
Alcaligenes xylosoxidans
Bacteroides spp
Citrobacter diversus
Citrobacter freundii
E. coli
Fusobacteriae
H. influenza
Klebsiella spp
N. gonorrhoeae
Peptococcus spp
Peptostreptococcus spp
indole-pos
Proteus spp
Providencia spp
Pseudomonas spp
Serratia spp
Streptococcus faecals
Yersinia enterolitica
Namna piperacillin inavyofanya kazi na utoaji taka mwilini
Piperacillin hufanya kazi kwa kujishikiza kwenye mlango wa penicillin, mlango huu hutumiwa na kimeng’enya cha peptidoglycan ili kuzalisha vijenzi muhimu vya ukuta wa bakteria. Kufanya kazi kwa dawa hii huzuia utengenezaji wa ukuta wa bakteria wanaodhuriwa na dawa hii na hivyo pia kuzuia uzalianaji wake. Utoaji taka wa Piperacillin mwilini Asilimia 80 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na kiasi kilichobaki hutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Namna ya kutumia piperacillin
Dawa hii hufyonzwa yote na kuingia kwenye mzunguko wa damu inapochomwa ndani ya mishipa ya damu. Dawa hii inapaswa kuchomwa taratibu kwa muda wa dakika 5 hadi 30
Mwingiliano wa Piperacillin na chakula
Piperacillin kwa kuwa hutumika kwa njia ya mishipa, inaweza kutumika na chakula au pasipo chakula
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Piperacillin
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Penicillin
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya cephalosporins
Wagonjwa wenye mzio na imipenem
Mwingiliano wa Piperacillin na dawa zingine
Mwingiliano mkali hazipaswi kutumika pamoja na Ampicillin
Antithrombin alfa
Antithrombin III
Argatroban
BCG vaccine live
Bivalirudin
Cholera vaccine
Dalteparin
Enoxaparin
Heparin
Omadacycline
Sarecycline
Warfarin
Piperacillin ikitumika na dawa hizi mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu :
Azithromycin
Bazedoxifene
Chloramphenicol
Clarithromycin
Demeclocycline
Dichlorphenamide
Doxycycline
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Minocycline
Probenecid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/Anhydrous citric acid
Tetracycline
Vancomycin
Dawa hizi zina mwingiliano mdogo na Piperacillin
Amikacin
Aspirin
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Chlorothiazide
Choline magnesium trisalicylate
Gentamicin
Hydrochlorothiazide
Ibuprofen IV
Meclofenamate
Neomycin PO
Rose hips
Streptomycin
Tobramycin
Willow bark
Matumizi ya Piperacillin kwa mama mjamzito
Tafiti za wanyama zinaonyesha hatari kwa vichanga kwa ksuababisha madhaifu ya kimaumbile. Taarifa za tafiti kwa binadamu hazipatikani au hazijafanyika.
Matumizi ya Piperacillin kwa mama anayenyonyesha
Usitumie dawa hii wakati wa kunyonyesha au acha kunyonyesha wakati unatumia dawa hii
Maudhi madogo ya Piperacillin
Kuharisha
Kizunguzungu
Homa
Maumivu ya kichwa
Upungufu wa damu kutokana na kuvunjwa cha chembe nyekundu za damu
Hemolytic anemia
Maumivu sehemu iliyochomwa sindano
Nephraitis
Maambukizi ya pseudomonas
Kichefuchefu
Fangasi mdomoni
Ongezeko la muda wa prothrombin
Harara kwenye ngozi
Degedege
Mzio mkali( anafailaksia)
Thrombophlebitis
Maambukizi ya fangasi ukeni
Kutapika
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-