Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Septemba 2021 11:50:24
Dawa Piperacillin/tazobactam
Piperacillin tazobactam ni dawa ya antibayotiki katika kundi la penicillin iliyounganishwa na tazobactam kwa ajili ya kuongeza uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria haswa wa gramu hasi, na kiasi cha bakteria wa gramu chanya na anaerobiki. Tazobactam inayoongezwa kwenye dawa hii huwa na uwezo wa kuzuia kimeng’enya muhimu cha bakteria chenye jina la β-lactamase huongeza uwezo wa dawa hii zaidi na kufanya dawa ifanye kazi kwa vimelea wanaozalisha kimeng'enya hiki.
Uzito na fomu ya Piperacillin Tazobactam
Piperacillin Tazobactam hupatikana kama unga kwenye kichupa kwa ajili ya kuchanganywa na maji na kuchomwa kwa sindano. Kichupa kinaweza kuwa na
2.25gm (2gm piperacillin na 0.25gm za Tazobactam)
3.375 gm (3gm piperacillin na 0.375gm za Tazobactam)
4.5 gm (4gm piperacillin na 0.5gm za Tazobactam)
40.5gm ( 36gm piperacillin na 4.5gm za Tazobactam)
Dawa zilizo kundi moja na Piperacillin/tazobactam
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja(penicillin) na Piperacillin/tazobactam ni zifuatazo :
Amoxicillin
Bacampicillin
Penicillin G
Penicillin V
Methicillin
Ampicillin
Procaine Penicillin
Dicloxacillin
Dawa ambazo zipo kundi moja na piperacillin/tazobactam kama kundi la dawa zilizoongezewa uwezo mpana wa matibabu
Piperacillin
Piperacillin/tazobactam
Pipracil
Ticarcillin/clavulanate
Timentin
Namna Piperacillin inavyoweza kufanya kazi
Piperacillin hufanya kazi kwa kujishikiza kwenye mlango wa penicillin, mlango huu hutumiwa na kimeng’enya cha peptidoglycan ili kuzalisha vijenzi muhimu vya ukuta wa bakteria. Kufanya kazi kwa dawa hii huzuia utengenezaji wa ukuta wa bakteria na hivyo pia kuzuia uzalianaji wake. Tazobactam inayoungwa na dawa hii, huzuia kimeng’enya beta lactamase ambacho huzalishwa na bakteria ili kuvunja dawa hii hivyo kufanya dawa iweze kufanya kazi vema na kuongeza upana wake wa matibabu ya bakteria gramu hasi, gramu chanya na wale jamii ya anaerobic.
Vimelea wanaodhuriwa na Piperacillin
Staphylococcus aureus
Escherichia Coli
Haemophilus influenza
Klebsiella Pneumoniae
Pseudomonas aeruginosa
Bacteroides fragilis
Bacteroides ovatus
Bacteroides thetaiotaomicron
Bacteroides vulgatus
Acinetobacter baumannii
Mwingiliano wa Piperacillin/tazobactam na chakula
Piperacillin Tazobactam haiathriwi na cha kula kwa kuwa hutumika kwa kuchoma ndani ya michipa ya damu.
Piperacillin/Tazobactam hutibu nini?
Matumizi ya Piperacillin/Tazobactam ni kama zifuatazo :
Kutibu maambukizi ya bakteria kwenye via vya tumbo
Kutibu maambukizi ndani ya via vya uzazi kwa wanawake (PID)
Kutibu nimonia ya jamii
Kutibu nimoni ya hospitali
Kutibu maambukizi ya bakteria kwenye ngozi
Michomo kwenye appendix (Appendisaitis)
Selilaitiz
Endometriosis baada ya kujifungua
Ili kuzuia usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa hii, dawa hii inapaswa kutumika kutibu au kukinga shidi ya vimelea ambao wanadhuriwa na dawa hii tu.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Piperacillin/Tazobactam
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Penicillin
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya cephalosporins
Wagonjwa wenye mzio na carbapenem
Tahadhari kwa watumiaji wa Piperacillin/Tazobactam
Huweza sababisha mzio makali wa anafailaksia au sindromu ya Stevens-Johnson
Kuvuja kwa damu kutokana na kuharibiwa kwa mchakato wa ugandishai damu , kama dalili zitatokea, dawa isitishwe haraka
Huweza sababisha upungufu wa chembe ulinzi za leucocyte na neutrophil inayoisha baada ya kuacha damu
Kuchokoza mfumo wa fahamu kiasi cha kupelekea degedege
Kudhuru figo kwa mgonjwa mwenye ugonjwa mkali
Huweza haribu kiwango cha madini kwenye damu kwamgonjwa anayedhibitiwa kiasi cha madini mwilini haswa madini sodiamu (Na+)
Kuhara kutokana na maambukizi ya Clostridium difficile
Ongezeko la usugu wa vimelea kwenye dawa hii endapo itatumika bila kuwa maambukizi
Utoaji taka wa Piperacillin/Tazobactam mwilini
Asilimia 80 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia zinazobaki hutolewa kwa njia ya haja kubwa
Mwingiliano wa Piperacillin/Tazobactam na dawa zingine
Mwingiliano mkali hazipaswi kutumika pamoja na;
Ampicillin
Antithrombin alfa
Antithrombin III
Argatroban
BCG vaccine live
Bivalirudin
Cholera vaccine
Dalteparin
Enoxaparin
Heparin
Omadacycline
Sarecycline
Warfarin
Piperacillin/Tazobactam ikitumika na dawa hizi mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu;
Azithromycin
Bazedoxifene
Chloramphenicol
Clarithromycin
Demeclocycline
Dichlorphenamide
Doxycycline
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Minocycline
Probenecid
Sodium picosulfate/magnesium oxide/Anhydrous citric acid
Tetracycline
Vancomycin
Dawa hizi zina mwingiliano mdogo na Piperacillin/Tazobactam;
Amikacin
Aspirin
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Chlorothiazide
Choline magnesium trisalicylate
Gentamicin
Hydrochlorothiazide
Ibuprofen IV
Meclofenamate
Neomycin PO
Rose hips
Streptomycin
Tobramycin
Willow bark
Matumizi ya Piperacillin/Tazobactam kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Piperacillin/Tazobactam kwa mama mjamzito Tafiti za wanyama zinaonyesha hatari kwa vichanga kwa ksuababisha madhaifu ya kimaumbile. Taarifa za tafiti kwa binadamu hazipatikani au hazijafanyika. Matumizi ya Piperacillin/Tazobactam kwa mama anayenyonyesha Dawa hii inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha ,hakuna tafiti zinazoenyesha madhara yatakayompata mtoto
Maudhi madogo ya Piperacillin/Tazobactam
Kuhara
Haja kubwa ngumu
Kichefuchefu
Gesi tumboni
Maumivu ya tumbo
Homa
Maumivu sehemu dawa ilipochomwa
Kukakamaa kwa misuli
Anafailaksis
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya misuli
Maambukizi ya fangasi ukeni
Maumivu ya maungio ya miguu na mikono
Kukosa usingizi
Harara kwenye ngozi
Vipele kwenye ngozi
Kuvimba kwa ngozi
Muwasho wa ngozi
Kuvia damu chini ya ngozi
Kushuka kwa sukari kwenye damu
Michomo kinga kwenye mshipa wa damu
Kushuka kwa shinikizo la damu
Kutokwa na jasho
Kutokwa na damu puani
Je endapo utasahau dozi yako ya Piperacillin/Tazobactam ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi inayofuata kama muda uliopangiwa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-