Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Septemba 2021, 09:57:07
Dawa Primaquine
Primaquine ni dawa kunywa jamii ya aminoquinoline inayotumika katika matibabu ya malaria inayosababishwa na plasmodium vivax na ovale, pia hutumika kaa kinga ya malaria kwa watu wanaorejea nyumbani katika maeneo ambayo hayana malaria.
Majina mengine ya Primaquine
Primaquine hufahamika kwa jina majina mengine kama
Jasoprim
Primachin
Primachina
Primachinum
Primaquin
Primaquina
Primaquine
Primaquinum
Fomu na uzito wa Primaquine
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa Milligramu 26.3
Primaquine hutibu nini?
Primaquine hutumika kwenye matibabu ya;
Malaria inayosababishwa na Plasmodium ovale
Malaria inayosababishwa na plasmodium vivax
Kutibu malaria inayosababishwa na plasmodium
Nimonia inayosababishwa na Pneumocystis Jirovecii
Namna Primaquine inavyoweza kufanya kazi
Ufanyaji kazi wa dawa ya primaquine haufahamiki vema mpaka sasa. Hudhaniwa kufanya kazi kwa kuzalisha radiko za oksijen zenye zinazoingilia usafirishaji wa elekroni ndani ya kimelea cha malaria, hii hufanya kimelea hao kufa. Hata hivyo licha ya kutofahamika namna unavyofanya kazi, primaquine ina uwezo wa kujishikiza na kubadili DNA vimelea wa malaria na protozoa wengine.
Utoaji taka wa Primaquine
Dawa hii hutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Primaquine
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Primaquine
Wagonjwa wenye upungufu mkali wa kimeng’enya glucose-6-phosphate dehydrogenase (G6PD)
Tahadhari kwa watumiaji wa primaquine
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kama
Itatumika pamoja na quinacrine au kwa wagonjwa waliotumia quinacrine hivi karibuni
Itatumika pamoja na dawa zinazosababisha kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu au dawa zinazopunguza uzalishaji wake kwenye uboho
Itatumika kwa wagonjwa wenye ugonjwa mkali unaosababisha granulocytopenia kama vile rheumatoid arthraitiz na lupus erythematosus
Matumizi ya primaquine na chakula
Matumizi ya dawa hii pamoja na chakula huzuia maudhi makubwa katika mfumo wa tumbo. Tumia pamoja na chakula kama utakavyoelekezwa na daktari wako.
Mwingiliano wa Primaquine na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika kabisa pamona na Lefemulin
Dawa zenye mwingiliano mkali za kuzuia dawa hii kutumika pamoja na dawa zingine;
Abametapir
Apalutamide
Carbamazepine
Clarithromycin
Dapsone a kupaka
Deferiprone
Entrectinib
Enzalutamide
Fexinidazole
Fosphenytoin
Glasdegib
Grapefruit
Idelalisib
Ivosidenib
Lonafarnib
Mifepristone
Pirfenidone
Pitolisant
Pomalidomide
Primidone
Quinacrine
Rifampin
Stiripentol
Tucatinib
Voxelotor
Primaquine ikitumika na dawa hizi mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu :
Acalabrutinib
Avapritinib
Axitinib
Bosentan
Kiandikizi cha Bupivacaine
Cenobamate
Crofelemer
Dabrafenib
Darunavir
Efavirenz
Elagolix
Eluxadoline
Elvitegravir
Encorafenib
Etravirine
Finerenone
Flibanserin
Fostemsavir
Ifosfamide
Iloperidone
Istradefylline
Itraconazole
Lemborexant
Lorlatinib
Midazolam intranasal
Mitotane
Nafcillin
Osilodrostat
Oxaliplatin
Pentoxifylline
Phenobarbital
Rifabutin
Rifapentine
Rucaparib
Stiripentol
Tasimelteon
Tazemetostat
Tecovirimat
Terbinafine
Tetracaine
Tinidazole
Triclabendazole
Zidovudine
Dawa hizi zina mwingiliano mdogo na Primaquine
Chloroquine
Dapsone
Isoniazid
Probenecid
Quinine
Ribociclib
Ruxolitinib
Sulfadiazine
Sulfamethoxazole
Sulfisoxazole
Matumizi ya Primaquine kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ina madhara endapo itatumika kwa mama mjamzito. Hivyo haipaswi kutumika isipokuwa kama kuna faida za matumizi kuliko madhara yanayofahamika kutokea. Wanawake wanaoshiriki ngono, wanapaswa kutumia dawa za uzazi wa mpango ili wasinase mimba wakati wanatumia dawa hii au kupimwa ujauzito kabla ya kuanza kutumia dawa hii.
Matumizi ya Primaquine kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha kutokana na tafiti kuonyesha kuwa huweza kuleta madhara kwa mtoto.
Maudhi ya Primaquine
Maumivu ya tumbo
Upungufu wa damu kwa wagonjwa wenye upungufu wa G6PD
Kichefuchefu
Kutapika
Agranulosaitosis
Arrhithmias
Muamivu ya kichwa
Uono hafifu
Leukopenia
Leukosatosis
Harara kwenye ngozi
Kizunguzungu
Muwasho
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje ?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapo kumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana utatakiwa kuruka dozi uliyosahau kisha kuendelea na dozi inayofuata kama muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-