Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Septemba 2021 17:48:16
Dawa Pyrazinamide
Pyrazinamide ni moja kati ya antibiotic inayofanya kazi ya kuzuia ukuaji wa bakteria aina ya mycobacteria tuberculae anayesababisha kifua kikuu (TB). Pyrazinamide ni Antibiotiki iliyo katika kundi la dawa za Kutibu TB.
Majina mengine ya Pyrazinamide
Majina mengine ya Pyrazinamide ni;
Rifater
Rimstar
Voractiv
Dawa zilizo kundi moja na Pyrazinamide
Dawa zilizo kundi moja na Pyrazinamide ni ;
Isoniazid
Ethambutol
Rifampicin
Fomu ya dawa ya Pyrazinamide
Dawa hii ipo kwenye fomu ya kidonge chenye uzito wa 500mg
Namna Pyrazinamide inavyoweza kufanya kazi
Hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria aina ya mycobacteria tuberculae.
Vimelea wanaodhuriwa na Pyrazinamide
Mycobacteria tuberculae
Pyrazinamide hutibu nini?
Pyrazinamide hutumika na dawa zingine kutibu maambukizi ya kutibu kifua kikuu (TB)
Ufozwaji na Mwingiliano wa Pyrazinamide na chakula
Ufyonzwaji
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula
Mwingiliano wa Pyrazinamide na chakula Dawa hii huweza kutumika mtu akiwa amepata chakula ama akiwa bado hajapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Pyrazinamide
Wagonjwa wenye mzio wa Pyrazinamide. Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii za TB
Utoaji taka wa Pyrazinamide mwilini
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo
Matumizi ya Pyrazinamide kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Pyrazinamide kwa mama mjamzito Tafiti zilizofanyika hazijaonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito ila kwa wanyama ilionekana kuleta madhara kwa watoto wao, hivyo haishauriwi kutumia wakati wa ujauzito. Matumizi ya Pyrazinamide mama anayenyonyesha Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha hivyo haitakiwi kutumika ama kimoja kati ya dawa na kunyonyesha mama anaweza akaacha kulingana na uhitaji.
Dawa zenye muingiliano na Pyrazinamide
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Pyrazinamide;
Peridartinib
Pretomanid
Rifampin
Dawa zinazoweza kutumika na Pyrazinamide chini ya uangalizi;
Cydosporine
Mipomersen
Probenecid
Dawa zenye muingiliano mdogo na Pyrazinamide;
Isoniazid
Taerolimus
Maudhi ya Pyrazinamide
Mwili kudhoofika
Mwili kuwasha
Kupoteza hamu ya kula
upele
Gauti
Maumivu kwenye viungio vya mwili
kichefuchefu
kutapika
Kuchoka
Anorexia
Homa
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-