Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Septemba 2021, 16:09:08
Dawa Pyrimethamine
Pyrimethamine ni moja kati ya dawa inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na vimelea vya toxoplasma na malaria ambayo huingia kwenye ubongo na macho pia kukinga dhidi ya ugonjwa wa toxoplasmosis kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi. Majina mengine ya pyrimethamine ni daraprim. Dawa zilizo katika kundi la Antimalarials zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni; Aryl aminoalcohol ambazo ni;
Quinine
Lumefantrine
Chloroquine
Quinidine
Antifolate compound
Pyrimethamine
Proguanil
Chlorproguanil
Trimethoprim
Artemisinin compound
Artesunate
Dihydroartemisinin
Artemisin
Artemether
Fomu ya dawa na uzito wa dawa Pyrimethamine
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa 25mg
Ufozwaji wa Pyrimethamine
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula.
Namna Pyrimethamine inavyoweza kufanya kazi
Pyrimethamine huzuia kimeng’enya cha malaria chenye jina la dihydrofolate reductase na hivyo kuzuia utengenezaji wa purines na pyrimidines vijenzi muhimu vya DNA na kutoa nakala za vimelea. Utendaji kazi huu hupelekea kufeli kwa uzalishaji wa nuklia za viini vya malaria ndnai ya chembe nyekundu za damu na ini.
Vimelea wanaodhuriwa na Pyrimethamine
Plasmodium
Toxoplasmosis
Pyrimethamine hutibu nini?
Hutumika kama kinga na kutibu malaria isyo kali na inayosababishwa na P. falciparum
Hutumika kukinga na kutibu toxoplasmosis kama ikiunganishwa na sulfonamide
Ufyonzaji na mwingiliano wa Pyrimethamine na chakula
Mwingiliano wa Pyrimethamine na chakula
Dawa hii ni nzuri ikitumika na chakula ili kupunguza kichefuchefu na kutapika
Ufozwaji wa pyrimethamine Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri kwenye mfumo wa chakula
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Pyrimethamine
Wagonjwa wenye mzio wa dawa ya pyrimethamine
Utoaji taka wa Pyrimethamine mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii hulolewa kwa njia ya mkojo.
Matumizi ya Pyrimethamine kwa mama mjamzito
Tahadhari inatakiwa kuchukuliwa wakati mama anatumia dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto.
Matumizi ya Pyrimethamine kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii inapatikana kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha hivyo chagua kuacha kutumia dawa au kunyonyesha mtoto lakini umuhimu wa dawa kwa mama unatakiwa uzingatiwe.
Dawa zenye muingiliano na
Pyrimethamine
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Pyrimethamine;
Dapsoneya kupaka
Deferiprone
Erdafitinib
Siponimod
Dawa zinazoweza kutumika na Pyrimethamine chini ya uangalizi;
Acalabrutinib
Brexpiprazole
Bupivacaine njiti
Folic acid
Hydroxyurea
Ifosfamide
L-methylfolate
Oliceridine
Tamsulosin
Dawa zenye muingiliano mdogo na Pyrimethamine;
Chlorpromazine
Dapsone
Ethotoin
Fluphenazine
Fosphenytoin
Lorazepam
Perphenazine
Phenytoin
Prochlorperazine
Promazine
Promethazine
Sapropterin
Sulfadiazine
Sulfamethoxazole
Sulfisoxazole
Thioridazine
Trifluoperazine
Zidovudine
Maudhi ya Pyrimethamine
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kuzimia
Kukosa hamu ya kula
Homa
Kupata mawazo
Mwili kudhoofika
Kutapika
Kuwashwa mwili na kupata vipele
Kukosa usingizi
Kizunguzungu
Magonjwa ya ngozi
Degedege
Sindromu ya Steven Johnson
Upungufu wa chembe nyeupe za damu
Kupungua uzito
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu kupata dawa hii kwa wakati sahihi. Kama umesahau dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia ambapo utatakiwa subiri muda huo kisha kuendelea na dozi inayofuata nakuacha dozi uliyosahau. Hauruhusiwi kutumia dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:25
Rejea za mada hii:-