Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Septemba 2021 16:37:05
Dawa Rifampicin
Rifampicin ni moja kati ya antibiotic kundi la antitubercular inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria aina ya mycobacteria tuberculae kwenye anayesababisha kifua kikuu (TB). Majina mengine ya Rifampicin
Majina mengine ya Rifampicin ni;
Rifadin
Rimactane
Rifampin
Dawa zilizo kundi moja na rifampicin
Dawa zilizo kundi moja na rifampicin ni ;
Isoniazid
Ethambutol
Pyrazinamide
Fomu ya dawa ya rifampicin
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Tembe yenye uzito wa miligramu 150 na 300
Unga wenye uzito wa gramu 600 kwa chupa kwa ajili ya kutumika kwa kuchoma
Rifampicin hutibu nini?
Hutumika kutibu kifua kikuu (TB)
Namna Rifampicin inavyoweza kufanya kazi
Rifampin inafikiriwa kufanya kazi kwa kuzuia DNA ya bakteria inayotegemea kimeng’enya RNA polymerase ndani ya njia za DNA/RNA ili kuzuia utengenezaji wa RNA. Ufanyaji kazi hu hudhaniwa kutegemea wingi wa kiini cha dawa.
Vimelea wanaodhuriwa na rifampicin
Mycobacteria tuberculae
Ufozwaji wa rifampicin
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikimezwa bila chakula kwani chakula hupunguza kiwango cha dawa kinachofyonzwa.
Utoaji taka wa Rifampicin mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kiwango kidogo kwa njia ya mkojo.
Mwingiliano wa Rifampicin na chakula
Chakula hupunguza uwezo wa dawa hii kufanya kazi hivyo inashauriwa kutumia dawa hii ukiwa hujapata chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Rifampicin
Wagonjwa wenye mzio wa Rifampicin Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya antitubercular
Dawa zenye mwingiliano na Rifampicin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Rifampicin;
Artemether/lumefantrine
Atazanavir
Atorvastatin
Bedaquiline
Carbamazepine
Chanjo hai ya BCG
Chanjo hai ya typhoid
Conjugated estrogen
Cortisone
Dexamethasone
Diazepam
Erythromycin
Felodipine
Fludrocortisone
Hydrocortisone
Isoniazid
Lansoprazole
Lopinavir
Lovastatin
Methadone
Norethindrone
Prednisolone
Progesterone
Pyrazinamide
Warfarin
Dawa zinazoweza kutumika na Rifampicin chini ya uangalizi;
Amlodipine
Artesunate
Artorvastatin
Azithromycin
Acetaminophen
Hydrocortisone
Ketamine
Methadone
Quinine
Tramadol
Digoxin
Dexamethasone
Pentobarbital
Phenobarbital
Diazepam
Chloroquine
Zidovudine
Clarithromycin
Clotrimazole
Ketoconazole
Esomeprazole
Losartan
Gentamycin
Cervedilol
Dawa zenye muingiliano mdogo na Rifampicin;
Acetaminophen
Ampicillin
Chloramphenicol
Diazepam
Diclofenac
Fluconazole
Ibuprofen
Isosorbide mononitrate
Ketoconazole
Lansoprazole
Loratadine
Meloxicam
Miconazole a kuweka ukeni
Morphine
Oxacillin
Piroxicam
Rabeprazole
Sulfamethoxazole
Tibolone
Tolbutamide
Trandolapril
Voriconazole
Warfarin
Matumizi ya Rifampicin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya Rifampicin kwa mama mjamzito Dawa hii inapita kwenye kondo la mtoto na kuonekana kwenye damu inayosafiri kwenda kwa mtoto hivyo inaleta madhara kwa mtoto. Haitakiwi kutumiwa na mama mjamzito. Matumizi ya Rifampicin mama anayenyonyesha Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha hivyo haitakiwi kutumika ama kimoja kati ya dawa na kunyonyesha mama anaweza akaacha kulingana na uhitaji.
Maudhi madogo ya Rifampicin
Kupata ganzi
Kutoa machozi rangi ya machugwa
Kichwa kuuma
Upele
kuharisha
maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
kutapika
Kuchoka
Tabia kubadirika
Kuvimba mwili
Kupunguza uwezo wa kufikili
Homa
Misuli kukosa nguvu
Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?
Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:25
Rejea za mada hii:-