Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 11:14:04

Dawa ya Butoconazole
Butoconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Femstat 3.
Fomu ya dawa Butoconazole
Butoconazole hupatikana katika fomu ya krimu yenye ujazo mbalimbali wenye asimilia 2 ya kiini cha dawa
Namna Butoconazole inavyofanya kazi
Dawa ya Butoconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi aina ya imidazole. Ufanyaji kazi wa dawa hii haujulikani lakini husababisha kuzuia utengenezaji wa homoni muhimu katika ukuta wa seli ya fangasi ijulikanacho kama egosteroli.
Dawa kundi moja na Butoconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: • Bifonazole • Clotrimazole • Econazole • Fenticonazole • Isoconazole • Ketoconazole • Luliconazole • Miconazole • Omoconazole • Oxiconazole • Sertaconazole • Sulconazole • Tioconazole
Kazi ya Butoconazole
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Butoconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Butoconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii hushauriwa kutumika wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Butoconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.
Maudhi ya Butoconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii yanayoweza kujitokeza ni pamoja na : • Kupata vipele • Kuhisi kuungua • Maumivu ya tumbo • Kuwashwa mwili
Ukisahau dozi ya Butoconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau tumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-