Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 12:22:48

Dawa ya Haloprogin
Haloprogin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la benzylidenebenzofuran.
Fomu ya Haloprogin
Dawa hii hupatikana katika fomu ya krimu yenye asilimia 1 ya kiini cha dawa
Namna Haloprogin inavyofanya kazi kutibu fangasi
Dawa hii ya haloprogin hufanya kazi kwa kuzuia seli za fangasi kutumia hewa ya oksijeni hivyo kusababisha zife
Kazi ya Haloprogin
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi ya tinea
Dawa zilizo kundi moja na Haloprogin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Alfuzosin
Alprazolam
Cobimetinib
Conivaptan
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine intranasal
Disopyramide
Dronedarone
Eliglustat
Flibanserin
Ibutilide
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Haloprogin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Haloprogin kwa mama mjamzito
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi ya Haloprogin kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya dawa Haloprogin
Baadhi ya maudhi madogo ya kutumia dawa hii yanayoweza kutokea ni pamoja na :
Kutapika
Maumivu ya tumbo na kichwa
Kizunguzungu
Kuharisha
Mwili kuwasha
Ngozi kuchoma
Ukisahau dozi ya Haloprogin
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-