Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 12:45:21
Dawa ya Isoconazole
Isoconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Albacort
Fomu ya dawa Isoconazole
Isoconazole hupatikana katika mfumo wa krimu wenye ujazo mbalimbali
Namna Isoconazole inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa ya Isoconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi liitwalo Imidazole. Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuharibu kuta za seli ya fangasi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni ya egosteroli, ambapo ni sehemu muhimu katika utengenezaji wa seli ya fangasi.
Dawa zilizo kundi moja na Isoconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: • Bifonazole • Butoconazole • Clotrimazole • Econazole • Fenticonazole • Ketoconazole • Luliconazole • Miconazole • Omoconazole • Oxiconazole • Sertaconazole • Sulconazole • Tioconazole
Kazi ya Isoconazole
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye mfumo wa umeng'enyaji wa chakula uliyosababisha na Kandidiasi
Wagonjwa wasiopaswa kutumua Isoconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao; • Wagonjwa wenye shida ya magonjwa ya Ini
Utofauti wa Isoconazole na dawa zingine zilizo kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (antifangasi aina ya Imidazole): • Dawa hii humeng'enywa na Ini na pia hutolewa mwili kwa njia ya Ini.
Matumizi ya Isoconazole kwa mama mjamzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito • Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Isoconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi ya Isoconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Kichefuchefu • Kutapika • Kuhisi kuungua • Kuwashwa mwili
Ukisahau kutumia dozi ya Isoconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa au kupaka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-