Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Machi 2021 20:44:19
Dawa ya Mebeverine
Mebeverine ni dawa iliyo kwenye kundi la antispasmodic, dawa ambazo hufanya kazi ya kuzuia mijongeo ya misuli laini mwilini inayopeleka kutokea kwa change la tumbo. Dawa hii huwa na kazi ya kuondoa na kuzuia maumivu ya tumbo kutokana na tumbo kunyonga.
Majina mengine na fomu ya dawa mebeverine
Majina mengine ya dawa hii ni Colofac na Aurobeverine. Huweza kupatikana kama yenyewe au mchanganyiko na dawa zingine
Fomu ya mebeverine
Mebeverine hupatikana katika fomu ya kidonge chenye miligramu 135, fomu ya tembe na kimiminika
Namna mebeverine inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuzuia kujongea kwa misuli ya utumbo, hufanya misuli itulie na hivyo kuondoa maumivu yanayotokana na kujongea kwa misuli ya utumbo
Dawa zilizo kundi moja na mebeverine
Dawa zingine kwenye kundi la antispasmodic hujumuisha
Kazi ya dawa mebeverine
Hutumika kuzuia maumivu ya tumbo la chakula yanayotokana na kujongea kwa misuli ya utumbo (kwa jina jingine hufahamika kama change la tumbo)
Hutumika kuzuia dalili za kuharisha kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa syndrome ya inflammatory bowel
Hutumika kutibu maumivu makali ya tumbo
Hutumika kutibu hali ya kuharisha kunakoambatana na tumbo kujaa gezi
Dawa hii inashauriwa kutumika dakika 20 mara baada ya kula, endapo dalili zitaendelea zaidi ya wiki mbili licha ya kutumia dawa hii, unapaswa kuwasiliana na daktari wako kwa uchunguzi zaidi na tiba.
Ufyonzaji na umetaboli wa mebeverine
Ufyonzwaji wa mebeverine
Dawa hii hufyonzwa yote na kwa haraka sana mara baada ya kumezwa.
Umetaboli wa mebeverine
Mara baada ya dawa kuingia mwilini humeng’enywa na homon esterase na kutengeneza viini vinavyofanya kazi yake asili ya dawa na kisha hutolewa kwa njia ya mkojo
Mambo ya kuzingatia kabla ya kutumia mebeverine
Unatakiwa fahamu kuwa, baadhi ya dawa huwa hazitumiki kwa baadhi ya watu. Endapo unataka tumia mebeverine, hakikisha unamwambia mfamasia au daktari wako endapo una kati ya mambo yafuatayo ili akushauri kwamba utumie dawa hii au la;
Wewe ni mjamzito
Una haja kubwa ngumu au hupati haja kwa wakati au kupata shida wakati wa kutoa haja kubwa
Unakunywa dawa zingine mbali na mebeverine
Una mzio na dawa mebeverine
Dawa zenye mwingiliano na mebeverine
1,10-Phenanthroline
2,5-Dimethoxy-4-ethylamphetamine
2,5-Dimethoxy-4-ethylthioamphetamine
4-Bromo-2,5-dimethoxyamphetamine
4-Methoxyamphetamine
5-methoxy-N,N-dimethyltryptamine
7,8-Dichloro-1,2,3,4-tetrahydroisoquinoline
7-Nitroindazole
Abediterol
Acepromazine
Aceprometazine
Acetazolamide
Acetophenazine
Acetylglycinamide chloral hydrate
Acipimox
Aclidinium
Acotiamide
Adenosine
Adinazolam
Adipiplon
Adrafinil
Agmatine
Agomelatine
Ajulemic acid
Alaproclate
Alcuronium
Alendronic acid
Alfaxalone
Alfentanil
Alimemazine
Allobarbital
Alloin
Almotriptan
Alosetron
Alphacetylmethadol
Alphaprodine
Alprazolam
Alprenolol
Aluminium clofibrate
Alverine
Amantadine
Ambenonium
Amibegron
Amineptine
Amiodarone
Amisulpride
Amitraz
Amitriptyline
Amitriptylinoxide
Amobarbital
Amoxapine
Amperozide
Amphetamine
Amphotericin B
Anagrelide
Aniracetam
Anisodamine
Anisotropine methylbromide
APD791
Apomorphine
Aprobarbital
Apronalide
Aprotinin
Arbaclofen Placarbil
Arbutamine
Arformoterol
Aripiprazole
Aripiprazole lauroxil
Articaine
Asenapine
Atomoxetine
Atorvastatin
Atracurium
Atracurium besylate
Atropine
Azaperone
AZD-3043
Azelastine
Baclofen
Bambuterol
Barbexaclone
Barbital
Batefenterol
Beclamide
Benactyzine
Bendroflumethiazide
Benmoxin
Benperidol
Bentazepam
Benzatropine
Benzhydrocodone
Benzilone
Benzocaine
Benzoctamine
Benzodiazepine
Benzphetamine
Benzquinamide
Benzthiazide
Benzyl alcohol
Betaine
Dawa zilizo kundi moja na mebeverine
Dawa zilizo kundi moja la Antispasmodic ikiwa pamoja na mebeverine ni;
Oxybutynin
Dicyclomine
Papaverine
Trihexyphenidyl
Tahadhari kabla ya kutumia mebeverine
Usitumie mebeverine kabla ya kuonana na daktari endapo una hali au mambo yafuatayo
Una umri zaidiya miaka 40
Umejidaidia kinyesi chenye damu
Unajihisi unaumwa au unaumwa
Unaupungufu wa damu au kuishiwa nguvu
Unapata haja ngumu au huendi haja kubwa
Una homa
Unakosa hamu ya kula
Una ujauzito
Unatokwa na damu au uchafu ukeni
Unapata shida kukojoa au maumivu wakati wa kukojoa
Matumizi ya mebeverine kwa mama mjamzito
Hakuna taarifa za kitafiti au zipo chache zinazohusu matumizi ya dawa hii wakati wa ujauzito. Dawa hii itumike endapo faida zakutumia ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza. Hata hivyo dawa hii haishauriwi kutumika wakati wa ujauzito kutokana na kukosekana kwa taarifa za kutosha
Matumizi ya mebeverine kwa mama anayenyonyesha na watoto wadogo
Kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii haifahamiki kama hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, hivyo hakuna taarifa zilizopo zinazofahamika kuhusu madhara yake kwa mtoto. Inashauriwa isitumike kwa mama anayenyonyesha isipokuwa endapo faida za matumizi ni kubwa kuliko madhara.
Matumizi ya mebeverine kwa watoto wadogo
Matumizi kwa watoto chini ya umri wa miaka 18 haishauriwi kutokana na kutokuwa na tafiti za kutosha kuhusu tabia ya dawa kwa watoto.
Maudhi ya mebeverine
Mzio (aleji)
Mzio mkubwa wa anaphylactic
Kuvimba kwa ngozi(urticarial)
Kuvimba kwa uso
Endapo umesahau dozi ya mebeverine ufanyaje?
Endapo umesahau kutumia dozi yako ya mebeverine, acha dozi uliyosahau kisha endelea na dozi nyingine. Usinye dozi mbili kwa wakati mmoja kama ulivyoelekezwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-