Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Julai 2020, 08:50:58
Dawa ya Miconazole
Miconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii iliyo maarufu pia kwa jina la Oravig huwa na rangi nyeupe japo huwa inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza.
Miconazole hupatikana katika mifumo mbalimbali, kidonge na krimu
Fomu ya na uzito wadawa
Miconazole hupatikana kama kidonge huwa na uzito wa miligramu 50 na pia hupatikana pia katika mfumo wa krimu wenye ujazo mbalimbali
Ufanyaji kazi wa miconazole
Dawa jamii ya Antifangasi ikiwa pamoja na Miconazole hufanya kazi zifuatvyo ili kutibu fangasi
Dawa hii ya Miconazole hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli ya fangasi. Miconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni ergosteroli,homoni hii ni muhimu sana kwani huhusika katika utengenezaji wa vijenzi muhimu vya ukita wa seli ya fangasi.
Dawazilizo kundi moja na miconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Fluconazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Ketoconazole
Naftifine hydrochloride
Nystatin
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Mivonazole hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye mfumo wa umeng'enyaji wa chakula uliyosababisha na Kandidiasi
Orodha ya dawa uzitimue na miconazole
Miconazole haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Lorazepam
Amoxicillin / clavulanate
Benadryl
Betamethasone
Clotrimazole
Dexamethasone
Diflucan (fluconazole)
Flagyl (metronidazole)
Flonase (fluticasone nasal)
Fluconazole
Gentamicin
Hydrocortisone
Ketoconazole
Lipitor (atorvastatin)
Metronidazole
NuvaRing
Nystatin
Paracetamol (acetaminophen)
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhari kwa watumiaji
Miconazole inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wenye aleji na dawa nyingine za antifangasi
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;
Dawa hii Nusu ya maisha yake ni masaa 24 na pia hutolewa mwili kwa njia ya mkojo na kinyesi.
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mama ila aishauriwi itumike kwa wamama wanaonyonyesha
Maudhi
Baadhi ya maudhi madogo ya miconazole ni;
Kichefuchefu
Maumivu ya tumbo
Kutapika
Kuharisha
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-