top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

15 Julai 2020 18:42:28

Dawa ya Norethisterone

Dawa ya Norethisterone

Norethisterone ni dawa ya kusanisiwa kizazi cha pili cha progesterone, inayofanana na progesterone inayotengenezwa na mwili, inayotumika kutibu matatizo ya hedhi yanayosababishwa na kuharibika kwa usawia wa homoni mwilini au saratani ya kizazi.


Majina ya kibiashara


Norethisterone hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kama;


  • Activella

  • Alyacen

  • Amabelz

  • Aranelle

  • Aurovela

  • Aygestin

  • Balziva

  • Blisovi

  • Brevicon

  • Briellyn

  • Camila

  • Charlotte

  • Chewable 28 Day

  • Combipatch

  • Cyclafem

  • Cyonanz

  • Dasetta

  • Deblitane

  • Errin

  • Estalis

  • Estrostep Fe

  • Femcon Fe

  • Femhrt

  • Fyavolv

  • Gemmily

  • Generess Fe

  • Hailey

  • Heather

  • Incassia

  • Jencycla

  • Jinteli

  • Junel

  • Kaitlib Fe

  • Larin

  • Layolis Fe

  • Leena

  • Lo Loestrin Fe

  • Loestrin

  • Lolo

  • Lomedia

  • Lopreeza

  • Lupaneta

  • Lyza

  • Melodetta

  • Mibelas

  • Microgestin

  • Mimvey

  • MinEstrin

  • Minastrin

  • Myfembree

  • Necon

  • Nexesta

  • Nora-BE

  • Norlutate

  • Norlyda

  • Norlyroc

  • Nortrel

  • Nylia

  • Oriahnn

  • Ortho Micronor

  • Ortho-novum

  • Philith

  • Pirmella

  • Select

  • Sharobel

  • Synphasic

  • Tarina

  • Tarina Fe

  • Taysofy

  • Taytulla

  • Tilia Fe

  • Tri-legest

  • Tulana

  • Vyfemla

  • Wera

  • Wymzya Fe

  • Zenchent


Namna inavyofanya kazi


Kwenye hatua ya kimolekuli progestin kama norethisterone hufanya kazi kwenye chembe zilizokusudiwa kwa kupitia mlango unaotumiwa na homon progesterone hivyo kupelekea mabadiliko kwenye jeni lengwa.

Chembe lengwa hupatikana kwenye mfumo wa uzazi, titi, tezi pituitary, hypothalamus, tishu za mifupa na mfumo wa kati wa fahamu.

Ufanisi wa dawa za uzazi wa mpango hutokana sana na uwezo wake wa kubadilisha ute wa shingo ya kizazi, hivyo norethisterone huongeza wingi wa chembe na uzito wa ute wkenye shingo ya kizazi na kufanya ugumu wa manii kupenyeza na kuingia kwenye mfumo wa uzazi.


Norethisterone huamsha mabadiliko mbalimbaki kwenye ukuta wa ndani ya kizazi-endometrium, ikiwa pamoja na;


  • Kusinyaa

  • Kuzalishwa pasipo utaratibu

  • Kuzuia uzalishwaji wake


Matokeo ya matendo ya hapo juu ni kupungua kwa uwezo wa yai lililochavushwa kujipandikiza kwenye ukuta wa kizazi na kukua.


Kwa kufanya kazi ya mrejesho hasi, norethisterone hufanya kazi ya kuzuia tezi uzalishaji hypothalamus na pituitaru ya mbele kuzalisha homon kichochezi cha follicle (FSH) na homoni luteinizing (LH). Kupungua kwa uzalishaji wa homon hizi huzuia ukuaji wa foliccle, ovulation na ukuaji wa corpus luteum.


Fomu ya Norethisterone


Norethisterone hupatikana kwenye fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu 5


Umetaboli


Norethisterone hufanyiwa umetaboli kwa hali ya juu kwenye ini haswa na kimeng’enya cha cytochrome P450 na kwa kiasi kidogo na vimeng’enya CYP2C19, CYP1A2 na CYP2A6.


Utolewaji taka mwilini


Asilimia 50 ya taka za norethisterone hutolewa kwa njia ya mkojo wakati asilimia 20-40 hutolewa kupitia kinyesi.


Nusu masha ya dawa


Norestherone huwa na nusu maisha ya masaa 8 hadi 10 kwenye damu.


Utumiaji na chakula


Norestherone inaweza kutumika pamoja na chakula au bila chakula. Matumizi yake na chakula huwa na mwingiliano mdogo usio na mashiko wala kupunguza ufanisi. Hakuna orodha ya chakula chenye mwingiliano na dawa hii kwa sasa.

Magonjwa yanayotibiwa na Norethisterone


Norethisterone hutumika kutibu au kupunguza matatizo yafuatayo;


  • Ukosefu wa hedhi

  • Hedhi yenye maumivu makali

  • Hedhi ya muda mrefu

  • Endometriosis

  • Saratani ya titi

  • Vimbe za fibroidi

  • Kuzuia/kuisubirisha hedhi

  • Kurekebisha mzunguko wa hedhi usioeleweka

  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

  • Kupunguza dalili za hedhi


Dawa zenye mwingiliano


Dawa zenye mwingiliano mkali na norethisterone hivyo kiasi cha kutopaswa kutumika pamoja

  • Abametapir

  • Acitretin

  • Apalutamide

  • Belzutifan

  • Carbamazepine

  • Enzalutamide

  • Fexinidazole

  • Fosphenytoin

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lumacaftor/ivacaftor

  • Mitotane

  • Phenobarbital

  • Phenytoin

  • Primidone

  • Rifabutin

  • Rifampin

  • Rifapentine

  • Topiramate

  • Tucatinib

  • Voxelotor


Dawa zeney mwingiliano mdogo na norethisterone kiasi cha kuhitaji uchunguzi wa karibu kama zitatumika pamoja

  • Albiglutide

  • Atazanavir

  • Cenobamate

  • Clobazam

  • Dabrafenib

  • Elagolix

  • Exenatide injectable solution

  • Exenatide injectable suspension

  • Fedratinib

  • Iloperidone

  • Insulin degludec

  • Insulin degludec/insulin aspart

  • Insulin inhaled

  • Istradefylline

  • Liraglutide

  • Maraviroc

  • Mifepristone

  • Rucaparib

  • Rufinamide

  • Siltuximab

  • Stiripentol

  • Tazemetostat

  • Tecovirimat


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Norethisterone


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wajawazito

  • Wenye Homa ya ini

  • Wenye aleji na dawa hii au chochote kilichotumika kutengeneza dawa hii.

  • Wanaotokwa damu ukeni bila kujulikana sababu

  • Kuwa na kushukiwa na saratani ya titi

  • Wenye thrombosis kwenye mishipa ya ndani ya vein

  • Historia ya au kuwa na magonjwa ya thromboemboliki katika arteri (mfano kiharusi, mayokadia infaksheni)

  • Kuferi kwa ini

  • Wanaotarajia kuwa wajawazito


Wakati gani unapotumia Norethisterone unatakiwa kuchukua tahadhali kubwa?


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wenye msongo wa mawazo

  • Wenye magonjwa ya moyo

  • Wenye kifafa

  • Wenye athma

  • Wenye shida ya figo

  • Wanaotokwa na damu ya hedhi isiyo na mpangilio


Matumizi ya Norethisterone kipindi cha ujauzito


Hairuhusiwi kutumika wakati wa ujauzito.


Matumizi Norethisterone wakati wa kunyonyesha


Hairuhusiwi kutumika wakati wa kunyonyesha. Hata hivyo inaweza kutumika endapo faida ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza


Maudhi ya Norethisterone


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja;


  • Kizunguzungu

  • Msongo wa mawazo

  • Kuongeza au kupungua uzito

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Mwili kuchoka

  • Kushindwa kulala

  • Kupunguza hamu ya kufanya mapenzi


Je kama umesahau kutumia dozi yako ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

bottom of page