Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020 13:15:06
Dawa ya Oxiconazole
Oxiconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Oxistat.
Fomu na uzito wa Oxiconazole
Oxiconazole hupatikana katika mfumo wa krimu wenye ujazo mbalimbali yenye asimilia 1 ya ya kiini cha dawa
Namna Oxiconazole inavyofanya kazi
Dawa ya Oxiconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi aina ya imidazole. Dawa hii huzuia utengenezaji wa homoni ya ergosteroli ambayo huhitajika kwa ajili ya kutengeneza ukuta wa seli ya fangasi.
Dawa zilizo kundi moja na Oxiconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Bifonazole
Butoconazole
Clotrimazole
Econazole
Fenticonazole
Isoconazole
Ketoconazole
Luliconazole
Miconazole
Omoconazole
Oxiconazole
Sertaconazole
Sulconazole
Tioconazole
Kazi ya Oxiconazole
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi aina ya Tinea
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Oxiconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Cisapride
Pimozide
Terfenafine
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine intranasal
Dronedarone
Ergotamine
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Everolimus
Lovastatin
Pimozide
Ranolazine
Silodosin
Simvastatin
Sirolimus
Tolvaptan
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Oxiconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Oxiconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi B ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Oxiconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.
Maudhi ya Oxiconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;
Kupata vipele
Kuhisi kuungua
Kuwashwa mwili
Endapo umesahau dozi ya Oxiconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, paka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-