Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 13:55:03

Dawa ya Ravuconazole
Ravuconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi jamii ya Triazole.
Fomu na uzito wa Ravuconazole
Dawa hii hupatikana kama kidonge chenye miligramu 100
Dawa zilizo kundi moja na Ravuconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Efinaconazole
Epoxiconazole
Isavuconazole
Itraconazole
Posaconazole
Propiconazole
Albaconazole
Terconazole
Voriconazole
Namna Ravuconazole inavyofanya kazi
Dawa ya Ravuconazole hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye kuta za seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu kwenye ukuta wa seli ya fangasi na kufanya ife. Ergosteroli ni aina ya steroli ambayo ni kuu katika ukuta wa seli ya fangasi na ni sehemu ambayo dawa hii hufanya kazi yake na dawa zingine jamii ya Triazole.
Kazi ya dawa Ravuconazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi waliosambaa mwili mzima
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Ravuconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kwa kuwa huwa na mwingiliano wa hatari:
Alfuzosin
Alprazolam
Cobimetinib
Conivaptan
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine intranasal
Disopyramide
Dronedarone
Eliglustat
Flibanserin
Ibutilide
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ravuconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Ravuconazole wakati wa ujauzito
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi ya Ravuconazole wakati wa kunyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya Ravuconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;
Kutapika
Maumivu ya tumbo na kichwa
Kizunguzungu
Kuharisha
Mwili kuwa wa njano
Kuogopa mwanga
Endapo umesahau dozi ya Ravuconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-