Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 14:09:23

Dawa ya Sertaconazole
Sertaconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Ertaczo
Fomu na uzito wa Sertaconazole
Sertaconazole hupatikana katika mfumo wa mafuta yenye
2%
Namna Sertaconazole inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng’enya kinachoitwa saitokromu P-450 ambayo ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda ergosteroli. Hii husababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli kwenye kuta za seli ya fangasi na kusababisha iwe na matundu na kufa
Dawa zilizo kundi moja na Sertaconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Bifonazole
Butoconazole
Clotrimazole
Econazole
Fenticonazole
Isoconazole
Ketoconazole
Luliconazole
Miconazole
Omoconazole
Oxiconazole
Sulconazole
Tioconazole
Kazi ya Sertaconazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi wa ngozi
Wasiopaswa kutumia Sertaconazole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Sertaconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Sertaconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wanaonyonyesha
Maudhi ya Sertaconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;
Ngozi kuwa kavu
Kuhisi kuungua
Kutokwa na vipele
Endapo umesahau kutumia dozi yako ya Sertaconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa au kupaka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-